Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Nimekaa na kutafakari kwa kina tunu ya lugha yetu hii ya Kiswahili.
Kiswahili kilitumika katika kuleta uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Kiswahili kilitumika kuunganisha makabila zaidi ya 120 yaliyopo Tanzania.
Kiswahili kilitumika kumng'oa Nduli Idd Amini Dadaa, alipojaribu kuivamia Tanzania.
Kamuzu Banda wa Malawi naye alijaribu kumega kipande cha kusini mwa Tanzania lakini alishindwa.
Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yalifanikiwa kwa sababu ya lugha hii adhimu ya kiswahili.
Kiswahili kimekuwa lugha ya umoja, ukombozi na silaha dhidi ya adui.
Katika mapambano ya gonjwa hili la Corona, gonjwa ambalo linadidimiza uchumi wa nchi zetu za uchumi wa kati. Lengo kubwa la gonjwa hili ni kuhakikisha ukoloni mambo leo unaendelea. Kuzifanya nchi changa ziendelee kuwa tegemezi huku watu wachache wakifaidi.
Kiswahili kimeibuka kidedea baada ya kutumika inavyotakiwa ili kufikisha ujumbe kwa jamii ya Waswahili na kuwaunganisha pamoja.
Siri hii ni kubwa mno wengi hawajui nguvu ya maamuzi, yakisukumwa na lugha ya Kiswahili.
Tukitunze na tukipende. Majirani siri kubwa ya kuweza kuondokana na janga hili, mwambieni kiongozi wenu mkuu aanze kuwasiliana na watu wake kwa kutumia Kiswahili.