Kitabu cha Sheikh Ponda "Juhudi na changamoto" kiko madukani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITABU CHA SHEIKH PONDA KATIKA MADUKA YA KUUZA VITABU

Kitabu cha Sheikh Ponda ''Juhudi na Changamoto Kinapatikana Ibn Hazm Media Centre katika maduka yao ya kuuza vitabu yaliyopo katika Misikiti ya Mtoro, Manyema (Kariakoo) na Mtambani (Kinondoni).

Kitabu In Shaa Allah kitapatikana mikoa yote ya Tanzania.

Bei Shs: 15,000

1662546665241.png
 
Mkuu tupe intro ya maudhui yaliyomo ili tukivutiwa nayo tununue kitabu
 
Gunst,
Sheikh Ponda haitaji kuandikiwa maudhui ya kitabu chake ili kinunulike.
Jina lake linatosha.

Lakini kwa kuwa umetaka maudhui ya kitabu sikiiza hiyo video hapo chini:

Naunga mkono hoja
''Siku Sheikh Ponda aliponiletea kitabu chake, ''Juhudi na Changamoto,'' nilimwambia, ''Ndugu yangu sasa umeingia umeingia katika dunia nyingine mpya kwako maisha yako hayatakuwa kama yale uliyozoea unaingia katika nchi hujapatapo kufika wala kuifikiria akilini kwako.''

Nimaeyasema haya wakati sikuwa najua kuwa Sheikh Ponda tayari kaandika vitabu 16.

Vitabu 16.

Vitabu 16 na vingine unakiogopa kitabu kwa kusikia jina lake tu ukaanza kujitisha mwenyewe.

Nani shujaa na jasiri kiasi akitajiwa Dr. John Sivalon asishtuke hata kidogo akitajiwa kuwa kuna kitabu kimeandikwa na Sheikh ponda kuhusu Dr. Sivalon.
Au akitajiwa kitabu cha ''Masheikh Gerezani,'' ''Waislam na Mkono wa Dola,'' ''Pitio la Zanzibar.''

Sheikh Ponda katufanyia kazi kubwa sana.
Kalamu ya Sheikh Ponda imetufungulia ukweli.

Sahib yangu na wengine mfano wake ambao hawakuwa wanaijua Tanzania vitabu hivi vitawasaidia kuijua nchi yetu na siasa zake.

Kweli Tanzania ni kisiwa cha amani?
Amani inawezaje kuwapo mahali pasipo usawa wala haki?

Soma kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''
Kuna mengi ya kufikirisha.''
 
Asante sana mzee wangu Mohamed Said kwa nyongeza hii. Umenifanya nizidi kupata kiu ya kutafuta vitabu vya mpambanaji Sheikh Ponda
 
Ni matumaini yangu serikali imekikagu vya kutosha kabla ya kuruhusu kuuzwa kisilete chuki kwa jamii
 
Back
Top Bottom