Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Utangulizi
Maisha ya mwanadamu, yana sehemu kuu tatu:-
Maisha ya mwanadamu, yana sehemu kuu tatu:-
- Kuzaliwa
- Kuishi
- Kufa
Sura 1: Kuzaliwa
- Mtu anazaliwa pale panapokuwa na uhusiano wa kimapenzi, kati ya mwanaume na mwanamke.
- Na uhusiano huo uleta ujauzito na baada ya miezi 9 mtoto uzaliwa.
- Na tukio hili hutokea mara moja
Sura 2: Kuishi
- Mtoto akishazaliwa, upitia malezi mbalimbali, pamoja na kupata elimu stahiki, itakayomuwezesha kuishi katika jamii.
- Kutofautiana kwa malezi, na elimu; kutoka kwa familia moja kwenda nyingine; kunasabisha kuwa na watu wenye tabia na mitazamo tofauti.
- Mitazamo hasi:-
- Ujambazi
- Uhuni
- Uzurumaji/utapeli
- Unafiki/uongo
- Ubinafsi
- Uchawi
- Ushoga
- Chuki
- Ujilimbikiziaji wa mali
- Tamaa n.k
- Mitazamo chanya:-
- Ustaarabu
- Kujali wengine
- Unyenyekevu
- Kupenda wengine wafanikiwe n.k
- Ni kipindi ambacho binadamu ataishi kwa furaha, pia ni kipindi ambacho ataishi kwa huzuni.
- Ni kipindi ambacho, watu uishi huku wakidharauliana; na mwingine kujiona bora zaidi kuliko mwingine; ni 'full' kukanyagana.
- Kutokana na viungo kuchoka, ulaji wa vyakula, umri mkubwa, magonjwa nyemelezi n.k; binadamu uanza kudhoofika.
Sura 3: Kufa
- Hii ni hatua ya mwisho, inayofunga kitabu cha binadamu, na kubaki kuwa historia kwa waliobaki.
- Na hii utokea mara moja tu.
- Kama alitenda mema atakumbukwa kwa mema, na kama hakutenda mema atakumbukwa kwa aliyoyafanya.
- Mali zote alizozitafuta, ataziacha; na mwili tu ndio utakao-ifadhiwa.
Mwisho
Nilichojifunza katika hiki kitabu, wote tulio hai leo; tupo kwenye sura 2, na wengi huwa tunajisahau kuwa hatutafika sura 3.
Ukijua sura 3 lazima ufike, itakusaidia kuishi vizuri katika sura 2; haya mambo ya kukanyagana katika sura ya 2 yatapungua.
Swali: Sura 2 kwako ikoje?
Nilichojifunza katika hiki kitabu, wote tulio hai leo; tupo kwenye sura 2, na wengi huwa tunajisahau kuwa hatutafika sura 3.
Ukijua sura 3 lazima ufike, itakusaidia kuishi vizuri katika sura 2; haya mambo ya kukanyagana katika sura ya 2 yatapungua.
Swali: Sura 2 kwako ikoje?