Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hashil Seif ameifanyia hisani kubwa sana historia ya Zanzibar kwa kueleza uongozi wa Abdulrahmani Babu katika kupigania uhuru wa Zanzibar na katika kuweka msingi wa mapinduzi.
Hashil Seif anasema Babu alimuathir zaidi katika maisha yake ya kutafuta kuleta mabadiliko visiwani na akamaliza kwa kusema kuwa hapajatokea kiongozi Zanzibar ambae anaweza akalinganishwa na uwezo aliokuwanao Babu.
Hashil anamsifia Babu kwa kusema kuwa ‘’bongo,’’ lake halikuwa la kawaida.
Nilipokianza kukisoma kitabu hiki hata kabla sijafika mbali ikawa imeshanidhihirikia kuwa mikononi mwangu nimeshika kitabu kinachofungua mengi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar na kwa ile harara yangu sikuweza kustahamili mara moja niliandika patio fupi kwa kile nilichokisoma na kukiweka katika mtandao na nikawaahidi wasomaji wangu In Shaa Allah nitarejea nitakapokimaliza kitabu.
Huenda ni hili patio langu ndilo lililosababisha hii leo mimi kuwa hapa mbele yenu kwani haikuchukua muda baada ya kukiweka kitabu mtandaoni ikawa ghafla kitabu kikafahamika, kikapata umaarufu na kikawa kinaulizwa; na kama kawaida linapokuja suala la Zanzibar malumbano yakaanza na mjadala ukawa unakwenda kwa kasi lakini bila ya wanaojadiliana kuwa wamekisoma kitabu.
Wengi walibakia na zile zile rejea zao za kale ambazo zingine ni shida kutambua ipi ni ‘’fact,’’ na ipi, ni ‘’fiction,’’ yaani upi ukweli na upi uongo.
Moto ukawaka.
Katikati ya mjadala nikaletewa mtandaoni picha ya Hashil Seif na wenzake wawili, Amour Dugheshi na Mussa Maisara wamebeba bunduki.
Yawezekana kwa baadhi picha hii ilinogesha kumbukumbu za mapinduzi na mchango wa makomredi na jinsi Hashil Seif na Amour Dugheshi walivyomshughulikia Field Marshall John Okello na kumfurusha visiwani.
Haukupita muda nikaletewa picha nyingine akiwamo Khamis Abdallah Ameir, Badawi Qullatein na Hashil Seif.
Kwangu mimi hizi picha zikaongeza mengi katika kukielewa kitabu cha Hashil Seif na nafasi ya Umma Party katika historia ya mapinduzi kwani picha husema maneno elfu.
Nilipoangalia picha ya Hashil Seif amebeba silaha na kusoma kuhusu mafunzo ambayo vijana wa Umma Party waliyapata Cuba wakati wa kupigania uhuru nilielewa kwa nini siku za mwanzoni za mapinduzi hawa vijana ndiyo walikuwa walinzi wa mapinduzi na wangejenga uti wa mgongo wa Jeshi la Zanzibar ingekuwa hapangekuwa na muungano na Tanganyika.
Hashil Seif ameeleza toka mwanzo nia ya makomredi kupindua serikali yoyote Zanzibar isiyokuwa yao na kuweka utawala utakaofuata siasa za ki-Marxist.
Haiwezekani kuwa na serikali kama hii bila ya jeshi madhubuti.
Sijui kwa nini Hashil Seif katika kitabu kizima hili hakugusia ingawa kaeleza mengi juu ya masikitiko yake kwa kuona mapinduzi hayakwenda kama walivyotegemea ingawa kaeleza kuwa laiti ushauri wa Babu kwa viongozi wenzake katika ZNP ungelifuatwa, basi mapinduzi yasingelitokea.
Hashil Seif ameeleza mgongano uliokuwapo ndani ya ZNP kati ya Babu na Ali Muhsin uliopelekea Babu kujitoa ZNP na kuunda Umma Party.
Hashil katika sintofahamu hii anaeleza kile anachokiita njama baina ya Waingereza na viongozi wahafidhina ndani ya ZNP kumfunga Babu jela kitu ambacho walifanikiwa. Hashil Seif anaeleza karoti aliyowekewa farasi mdomoni kummaliza Babu.
Hakika katika simulizi hii Hashil Seif kaeleza mengi ya kufikirisha.
Hashil katika kurasa za mwisho wa kitabu kwa masikitiko kasema kuwa mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar si mapinduzi ambayo Umma Party walikuwa wakiyafikiria na walijitayarisha kwa hilo, wala si mapinduzi ambayo Abdallah Kassim Hanga wa ASP alitaka yatokee.
Nahitimisha kwa kusema kuwa hili somo la mapinduzi kama alivyoeleza Hashil Seif bila shaka litawastaajabisha wasomaji na wanafunzi wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwani mapinduzi yalifanyika na ASP wamesema kuwa ni wao ndiyo waliopindua na kuja na kauli mbiu ya, ‘’Mapinduzi Daima.’’
Wengi bila shaka wataguswa na maelezo ya Hashil Seif na vijana wenzake wa Umma Party kwa kazi waliyofanya ya kukamilisha mapinduzi kwa kuzuia umwagaji damu uliokuwa si wa lazima baada ya serikali kuanguka na jinsi walivyorejesha nidhamu kwa wale wanamapinduzi waliokuwa na mapanga mikononi. Wapo wanaoamini kuwa bila ya uongozi wa Umma Party na watu kama Badawi Qulatein na vijana kama Hashil Seif Hashil damu nyingi zaidi ingelimwagika na Mji Mkongwe pengine ungechomwa moto.
Mohamed Said
1 March, 2019.
Baada ya kukiweka kitabu hiki mtandanoni na wasomaji kuwa wengi na mijadala kuzidi kuhusu mapinduzi na kitabu chenyewe Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Institute of Research and Public Policy (ZIRPP) Muhammad Yussuf alinialaka kwenye taasisi yake Zanzibar kukiwasilisha kitabu hiki.
Picha ya kwanza nijaeleza ya pili kushto ni Mkurugenzi Mkuu wa ZIRPP Muhammad Yussuf na ya tatu washiriki katika ukumbi wa ZIRPP mbele kulia ni Dr. Miraji wa SUZA na kushoto ni Othman Miraji aliyekuwa Mtangazaji Sauti ya Ujerumani.

2Francis DM and Samuel Mnkande
2 Comments