Bosi Kalewa
Member
- Aug 27, 2022
- 7
- 4
Kitabu cha kiswahili utasoma siku moja au mbili umemaliza. Cha kiingereza utasoma wiki na zaidi na usimalize kamwe. Kwa sababu kiingereza kwetu huumiza kichwa na akili na kuleta kigugumizi.
Hata totozi ikiwa na viingereza vingi wanaume hupunguza kujiamini. Sasa kwanini tutumie kiingereza kuelimishia watoto ngazi ya sekondari tu? Maarifa si ni yaleyale iwe kwa kiingereza ama kiswahili?
Mateso haya hufanya watoto wakose hamu ya kuendelea na sekondari. Hata wanaendelea wengi hufeli ama kukariri tu bila kuelimika. Sasa kwanini kesi hii tunaihalalisha kiwa ya kitaifa?
Tumepotea na tunaona wavivu kurudi nyuma. Miaka saba ni kiswahili, katika umri mzuri wa watoto kukariri kila kitu. Kisha ghafla tunatumia kiingereza tena ukubwani wakiwa wamekomaa? Hii siyo sawa.
Tunajimwambafai Kiswahili ni lugha ya taifa. Ofisi za umma majina ya lugha ngeni tupu. TCRA, TBS, NHC, TPA, TRA, NSSF, TACAIDS, TBL, TRC, TASAF, SIDO, TANESCO nk. Yote haya kirefu chake ni kiingereza kile cha ndani ndani kabisa.
Hata vyeo serikalini kiingereza mwanzo mwisho. CAG, IGP, DCI, DPP, RC, DC, DED, RAS, DAS, RTO na OCD yaani mpaka nachoka. Utadhani hii nchi ni ya Waingereza wengi kuliko Waswahili.
Tunazalisha kizazi cha kuamini lugha ngeni ndo maendeleo. Na watoto wetu kushindwa kwenye ushindani wa ajira na wageni tena majirani zetu. Wabunge kimya, wanaharakati kimya, wanasiasa kimya, wanahabari kimya. Tunaacha gari liende bila mafuta.