Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 4,460
- 13,715
Kitabu kinaitwa TOBA na kimeandikwa na Mai Godrey.
Ni kitabu chenye sala za TOBA za aina nyingi ambazo ukizisali kwa Imani na utulivu unatengeneza ukaribu na Mungu wako.
Kuna wakati nilipitia changamoto nzito na nikachagua moja ya sala za TOBA kwa siku 21 nikawa naamka saa 8 usiku na pia nikaandika vifungu vya biblia vinavyoendana na shida yangu ambavyo nilivisimamia asubuhi na mchana nikiviunganisha na maombi.
Kuna wakati nilimuomba Mungu na anioneshe nini chanzo cha shida yangu akafanya hivyo na pia Kuna wakati nilimuuliza Mungu makusudi yake kwangu akanipa maono flani hivi.
Pia unapaswa Katika sala hii uache anasa zote kama ngono, ulevi, vijiwe vya stori za umbea na matusi, nk ili uwe msafi.
WAKUU nilimuahidi Mungu atakapo nitendea Makuu na nitashare na watu hiki kitabu ili nao wamfiikie yeye kwa kwa maombi na kumlimlia.
Sasa kwa kuwa amenitendea Makuu basi hauna budi na wewe pia kumuomba Mungu aliejaa utukufu.
MUWE NA SIKU NJEMA, MUNGU ATUKUZWE MILELE.