Kitabu kipya: Watu mashuhuri katika uhuru wa Tanganyika - Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Peter Mhando kitabu cha pili

Kitabu kipya: Watu mashuhuri katika uhuru wa Tanganyika - Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Peter Mhando kitabu cha pili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITABU KIPYA: WATU MASHUHURI KATIKA UHURU WA TANGANYIKA - SALUM MPUNGA, YUSUF CHEMBERA NA PETER MHANDO
KITABU CHA PILI


1574355063508.png


1574276661593.png

1574276704247.png

Kitabu kipya kufuatilia cha kwanza kilichoeleza mchango wa Sheikh Rashid Sembe, Tewa Said Tewa na Zuberi Mtemvu kitakuwa Ibn Hazm Media Centre, Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 22 November 2019.

Kitabu hiki kinaeleza maisha ya marafiki wawili kutoka Lindi Salum Mpunga na Yusuf Chembera wote wanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi jinsi walivyoweza katika hali ngumu ya ukoloni uliokuwa Southern Province (Mkoa wa Kusini) ambako serikali ya kikoloni na mshirika wake mkuu walikuwa wanawatisha wananchi wasijiunge na TANU lakini juu ya vitisho hivi wazalendo hawa kutoka tabaka la chini kabisa waliweza kuwahamasisha wananchi wa mikoa ya kusini kujiunga na TANU.

Wakaweza pia kumuingiza na mwalimu wao Sheikh Yusuf Badi kujiunga na TANU na kujiunga na TANU kwa Sheikh Yusuf Badi kukaipa TANU nguvu kubwa ya kuweza kukieneza chama kote hadi Peramiho, Masasi na kusini yote.

Safari ya kwanza ya mafanikio aliyofanya Mwalimu Nyerere ilikuwa Lindi kwa kuitika mwaliko uliotoka kwa wanachama wa TANU, mwaliko ambao ulifikishwa Ofisi ya TANU wakati wa mkutano wa mwaka wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955, na wajumbe kutoka Lindi Salum Mpunga na Ali Mnjale.


Jina la Peter Mhando halijasikika katika historia ya TANU.

Peter ni mdogo wake Steven Mhando ambae na yeye kama kaka yake jina lake halipo katika historia ya TANU ingawa mchango wake ni mkubwa kiasi wakoloni wakamuitikadi kuwa ni Mkomunisti.

Peter Mhando ndiye aliyepelekwa Makao Makuu ya TANU, New Street kutoka Tanga kuja kuongeza nguvu katika uongozi wa TANU uliokuwa Makao Makuu.

Peter Mhando sasa kutoka Dar es Salaam akatumwa Tabora akamalize mgogoro wa TANU uliokuwa unafanya chama kisipige hatua kusonga mbele.

Peter Mhando katika taarifa yake kwa Rais wa TANU Mwalimu Julius Nyerere, alipendekeza Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka wa 1958 ufanyike Tabora na ikasadifu kuwa ndiyo ukawa Mkutano wa Kura Tatu.

Peter Mhando hakuwa na maisha baada ya kukamilisha kazi hii aliyotumwa na Mwalimu Nyerere.

Peter Mhando alikufa kijana sana na hakushuhudia Mkutano wa Kura Tatu.

Hawa ndiyo mashujaa wa TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika ambao historia imewasahau.

Kitabu hiki cha pili ni muendelezo wa vitabu vidogo vya kuwakumbuka mashujaa hawa.
 

Attachments

Nashukuru kwa habari hii njema kwetu sisi tunaopenda kujifunza hasa kupitia maandiko yako
 
Back
Top Bottom