Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KITABU "JUHUDI NA CHANGAMOTO" SHEIKH PONDA NA SUALA LA ELIMU
Siku moja Sheikh Ponda kanipigia simu akaniambia kuwa wamefungua shule na ananialika hapo shuleni nizungumze na wanafunzi.
Mimi sikuwa na taarifa ya haya kumbe shule imefunguliwa muda mrefu.
Hapo shuleni kuna msikiti mkubwa naingia msikitini naukuta msikiti umejaa wanafunzi.
Vijana wa kiume wamekaa mbele na dada zao wakiwa katika hijab wamejipanga nyuma.
Mbele nawaona waalimu wao wamejipanga kulia na kushoto kwangu.
Katikati ya umma huu kasimama mpiga video.
Najisemea kimoyomoyo kumbe hii shughuli kubwa.
Aliponipa mwaliko Sheikh Ponda aliniambia nizungumze na wanafunzi niwafunze historia ya kweli ya Tanganyika nikiweka msisitizo katika juhudi za Waislam wa wakati ule katika elimu na vikwazo walivyowekewa na wakoloni na kisha serikali iliyokuja kushika madaraka baada ya wakoloni kuondolewa na nchi kuwa mikononi kwetu wenyewe wananchi..
Sheikh Ponda akanisisitizia kuwa kuna propaganda kubwa inaenezwa kuwa Waislam hawathamini elimu na ndiyo maana wako nyuma.
Wanatangaza kuwa Waislam hatupendi shule tunapeleka watoto madrasa na haya wanayasema kinywa kipana na kwa kebehi.
"Ndugu yangu njoo usafishe bongo za vijana wetu hawa wajue ukweli kwani huu ukweli utawapa nguvu ya wao kujitambua na hii italinda heshima yao na heshima yetu sisi wazazi wao."
Nimesimama pale msikiti mbele ya kibla nawaangalia wanafunzi waliokuwa mbele yangu nahisi kuna kitu kimepanda kwenye koromero na machozi kama yanataka kunitoka.
Namkumbuka Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na juhudi zake chini ya Daawat Islamiyya za kuwahamasisha Waislam kujenga shule wakati wa ukoloni na hata baada ya ukoloni kuondoka Tanganyika.
Na ni juhudi hizi ndizo zilizomfanya afukuzwe Tanganyika arejeshwe kwao Zanzibar.
Huyu Sheikh Ponda huyu...
Msikiti uko kimya kabisa.
Nilishatambulishwa.
Hadhira inanisubiri mimi nianze kuzungumza.
Fikra za Sheikh Hassan bin Ameir na Ponda na ule umma uliokusanyika pale ndiyo ulionitoa pale nikiwa kama nimeduwaa.
Akili imerejea mahali pake.
Nasoma dua ya Nabii Mussa kimoyomoyo kisha nafungua kinywa kuzungumza.
Naanza kwa kueleza kuwa Waislam ndiyo jamii ya kwanza Pwani ya Afrika ya Mashariki kujua kusoma na kuandika kupitia madrasa.
Uislam uliingia Pwani ya Afrika ya Mashariki pamoja na elimu.
Waislam wakawa ndiyo watu wa kwanza kujua Kusoma, Kuandika na Hisabati.
Kipindi cha maswali na majibu hakika kilinifurahisha.
Somo lilikuwa limeeleweka.
Vijana wanauliza imekuwaje wanafundisha historia isiyo ya kweli?
Sheikh Ponda sasa kuwa ana shule anasomesha ikawa yale aliyokuwa anayasikia kuwa kuna mfumo uliojengwa wa kuwahujumu Waislam katika elimu sasa yakawa yanamkabili usoni moja kwa moja.
Changamoto hii ndiyo ikawa inafungua sura ya kwanza ya kitabu.
Kweli imedhihiri.