Kitabu: Maisha ya Malcom X

sura ya 13. Imam Malcom X

Niliacha kazi kwenye kampuni ya Ford. Ilikuwa wazi kwangu kuwa Bwana Muhammad anahitaji wahubiri wa kutangaza mafundisho yake na kuanzisha Mahekalu mengine kwa watu weusi milioni ishirini na mbili waliokuwa wameshikwa akili na “kulala” kwenye majiji ya Marekani.
Uamuzi wangu ulikuja mara moja bila kusita. Mara zote nimekuwa ni mwanaharakati, na pengine hilo ndilo lililonifanya nichukue hatua haraka kuliko Maimam wengine. Lakini kila Imam, kwa muda wake na kwa nafasi yake alifikia hitimisho kuwa ilikuwa imeandikwa awe mwanafunzi wa bwana Muhammad, na maisha yake yote yalikuwa ni maandalizi kwa ajili ya suala hilo.
Uislamu unafundisha kuwa kila kinachotokea kimeandikwa.
Kwa miezi kadhaa aliyokuwa akinifundisha, Bwana Muhammad alinikaribisha kumtembelea nyumbani kwake Chicago mara nyingi niwezavyo.
Hata gerezani sikuwahi kusoma na kujifunza kwa makini kama nilivyojifunza chini ya bwana Muhammad. Nilizama kujifunza taratibu za ibada; mafundisho yake juu ya wanawake na wanaume; taratibu za kiuongozi; maana halisi na maana zingine, na matumizi ya Biblia na Quran.
Kila usiku nilienda kulala nikiwa nimeshangazwa zaidi. Kama si Allah basi ni nani mwingine angeweza kuweka hekima ile ndani ya mwanakondoo mnyenyekevu yule kutoka Georgia aliyeishia darasa la nne. Neno “mwanakondoo” nililitoa kwenye unabii unaopatikana kwenye kitabu cha Ufunuo ambako kuna kondoo wa mfano aliyekuwa na upanga wenye makali kuwili mdomoni mwake. Upanga wenye makali kuwili wa bwana Muhammad ulikuwa ni mafundisho yake, ulikata mbele na nyima ili kuiweka huru akili ya mtu mweusi kutoka kushikwa na mzungu.
Nilimhusudu bwana Muhammad kwa maana halisi ya neno la Kilatin nilalomanisha kuhusudu—yaani “Adorare.” Linamaanisha zaidi ya kuhusudu. Linamaanisha kumsujudu kwangu kulikuwa kukuu sana kiasi kwamba ndiye alikuwa mtu pekee niliyewahi kumuogopa—si kuogopa kama kule kumuogopa mtu mwenye bunduki, bali kuogopa kama vile kumuogopa mtu mwenye nguvu za jua.
Baada ya bwana Muhammad kuona kuwa nimeiva alinituma Boston. Ndugu Lloyd X aliishi huko. Aliwakaribisha watu waliopendezwa na mafundisho yake ya Kiislamu kuja kunisikiliza sebuleni kwake.
Nitanukuu niliyosema pale na sehemu nyingine nilizoenda kuhubiri. Maana nakumbuka mambo niliyohubiri mara kwa mara. Nakumbuka siku zile nilipenda sana kuanza na mfano juu ya bwana Muhammad.
“Mungu amempa bwana Muhammad ukweli mkali,” niliwaambia. “Ni kama upanga wenye makali kuwili. Unakukata na kukusababishia maumivu makali, lakini kama unaweza kuukubali ukweli, utakuponya na kukuokoa kutoka katika kifo.”
Baada ya utangulizi huo sikupoteza muda, mara moja nilianza kuwafungua macho juu ya shetani mweupe. ‘Najua hamtambui ukubwa wa madhira ya uhalifu wa mzungu mkristo . . .
‘Hata katika Biblia hakuna uhalifu kama huo! Mungu kwa hasira aliwaua kwa moto waliofanya uhalifu mdogo kuliko huu. Watu weusi milioni mia moja! Mababu wako na wangu! Waliuawa na mzungu huyu ili tu kutufikisha hapa watu milioni kumi na tano na kutufanya watumwa. Njiani aliua watu milioni mia moja. Natamani ningeweza kuwaonyesha sakafu ya bahari ilivyokuwa wakati huo. Miili ya watu weusi, damu, na mifupa iliyovunjwa kwa mateke na marungu. Miili ya wanawake wajawazito waliotupwa baharini baada ya kuwa wagonjwa sana. Wakitupwa baharini kwenye papa, papa waliojifunza kuwa kufuata meli za watumwa ni njia rahisi ya kujipatia chakula.
“Kitendo cha wazungu kubaka wanawake weusi kilianza mle mle melini! Shetani mwenye macho ya bluu hakusubiri awafikishe kwanza! Binadamu aliyestaarabika hajawahi kushuhudia uchafu na mauaji na namna ile ”
Kuzungumzia ubaya wa utumwa hakujawahi shindwa kuwagusa watu weusi. Inashangaza sana kuona watu wengi
weusi wamekubali mzungu awapotoshe kiasi cha wengine kudhani kuwa enzi za utumwa zilikuwa enzi za starehe! Mara baada ya kuwachochea kwa habari za utumwa nilianza kuwazungumzia wao wenyewe.
‘Nataka mtakapo chumbani hapa muone hili kila mnapoonana na shetani wa kizungu. Ndiyo, ni shetani. Nataka muanze kumchunguza kwenye maeneo yake ambayo hataki nyinyi muwepo. Mchunguzeni anapokuwa anajifunua waziwazi.
“Kila mara unapomuona mzungu, fikiria kuhusu shetani unayemuona! Fikiria kuwa ni kupitia damu na jasho la babu zako watumwa ndiyo alijenga Milki hii ambayo leo hii ndiyo nchi tajiri kuliko zote duniani-dunia inayomchukia kutokana na uovu na tama yake.
Kila mkutano, wale waliofika mkutano uliopita walirudi wakiwa na rafiki zao. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kushuhudia mzungu akivuliwa kinyago alichojivika. Kila baada ya mkutano niliuliza, “kila anayeamini aliyosikia asimame.” Sikumbuki kuona mtu ambaye hakusimama. Na hata siku za Jumapili usiku niliposema, “Nani anataka kuwamfuasi wa Mtukufu Elijah Muhammad?” walisimama hata wale ambao niliona wazi hawako tayari.
Baada ya kama miezi mitatu tulikuwa na watu wa kutosha kuweza kufungua Hekalu dogo. Nakumbuka furaha tuliyokuwa nayo tulipokodi viti vya kukunjwa kwa ajili ya Hekalu letu. Nilijawa na furaha sana siku niliyomjulisha bwana Muhammad anuani ya Hekalu letu.

