KISWAHILI SOUTH AFRIKA KINAZUNGUMZWA MAENEO YAPI

KISWAHILI SOUTH AFRIKA KINAZUNGUMZWA MAENEO YAPI

Ukaridayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
515
Reaction score
476
Wakuu habr zenu,

imenilazimu nije hapa kuuliza hilo swali hapo juu kwasababu ninajua humu ndani tupo watu tofauti tofauti ktk kushare ideas pamoja na kuelimishana..

Mara nyingi mimi huwa ni mpenzi wa kusikiliza nyimbo za south afrika kama kwaito vile, gwara gwara n.k, nilichogundua ktk nyimbo zao hawa mabwana yani ni lazima utakuta maneno mawili ama hata robo ya verse ipo ktk kiswahili..

hata wale joyce celebration nao huwa ktk gospal zao kipo kiswahili..

nauliza huko south kiswahili kinazungumzwa maeneo yapi..na je kwa mswahili aliyepo hapo south kiswahili anakitumiaje?
 
South Africa ina watu wengi sana wanaotoka Afrika mashariki ikiwemo Congo (DRC). Hawa wote wakiwa wakikutana huzungumza Kiswahili, maana ndo fahari yenyewe!

Lakini "Wasouth" Kama wao hawana wazungumzaji wa kiswahili labda wale waliowahi kuishi Tanzania ikiwemo wale wakimbizi na wapigania uhuru.

Kusikia maneno ya Kiswahili kwenye nyimbo ni jambo LA kawaida, wasanii wengi huwa wanataka kulifikia soko pana zaidi LA wasikilizaji. Hata Michael Jackson ana wimbo wake mmoja anachanganya na Kiswahili.
 
Dimela.
nadhani kama ni kwenye nyimbo itakuwa ni ujanja tu wa msanii.
 
South Africa ina watu wengi sana wanaotoka Afrika mashariki ikiwemo Congo (DRC). Hawa wote wakiwa wakikutana huzungumza Kiswahili, maana ndo fahari yenyewe!

Lakini "Wasouth" Kama wao hawana wazungumzaji wa kiswahili labda wale waliowahi kuishi Tanzania ikiwemo wale wakimbizi na wapigania uhuru.

Kusikia maneno ya Kiswahili kwenye nyimbo ni jambo LA kawaida, wasanii wengi huwa wanataka kulifikia soko pana zaidi LA wasikilizaji. Hata Michael Jackson ana wimbo wake mmoja anachanganya na Kiswahili.

Naomba nikurekebishe kidogo, kuna watu wanaitwa "wazanzibar" huko Afrika ya Kusini, hawa asili yao walitokea Zanzibar enzi za utumwa na kuishia karibu na Durban, wanazungumza kiswahili tena Safi na lafdhi yao ya kiunguja na Wala sio Watanzania. Pia wanazungumza kimakua , kwani walitekwa Umakuani na kuuzwa Zanzibar na hatimaye kufikia CHATSWORTH , karibu na Durban.

Islam among the Zanzibaris of South Africa on JSTOR

https://www.google.com/search?ie=UT...are+south+African+Zanzibaris+speaking+Swahili[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom