Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KITABU CHA MAISHA YA KANALI AYUBU SIMBA
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka wa 1988 katika kuadhimisha Miaka 30 ya Azimio la Busara Tabora alisema CCM iwatafute wale wote walioingia TANU kati ya waka wa 1954 – 1958 kwani kipindi kile kilikuwa kipindi kigumu sana.
Kanali Ayubu Simba ni mmoja wa wazalendo hawa na alikuwa mjumbe katika mkutano wa Tabora kujadlli Kura Tatu na alikuwa kijana mdogo sana.
Mwalimu aliyasema maneno haya baada ya Ramadhani Singo mmoja wa vijana waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika kumkabili Mwalimu na kumwambia mbona chama kimekuwa mwizi wa fadhila kwa kuwasahau wote waliojitolea kukitumikia wakati wa kupigania uhuru?
Maneno mazito lakini yana ukweli ndani yake.
Wakati Mwalimu alimjua Singo mwaka wa 1958 wakati wa Mkutano wa Kura Tatu Tabora kujadili TANU kuingia Uchaguzi wa Kura Tatu au kususa.
Ramadhani Singo alikuwa kijana mdogo wa miaka 24.
Singo ndiye alikuwa mlinzi wake akilala usiku nje ya nyumba aliyofikia Nyerere kumlinda.
Mwalimu alipomuona Singo Tabora mwaka wa 88, Singo alikuwa mzee na kachoka kwa kupigwa na maisha.
Hakuwa peke yake wanachama wa TANU ile ya mwaka wa 1954 waliletwa mbele yake wasalimiane na Baba wa Taifa.
Mwalimu aliziona hali zao na alihisi vibaya.
Katika hotuba yake baada ya pale aliwaadhimisha wale walioingia TANU siku zile za awali.
Kanali Simba jina lake lake la Simba limesibu ushujaa wake,
Kanali Simba hana tofauti na Simba Mfalme wa Porini.
Nimemaliza kukisoma kitabu cha Kanali Ayubu Simba, ‘’Tenda Wema Nenda Zako Usingoje Shukurani.''
Kanali Simba ni miongoni mwa vijana mfano wa Ramadhani Singo na Abdallah Said Kassongo ambao nishawataja hapa waliofanya makubwa katika kuitumikia TANU kwa kujitolea.
Kama Kanali Ayubu Simba asingenyanyua kalamu na kuandika kumbukumbu zake hakuna mtu angejua mchango wake kwa taifa hili.
Jina lake lingepita kama yalivyopita majina mengi ya wapigania uhuru wa Tanganyika.
Unapofungua kitabu hiki ni sawa na kuwa jumekaa kwenye kiti cha mbele unatazama senema nzuri iliyojaa mikasa.
Utamwona kijana Ayubu Simba akijitahidi kusoma masomo kwa njia ya posta akijaribu kuipata elimu ambayo hakujaaliwa kuwa nayo.
Miaka hiyo elimu hii ikitolewa na British Tutorial College (BTC) ya Uingereza.
Utamwona kijana Ayubu Simba akifanya kazi kwa makampuni ya Kiingereza na kuhimili kila aina ya shida ya makampuni hayo ya Wazungu kwa Waafrika.
Utamwona kijana Ayubu Simba anaacha kazi ya mshahara anaingia TANU kufanya kazi isiyo na mshahara kupigania uhuru wa Tanganyika.
Utamwona kijana Ayubu Simba akisafari kwa miguu na wakati mwingine kwa baiskeli kutoka kijiji kimoja hadi kingine mchana na wakati mwingine usiku akipita porini kuwafuata wananchi kuwaingiza katika chama cha TANU na kuwaamsha wasimame kwa umoja wao wadai uhuru wa nchi yao.
Kijana mdogo Ayubu Simba analala juu ya miti kukimbia wanyama wakali akiwa porini katika kupigania uhuru.
Kijana Ayubu Simba anakirimiwa na wananchi wenzake na wazalendo huko vijijini kumsaidia katika kazi ambayo wao kama wananchi chini ya ukoloni wanaiunga mkono.
Utamsoma Ayubu Simba katika hali yake halisi ya ‘’Askari wa Miguu,’’ hata kabla hajaingia katika JWTZ.
Kupitia kitabu hiki cha maisha yake msomaji utapata fursa ya kuwajua wazalendo wengi ambao hawafahamiki wala hawajapata kutajwa katika histori ya uhuru wa Tanganyika.
Katika hawa kuna wazalendo na maadui wa wazalendo.
Kanali Ayubu Simba atakufikisha kwa Ivor Bayldon Mzungu tajiri na muasisi wa United Tanganyika Party (UTP) chama cha Wazungu kilichokuwa kinapinga TANU.
Kupitia kalamu ya Kanali Ayubu Simba atakukutanisha na Mohamed Kissoky, Abbas Max, Mbuta Milambo, Bi. Zaituni Matola, Dr. Wilbard Mwanjisi, Madestus Choga, Dr. Michael Lugazia na Robert Mwakitwange.
Hawa ndiyo walikuwa miamba ya siasa Nyanda za Juu wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Katika orodha hii walikuja kuwapo maadui wa Nyerere wakapambana na yeye katika Tanganyika huru.
Ukikitia mkononi kitabu hiki hutakiweka chini hadi umefika ukurasa wa mwisho.
Kanali Ayubu Simba katufanyia ikhsani na kheri kubwa kutuandikia maisha yake katika kitabu hiki ambacho kimeongeza elimu kubwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.