Ni wakati tulipopata Msikiti huu mdogo ndipo dada yangu Ella alianza kuja kunisikiliza. Alikaa na kustaajabu kama vile haamini nilikuwa ni mimi kweli. Ella hakuwahi kuinuka hata pale niliposema wale wanaoamini waliyosikia wasimame. Lakini alichangia tulipopitisha mchango wa sadaka. Lakini suala la Ella halikunihangaisha, wala sikuwahi kufikiria kumsilimisha, nilimfahamu ni kichwa ngumu na anayechukua tahadhari sana kabla ya kujiunga na chochote. Sikutegemea mtu yeyote amsilimishe Ella zaidi ya Allah mwenyewe.
Nilifunga mikutano kama nilivyofundishwa na bwana Muhammad: “Kwa jina la Allah, mlezi na mwenye rehema. Sifa zote zimuendee Allah, Bwana wa ulimwengu mzima. Bwana mwenye rehema wa siku za hukumu ambazo tunaishi. Ni wewe pekee tunayekutumikia. Hakuna Mungu ila wewe, na Mtukufu Elijah Muhammad ni mtumishi na mtume wako.” Niliamini kuwa Elijah Muhammad alitumwa kwetu na Allah mwenyewe.
Niliinua mkono kuwaashiria kuwa wanaweza kwenda: “Usimfanyie mtu yeyote vile usivyopenda wewe wenyewe kutendewa. Tafuta amani na kamwe usiwe mwenye kuonea— lakini kama mtu akikushambulia, hatufundishi umgeuzie shavu jingine. Allah awabariki mfanikiwe katika yote mfanyayo.”
Ukiacha siku ile niliyolala kwa Ella nilipokuwa naenda Detroit, nilikuwa sijatembelea mitaa ya Roxbury kwa miaka saba. Basi nikaenda kuonana tena na Shorty.

Nilipoonana na Shorty hakuwa kawaida. Habari zilikuwa zimemfikia kuwa nipo mjini na nimezama kwenye mambo fulani ya kidini. Hakuwa na hakika kama nimezama kweli au nilikuwa tu mhubiri –kuwadi mwingine kama wale wanaopatikana kwenye maeneo ya maghetto ya watu weusi. Wale wenye makanisa madogo kwenye fremu za maduka, makanisa ambayo waumini wake wakubwa ni wanawake wazee ambao hufanya kazi kwa bidii kuwafanya wachungaji wao vijana kuvaa kitanashati na kuendesha magari ya gharama. Mara moja nilimfanya Shorty aamini kuwa sikuwa na utani na Uislamu, lakini tuliongea maongezi ya mtaani na tukawa na wakati mzuri. Tulicheka hadi kutokwa na machozi tulipokumbuka jinsi Shorty alivyokuwa Jaji alipoendelea kuhesabu “Kosa la kwanza, miaka kumi. . . kosa la pili, miaka kumi. . . “ tuliongea jinsi ambavyo kuwa na wasichana wale wa kizungu kulitupatia miaka kumi wakati gerezani tumekutana na wafungwa wenye makosa mazito zaidi yetu lakini wakiwa na miaka michache zaidi yetu.
Shorty bado alikuwa na bendi yake ndogo na alikuwa anaendelea vizuri. Alikuwa anajivuna sana kwamba aliweza kusoma muziki akiwa gerezani. Nilimueleza kiasi kuhusu Uislamu na niliona kuwa hakuwa tayari kusikia habari zake. Akiwa gerezani alikuwa amesikia habari mbaya kuhusu dini yetu. Alinikatiza kwa kuingiza masihara kwenye mazungumzo. Alisema kuwa bado hajala nyama ya nguruwe wala kupata wanawake wa kizungu wa kutosha kuridhisha nafsi yake. Sifahamu kama sasa ameridhika, ninachojua ni kuwa sasa ameoa mwanamke wa kizungu. . . na amekuwa mnene kama nguruwe kwa sababu ya kula nguruwe.
Nilionana na John Hughes, mmiliki wa nyumba ya kamari na wengine niliowafahamu ambao bado waliishi Roxbury. Habari juu yangu ziliwafanya wote wasinichangamkie kama kawaida, lakini maneno yangu ya mtaani yalisaidia walau tukawa na maongezi. Wengi wao sikuwaeleza kuhusu Uislamu. Kwa jinsi nilivyoishi nao hapo zamani nilifahamu jinsi walivyochotwa akili.
Nilitumikia kwa muda mfupi sana kama Imam wa Hekalu Namba Kumi na Moja. Mara tu nilipoliweka sawa nikaliacha chini ya Imam Ulysses X, hiyo ilikuwa mwezi wa tatu mwaka 1954. Mtume alinihamishia huko Phildelphia.
Watu weusi wa Philadelphia waliikubali kweli kuhusu mzungu haraka kuliko wale wa Boston. Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huo Hekalu Namba Kumi na Mbili la Philaelphia likawa limeanzishwa. Ilichukua chini ya miezi mitatu kulianzisha.

Mwezi uliofuata, kutokana na mafanikio yangu ya Boston na Philadelphia, bwana Muhammad aliniteua kuwa Imam wa Hekalu Namba Saba huko jijini New York.

Siwezi kuelezea hisia zangu zilivyokuwa. Maana ili mafundisho ya bwana Muhammad yamuamshe mtu mweusi wa Marekani, ilihitajika Uislamu ukue, ukue sana. Na hakuna sehemu nyingine ndani ya Marekani ambayo hilo liliwezekana zaidi ya wilaya tano za jiji la New York. Huko walikaa watu weusi zaidi ya milioni moja.

