Kitabibu, inawezekana kutokulala kwa week 6?

Troll JF

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
7,804
Reaction score
12,237
Wadau Mkuu wa Kambi moja ya jeshi alikua akisoma Risala na Kusema vijana hawa wamefaulu mafunzo ya Jeshi Ikiwemo Kutokulala kwa week 6.

Wakuu kitabibu hiki kitu kinawezakana? Je Mtu hawezi kuanguka kwa sababu ya Fatigue? muda huo wa week 6 huwa wanafanya nini hasa.
 
mtakimbia,mtabeba na kurushiana logs,mtapiga push up,mtaimba ila si nyimbo za kina diamond
 
inawezekana...ila utalala ukiwa umesimama aisee au ukitembea!
 
Mtu akikosa kulala kwa mda wa siku tatu mfululizo anakuwa mwehu
 
Ha ha ha..ndani ya wiki sita sio siku zote unakesha "mwanzo mwinga" jicho.Kuna viepisodes vya usingizi ila vifupi sana,kama dakika kumi hadi nusu saa kwa afande mpole

Ila inawezekana mtu akamaliza wiki sita akiwa amelala muda mfupi sana na hii ndio siri ya macho mekundu ya makamanda

Na ni ukweli kuwa kuna wengine huwa wanapata psychotic disturbances kama kuwehuka kidogo ila baadae wanakuwa vizuri

Sitosahau nilipopoteza channel siku ile ya mchaka mchaka tumeondoka vizuri chenja ya F Coy tunaenda Myobozi najikuta nipo uwanja wa damu halafu sijui nimefika.....ilikua 821 KJ Kigoma
 
Hiyo inawezekana ila kunawengine wanawehuka, kijeshi wanaita "NET" sisi tulipiga six week kisha commandant akatuongeza wiki mbili. ilikua mgambo jkt tanga
 
Sikuizi jkt mafinga naskia hawapigi six weeks pia hata hawapigwi nua kwasababu ya baridi.
 
Mtu akikosa kulala kwa mda wa siku tatu mfululizo anakuwa mwehu


Acha uongo mkuuu! Mie nishapiga 3weeks mfululizo ila siku ya kulala nilikua nalala mda wote mpaka mwili ukachoka
 
Mnasiniza tu lakini siyo kulala mpaka unaota au unakoroma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…