''Siku Sheikh Ponda aliponiletea kitabu chake, ''Juhudi na Changamoto,'' nilimwambia, ''Ndugu yangu sasa umeingia umeingia katika dunia nyingine mpya kwako maisha yako hayatakuwa kama yale uliyozoea unaingia katika nchi hujapatapo kufika wala kuifikiria akilini kwako.''
Nimaeyasema haya wakati sikuwa najua kuwa Sheikh Ponda tayari kaandika vitabu 16.
Vitabu 16.
Vitabu 16 na vingine unakiogopa kitabu kwa kusikia jina lake tu ukaanza kujitisha mwenyewe.
Nani shujaa na jasiri kiasi akitajiwa Dr. John Sivalon asishtuke hata kidogo akitajiwa kuwa kuna kitabu kimeandikwa na Sheikh ponda kuhusu Dr. Sivalon.
Au akitajiwa kitabu cha ''Masheikh Gerezani,'' ''Waislam na Mkono wa Dola,'' ''Pitio la Zanzibar.''
Sheikh Ponda katufanyia kazi kubwa sana.
Kalamu ya Sheikh Ponda imetufungulia ukweli.
Sahib yangu na wengine mfano wake ambao hawakuwa wanaijua Tanzania vitabu hivi vitawasaidia kuijua nchi yetu na siasa zake.
Kweli Tanzania ni kisiwa cha amani?
Amani inawezaje kuwapo mahali pasipo usawa wala haki?
Soma kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''
Kuna mengi ya kufikirisha.''