LUKAMA Siogye
 
pamoja sana mkuu
 
Sura ya 13 inaendelea

Ilikuwa imepita miaka tisa tokea tuviziane mitaani na West Indian Archie. Tukijaribu kuuana kama mbwa.
“Red!”. . . “Red mtu wangu!”. . . Siamini ni wewe.sasa nywele zangu nyekundu zikiwa zimekatwa na kuwa fupi badala ya zile ndefu zilizotiwa dawa walizozoea kuniona nazo, mimi mwenyewe nilifahamu kuwa nilionekana tofauti sana. “Mhudumu mpatie kinywaji. Nini? Umeacha! Acha hizo mtu wangu!”
Ilikuwa furaha sana kukutana na wengi niliowafahamu vyema wakiendelea vyema. Lakini Sammy the Pimp na West Indian Archie ndiyo hasa niliowatafuta. Mshtuko wa kwanza ulikuwa kuhusu Sammy. Alikuwa ameacha ukuwadi na alikuwa amekuwa mtu mkubwa kwenye biashara ya kamari. Kisha akaoa msichana fulani mdogo mapepe. Lakini muda mfupi baada ya kuoa alikutwa kitandani kwake amekufa— wanasema alikutwa na dola elfu ishirini na tano mfukoni mwake. (Watu huwa hawataki kuamini kiasi cha pesa ambazo hata mabosi wadogo wa kwenye biashara haramu hushika. Kwa mfano: mwezi wa tatu mwaka 1964, mchezesha kamari kwa kutumia gurudumu la bahati huko Chicago, Lawrence Wakefield alifariki na nyumbani kwake zaidi ya dola 760,000 zilikutwa kwenye mabegi na vifurushi. . . zote kutoka kwa watu weusi masikini. . . na bado tunashangaa kwa nini tunaendelea kuwa masikini)

Nikiwa nimesikitishwa na habari kuhusu Sammy, nilitembea baa moja hadi nyingine nikiwauliza wakongwe kuhusu West Indian Archie. Hakukuwa na habari za kifo chake au kuishi sehemu fulani. Lakini hakuna aliyefahamu alikokuwa. Nilisikia mambo yaliyowapata wengine wengi, mambo ambayo huwapata wapambanaji kwa kawaida. Kupigwa risasi, kuchomwa visu, gerezani, madawa ya kulevya, magonjwa, kurukwa na akili na ulevi wa pombe na mabo kama hayo. Wengi waliokuwepo, watu ambao niliwafahamu kama fisi na mbwa mwitu wenye nguvu wa nyakati zile walikuwa kwenye hali ya kusikitisha sana. Walijua michakato mingi lakini ndani yao walikuwa watu weusi masikini, wajinga na wasio na ujuzi wowote; maisha ni kama yalikuwa yamewachezea mchezo. Nilikutana na wakongwe hawa niliowafahamu vyema karibu ishirini na tano, ndani ya miaka tisa walikuwa wamefanywa kuwa machokoraa wa maghettoni, watu wanaotafuta tu pesa ya kula na kodi. Wengine walikuwa wakifanya kazi mjini kama watumishi, wafanya usafi na kazi kama hizo. Nilimshukuru Allah kuwa nilikuwa Muislamu na kuepuka mwisho kama wao.
Kulikuwa na Cadillac Drake, alikuwa ni kuwadi mmoja mnene, mweusi tin a aliyependelea kuvuta cigar. Alikuwa ni mteja wa kawaida wa mchana wakati nilipokuwa mhudumu wa Small’s Paradise. Nilimtambua alipokuwa akielekea upande wangu mtaani. Niliambiwa kuwa alikuwa amekuwa teja wa heroin. Alikuwa ni mtu mchafu na wa hovyo kuliko yoyote uliyewahi kumuona. Nilimkimbia haraka maana sote tungeaibika iwapo angenitambua, mtoto aliyezoea kunirushia dola kama bakshishi.

Habari za aliko West Indian Archie zikaibuka. Watu wa mtaani wakidhamiria kupata habari huwa kama Western Union iliyo na F.B.I kama mpeleka taarifa. Kwenye huduma zangu za mwanzo katika Hekalu Namba Saba, mpambanaji mmoja mzee aliyechoka, ambaye nilikuwa nimempa dola kadhaa kumsaidia, alinifuata baada ya kufunga ibada. Aliniambia kuwa West Indian Archie alikuwa anaumwa na alikuwa anaishi kwenye chumba alichopanga huko Bronx.
Nilichukua taxi mpaka kwenye makazi yake. West Indian Archie alifungua mlango. Alisimama pale akiwa peku na nguo za kulalia.

Umewahi kuona mtu anayeonekana kama mzimu wa mtu unayemfahamu? Ilimchukua sekunde kadhaa kunikumbuka. Alisema kwa sauti ya kukwaruza, “Red! Nimefurahi kukuona!”

