Kitaalam, alichomaanisha Polepole ni hiki

Wapuuzi sana hawa watu mwaka jana wakati wa uandikishaji wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa ulihitimishwa saa kumi jioni na kesho yake alfajiri Mchengerwa anatangaza idadi ya watu waliojiandikisha kwa nchi nzima, hawana hata mishipa ya aibu kuongopa.
 
Marehemu kupiga kura kwa Tz hapa ni kawaida sana
 
Mshipa wa aibu ulishakatika. Walishawaona watanzania ni wajinga.
 
Polepole sio wa kumwamini sana.
 
Mkuu asante kwa kuniwahi kulielezea hili jambo. Bado nilikuwa kwenye tafakari nzito baada ya kusoma ujumbe wa NEC walioutoa leo kukanusha alichoongea POLEPOLE mtu ambaye alishawahi kuwa mtendaji mkuu wa chama cha CCM. Hili si jambo la kulipuuzia hata kidogo, watanzania tutaonekana mazumbukuku kama hii disclosed information haitafanyiwa kazi. Tusishangae kwanini wakuu wa vyombo vya ulinzi wanabadirishwa mara kwa mara especially idara yetu pendwa inayotakiwa kuangaza jicho nchi nzima ili kuzima vitisho na hatari yoyote juu ya watanzania na nchi yao.
Poor my country...๐Ÿ˜ฐ
 
INEC: ^Mfumo wetu wa kupiga kura ni wa manualโ€ฆ^ ^Hakuna kura za kielekroniki.^
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Aliye na kadi ya mpiga kura ambaye ni marehemu aingize kwenye uhakika sone kama haitasoma!
 
Hizi ndizo sababu 5 kwanini tumchague Rais Samia:


  1. Kiongozi mwenye dira na hekima โ€“ Ameonyesha uongozi wa utulivu, busara na maamuzi yenye kulinda maslahi ya Watanzania.
  2. Mageuzi ya kiuchumi โ€“ Amefungua Tanzania kimataifa, kuongeza uwekezaji na kusimamia miradi mikubwa ya kimkakati inayoongeza ajira na mapato ya taifa.
  3. Kuboresha huduma za jamii โ€“ Amewekeza kwenye elimu bila ada, afya bora, maji safi na nishati vijijini ili kuinua maisha ya wananchi.
  4. Kuimarisha mshikamano wa kitaifa โ€“ Ni kiongozi anayeunganisha Watanzania, kusikiliza sauti za wananchi na kushirikisha makundi yote katika maamuzi ya kitaifa.
  5. Ushirikiano wa kimataifa โ€“ Ameimarisha diplomasia ya uchumi na heshima ya Tanzania duniani, kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha fursa na maendeleo.
 
Sasa siku ya kupiga kura, sababu unaamini huna vigezo, hautatokea kituoni, ila wakija kuhesabu baadae ( baada ya kuongeza box za kura feki ambazo zitakua na kura zenye taarifa halali kutoka NEC ) utajikuta upo katika orodha ya watu waliopiga kura
Duh,
Hatari sana hao wahuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