Jamani wana Familia ya JF, mimi kichenchele naomba kutoa yaliyo yangu maoni juu ya huu uwanja ambao tumekuwa tukipata taarifa/habari juu ya maswala mbalimbali yahusuyo maisha yetu kama Watanzania, Waafrica, wasomi, weledi, na watu wa kada mbalimbali, nashukuru sana kwa hilo, inaniwia vigumu sana kuamini, kama tunataka kuugeuza uwanja huu kuwa mahala pa kutoa matusi na kutukanana bila haya na kusahau kuelimishana na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wa kimawazo. ukweli haiingii akilini kuona mtu anadiriki kuandika lugha isiyo na nidhamu kwa mwanachama mwenzake, nafikiri kama mtu amekosea tumsaidie kumwelewesha juu ya kile alichokosea, naamini hapa kuna watu wazima na waelewa wa maswala mbalimbali yanayozunguka jamii yetu na jamii za kimataifa, ila kama tutaonekana kutothamini umuhimu wa watu kuwa ktk huu uwanja ukweli wengi watashindwa kutoa misaada yao kimawazo kwa kuwa wataona watu tuliomo JF wengi ni wahuni kitu ambacho si kizuri hata kidogo, nachofahamu mimi JF ni sehemu nzuri sana ya kupata taarifa za kila aina za matukio yanayotokea kila siku za maisha yetu, hali ambayo inamsaidia hata yule asiyeweza kununuwa gazeti kupata taarifa sahihi au kama umesahau kununuwa gazeti JF inaweza ikakuhabarisha. Watanzania wenzangu nawaombeni wale wenye tabia ya kutukana wenzao tuache jamani si vizuri kutukanana hadharani, hata kama majina yetu si halisi lakini ukishazoea kuutukana ukuta wa nyumba ipo siku utakuja kutukana kiumbe aina ya mwanadamu, tupendane, tusaidiane, tushirikishane, tueleweshane, tusahihishane,tuelimishane ili mwisho wa siku tuweze kuwa na jamii elevu na yenye kupata taarifa zilizo sahihi.Watanzania wengi tunahitaji kupata msaada wa kimawazo toka kwa watu mbalimbali waliomo JF, tuitumie kwa manufaa. matusi si mazuri, ukimtukana mwenzio ni sawa na kumvua nguo hadharani.