Nilimsaidia kurudi ndani. Alikaa kitandani nami nilikaa kwenye kiti chake kimoja na kumwambia jinsi kunikimbiza kwake Harlem kulivyookoa maisha yangu kwa kuniongoza kwenye Uislamu.
Alisema, “Siku zote nilikupenda Red,” akasema pia kuwa hakuwa na dhamira hasa ya kuniua. Nilimwambia jinsi ambavyo nimetetemeka mara nyingi ninapokuwa nafikiria jinsi tulivyokuwa karibu kuuana. Nilimwambia kuwa niliamini kabisa kuwa nilishinda zile dola mia tatu alizonipa. Archie aliniambia kuwa baadaye alitafakari iwapo labda
alikuwa amekosea maana nilikuwa tayari kufa kwa sababu ya jambo lile. Mwishowe tulikubaliana hakuna haja ya kuliongelea, halina maana tena. Katika maongezi yetu alirudia tena na tena kusema kuwa amefurahi sana kuniona.
Nilimueleza kidogo Archie juu ya mafundisho ya bwana Muhammad. Nilimueleza jinsi ambavyo sote tuliokuwa mtaani tulikuwa ni wahanga wa jamii iliyotengenezwa na mzungu, nilimueleza jinsi nilivyomfikiria nilipokuwa gerezani; kwamba akili yake iliyoweza kutunza kutunza mamia ya namba kwa siku, ilitakiwa kutumika kwenye hesabu au sayansi. Nakumbuka alisema, “Hilo linafikirisha sana Red.”

Lakini hakuna kati yetu aliyesema kuwa bado hajachelewa. Nafikiri alifahamu kama nilivyofahamu kuwa mwisho wa Archie umekaribia. Sikuweza kukaa sana sababu nilisikitishwa sana na hali aliyokuwa nayo ukilinganisha na jinsi alivyokuwa huko nyuma. Sikuwa na pesa nyingi naye hakutaka kupokea kidogo nilichompatia. Lakini nilimsisitiza apokee.

***

Kila mara inabidi nijikumbushe kuwa bado kuwa wakati ule, mwezi wa sita wa mwaka 1954, Hekalu Namba Saba jijini New York lilikuwa ni chumba cha duka tu. Haukuwezekana kujaza basi moja kwa Waislamu waliokuwako jijini New York. Hata kati ya watu weusi walioishi Harlem hakukuwa na Waislamu, ungeweza sema “Muislamu” kati ya watu elfu moja na labda ni mmoja tu ambaye hangekuuliza, “Ni kitu gani hicho?” na kati ya wazungu, ukitoa wale walioweza kupitia majalada ya polisi au ya gerezani—waliofahamu uwepo wetu hawakuzidi mia tano.
Nilianz kutema mafundisho ya bwana Muhammad kwa kwa washiriki wa New York na rafiki zao waliowaleta. Na kila mkutano kuhangaika kwangu moyoni kulizidi kukua, kwamba Harlem iliyojaa masikini na watu weusi wasio na elimu, wakitaabika kwa madhira yote yanayoweza kutibiwa na Uislamu lakini kila nilipohubiri na kuuliza wale wanaotaka kuwa wafuasi wa bwana Muhammad wasimame, walisimama wawili au watatu tu. Na nikiri kuwa wakati mwingine hata idadi hiyo haikufika.

Nafikiri nilikasirikia zaidi kutokana na kutofanikiwa kwangu kwa sababu niliijua mitaa yote. Ilinibidi kukaa na kutafakari tatizo ni nini. Tatizo kubwa lilikuwa ni tulikuwa moja tu kati ya vikundi vingi vya watu waliohubiri manung’uniko ya mtu mweusi kwenye kila kona ya Harlem. Makundi mbalimbali yaliyohubiri Utaifa wa mtu mweusi, waliohimiza kununua kwa weusi wenzao tu na wengine kama hao. Makumi ya wasemaji wao walihubiri kwenye ngazi za Harlem ili kujiongezea wafuasi. Sikuwa na tatizo lolote na mtu yeyote aliyekuwa akihimiza watu weusi kujitegemea na kuungana lakini walifanya iwe vigumu sana kwa sauti ya bwana Muhammad kusikika.

