Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KITABU KIMESHEHENI
Mtunzi
Mohamedi Bushiri
@Dedesi Baba Wawili
Nimepiga mahesabu,
Kalamu kushikilia.
Niunganishe irabu,
Shairi kujitungia.
Dedesi ni aghalabu,
Maneno anapatia.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Nimekisoma kitabu,
Alichoandika Shekhe.
Kina mengi masaibu,
Si mambo ya starehe.
Tena yale ya aibu,
Sio mambo ya sherehe.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Shekhe mstaharabu,
Upole amejaliwa.
Kaeleza zote tabu,
Shekhe alizofanyiwa.
Kapigwa bila sababu,
Risasi amerushiwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Shekhe si mtu wa gubu,
Fujo anasingiziwa.
Alifanyiwa jaribu,
La kutaka kumuuwa.
Mola ni wake Muhibu,
Begani kajeruhiwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Tununueni kitabu,
Shekhe tupate mjuwa.
Kitabu kakiratibu,
Swafu zimepangiliwa.
Ili tusione tabu,
Kurasa kuzifunguwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Kina nyingi harakati,
Shekhe alizopitia.
Kina pia mikakati,
Ya Shekhe kumvamia.
Mola aliyadhibiti,
Yote walo dhamiria.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Kaditama nimefika,
Ujumbe kuufikisha.
Kitabu kwa uhakika,
Chatufundisha maisha.
Matukio yaso shaka,
Shekhe ameyaonesha.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Mtunzi
Mohamedi Bushiri
@Dedesi Baba Wawili
Nimepiga mahesabu,
Kalamu kushikilia.
Niunganishe irabu,
Shairi kujitungia.
Dedesi ni aghalabu,
Maneno anapatia.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Nimekisoma kitabu,
Alichoandika Shekhe.
Kina mengi masaibu,
Si mambo ya starehe.
Tena yale ya aibu,
Sio mambo ya sherehe.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Shekhe mstaharabu,
Upole amejaliwa.
Kaeleza zote tabu,
Shekhe alizofanyiwa.
Kapigwa bila sababu,
Risasi amerushiwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Shekhe si mtu wa gubu,
Fujo anasingiziwa.
Alifanyiwa jaribu,
La kutaka kumuuwa.
Mola ni wake Muhibu,
Begani kajeruhiwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Tununueni kitabu,
Shekhe tupate mjuwa.
Kitabu kakiratibu,
Swafu zimepangiliwa.
Ili tusione tabu,
Kurasa kuzifunguwa.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Kina nyingi harakati,
Shekhe alizopitia.
Kina pia mikakati,
Ya Shekhe kumvamia.
Mola aliyadhibiti,
Yote walo dhamiria.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.
Kaditama nimefika,
Ujumbe kuufikisha.
Kitabu kwa uhakika,
Chatufundisha maisha.
Matukio yaso shaka,
Shekhe ameyaonesha.
Kitabu kimesheheni,
Matukio ya fedheha.