South Africa ina watu wengi sana wanaotoka Afrika mashariki ikiwemo Congo (DRC). Hawa wote wakiwa wakikutana huzungumza Kiswahili, maana ndo fahari yenyewe!
Lakini "Wasouth" Kama wao hawana wazungumzaji wa kiswahili labda wale waliowahi kuishi Tanzania ikiwemo wale wakimbizi na wapigania uhuru.
Kusikia maneno ya Kiswahili kwenye nyimbo ni jambo LA kawaida, wasanii wengi huwa wanataka kulifikia soko pana zaidi LA wasikilizaji. Hata Michael Jackson ana wimbo wake mmoja anachanganya na Kiswahili.