Kitabu kipya: Jino kwa jino

Kitabu kipya: Jino kwa jino

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3,359
Reaction score
4,528
IMG_20240707_105340_6.jpg


Fikiria wewe ni mfanyabiashara mkubwa sana mjini, unamiliki kampuni iliyopata heshima kubwa. Baba yako ni mkuu wa majeshi mstaafu, kaka yako ni kanali wa jeshi, shemeji yako ni mbunge na mtoto wa Rais wa nchi. Mjini kote wanatambua nguvu kubwa ya ushawishi waliyonayo familia yako.

Unapewa taarifa binti yako kapigwa kibao na mwenzake huko wakiwa ziarani, kisa alijaribu kumuuliza kuhusiana na mahusiano kimapenzi na binamu yake (mjukuu wa Rais wa nchi, ambaye ni mwana wa dada yako). Pia baadaye akaja kupigwa na baba wa binti yeye na binamu, hadi waliumia wakatakiwa kupewa tiba ya haraka.

Hasira inakujaa unaamua kukaa na kaka yako, dada, shemejiyo na mkeo. Mnaamua kusuka mpango huyo binti atekwe na kufanyiwa kitu mbaya, ajua familia zingine si za kuzichezea. Mpango huo mnatimiza vyema, anakuwa kashikiliwa. Ila napo kabla hata siku haijaisha yule baba wa binti anavamia nyumbani kwako, anapiga walinzi wote na wengine wote sambamba na kukuvunja goti. Anaulizia alipo binti yake,, ila unaonesha hujui.

Unapewa matibabu ila unapokuja kuruhusiwa baba yako anakuuliza kama kweli umehusika na kumteka binti yake. Unakana waziwazi ila ukweli unaujua mwenyewe, unaamua kuficha ukiwa humwoni kama anaweza kuwa tishio kwako. Anakuusia umweleze ukweli, ila napo kwakuwa una nguvu ya ndugu zako wala huoni kama ana hatari namna hiyo.

Haya ni mambo yaliyomkuta Hamdani Singano, kwa kumwendekeza binti yake mwenye tabia zisizo nzuri, hadi kumsikiliza kila alipoelezwa pasipo kuchunguza. Mambo anakuja kujua si mambo, ule uwezo wa familia na ushawishi mkubwa wa shemejiye, hauwezi kufua dafu dhidi ya balaa walilolitibia.

Kumbe walimgusa mtu wa kikosi wa maalum cha siri sana, ambayo kiliundwa kuisaidia iwapo nchi ipo mashakani. Kutokana na usiri wake ilielezwa kundi lile hakuna sheria ya kuwadhibiti wala kiongozi mwenye mamlaka ya kuwaongoza. Hata ikitokea dharura kitu ambacho kitawafanya wachukue hatua ni hati yenye saini tatu. Hizo nazo ni ya Rais, Mkuu wa majeshi na Kiongozi wao mkuu.

Matokeo ni umwagaji damu unafuatia, si Rais wala Mkuu wa majeshi aliyeruhusu uchunguzi ufanyike kwa watu. Jalada lilipofunguliwa tu na polisi, amri ilifikishwa kwa JGP lifungwe mara moja

Habari yao anaelezwa Rais akishakula kiapo tu, na Mkuu wa majeshi akiteuliwa, zaidi ya hapo hakuna mwingine anayewajua. Watu hao ambao ni hatari na hawana suluhu nyingine ya kutatua jambo, isipokuwa kumwaga damu. Hao waliundwa kwa ajili ya operesheni ya kuzuia makaburu wa kusini mwa Afrika, waliyotaka kuchukua hatua dhidi ya Tanzania. Na walibakishwa kwa ajili ya kuilinda nchi pekee.

____________________
Naam hii riwaya inayoitwa JINO KWA JINO- Mlie kama nilivyolia, riwaya hii ipo kwenye mfumo wa nakala ngumu (hard copy) na inapatikana kwa shilingi 13000 kwa nakala ya kurasa za rangi maalum kwa wenye matatizo ya macho, na sh 10000 kwa kurasa nyeupe (hizi kwa sasa zimeniishia). Ndani ya Dar es salaam ninakufanyia delivery kwa shilingi 2000, mkoani napo unatumiwa kwa gharama yako ya usafiri.
Kusafirisha mikoani ipo kama ifuatavyo;
Mikoa ya kanda ya kaskazini, Tanga, Kilimanjaro na Arusha gharama inakuwa ni shilingi 5000 jumlisha na pesa ya kitabu husika.

Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songea ni shilingi 6000

Kanda ya ziwa, Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Singida ni shilingi 10000 au chini ya hapo kutokana na mkoa husika.

Mikoa ya kusini ni shilingi 6000 kulingana na eneo unaloenda.

UTUMAJI NI WA UHAKIKA KWA UAMINIFU MKUBWA SANA, UTAKIPATA KITABU CHAKO KWA NJIA YA BASI ULIPO SAMBAMBA NA VIELELEZO VYA MZIGO HUSIKA. KWA MAELEZO ZAIDI FIKA DM AU WHATSAPP NAMBA 0762219759.

KWA WENYE KULIPA BILA MLOLONGO WA MAELEZO YA ZIADA BASI NAMBA YA MALIPO NI MPESA 0762219759 JINA NI HASSANI OMAR MAMBOSASA.. UKILIPA TOA TAARIFA UKITAJA JINA LAKO NA ENEO AMBALO UNATAKIWA KUFIKISHIWA KITABU CHAKO
 

Attachments

  • IMG_20240707_105355_6.jpg
    IMG_20240707_105355_6.jpg
    4.7 MB · Views: 9
  • IMG_20240707_105413_5.jpg
    IMG_20240707_105413_5.jpg
    4.6 MB · Views: 11
Back
Top Bottom