Hatua ya kwanza niliyochukua kukabiliana na hili ilikuwa kuchapisha vipeperushi. Hakuna kona ya Harlem yenye pilika nyingi ambayo hatukuitembelea nikiwa na ndugu zangu wengine wa Wakiislamu kama watano au sita hivi. tuliwakaribia watu waliokuwa wanatembea mtaani kiasi kwamba hawakuwa na jinsi zaidi ya kupokea vipeperushi vyetu, na kama walisita hata kwa sekunde moja walitusikia tukisema, “Sikia jinsi ambavyo mzungu ameteka, amepora na kuharibu jamii yetu ya watu weusi-”

Baada ya hapo tukaenda kufanya uvuvi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Harlem-mbali na wahubiri wengine. Siku hizi mbinu zimebadilika, lakini wakati ule ilitakiwa kuendana na muelekeo wa umati ambao ulibadilika kila leo. Kwenye mikotano ya waliohubiri utaifa, kila aliyehudhuria kusikiliza alitaka kusikia habari za mapinduzi ya jamii ya watu weusi. Tulianza kuona matokeo mara moja baada ya kuanza kuwapatia watu vipeperushi kwenye mikutano hiyo, ‘Karibu ndugu utusikilize na sisi. Mtukufu Elijah Muhammad anatufundisha jinsi ya kutibu magonjwa ya kiroho, kiakili, ya kimaadili, kiuchumi na kisiasa yanayomkabili mtu mweusi. Nikaanza kuona sura mpya Hekaluni. Kisha tukagundua watu rahisi kabisa wa kuwafanyi uvuvi. Watu waliokuwa tayari zaidi kusikiliza mafundisho ya bwana Muhammad walikuwa ni waenda makanisani. Tulifanya mikutano yetu ya jumapili saa nane mchana. Kama saa moja kabla ya hapo ibada ilikuwa inaisha kwenye makanisa kotekote katika Harlem. Hatukwenda kwenye makanisa makubwa ambayo waumini wake wengi walikuwa ni watu weusi wa “Daraja la kati” watu waliojivuna na kujidai kiasi kwamba wasingeweza hudhuria kwenye Hekalu letu dogo kwenye chumba cha duka.

Mara tu makanisa yale madogo yalipoachia waumini wake thelathini hadi hamsini, tuliingia barabarani mara moja kufanya uvuvi. “karibu utusikilize dada—ndugu-” “Hujasikia kitu kama bado hujasikia mafundisho ya Mtukufu Elijah Muhammad.” Wengi wa waumini wa makanisa haya walikuwa ni wahamiaji kutoka kusini, hasa wazee ambao walienda sehemu yoyote kusikia walichoita, “Mahubiri mazuri.” Haya ndiyo yale makanisa ambayo nje yalikuwa na matangazo kuwa ndani wanauza kuku wa kukaanga na utumbo ili kuongeza kipato. Na siku tatu au nne kwa juma walifika kanisani kwao usiku wakifanya mazoezi kwa ajili Jumapili, nadhani mazoezi ya kucheza na kuimba injili kwa magitaa na tari.
Sijui kama unafahamu, lakini kuna wasanii wengi wa nyimbo za injili ambao wametokea kwenye makanisa haya madogo ya maeneo ya maghetto au huko kusini. Watu kama dada Rosetta Tharpe na The Clara Ward Singers ni mifano michache lakini kuna walau wasanii wengine wadogowadogo mia tano wa aina hiyo. Mahalia Jackson, msanii mkubwa kuliko wengine wote ni mtoto wa mchungaji huko Lousiana. Alienda Chicago na kufanya kazi za usafi na upishi kwa wazungu na baadaye kiwandani huku akiimba kwenye makanisa ya watu weusi, nyimbo zake zilimfanya kuwa mtu mweusi wa kwanza kufanywa maarufu na watu weusi wenyewe. Alikuwa anauza mamia elfu ya albamu zake kwa watu weusi kabla hata wazungu hawajamjua Mahalia Jackson ni nani. Kuna mahali nilisoma Mahalia mwenyewe akisema kuwa kila alipopata nafasi alikuwa akienda kwa kushtukiza kwenye makanisa haya madogo ya watu weusi na kuimba na watu wake, anaita makanisa hayo “kituo changu cha kunijaza nguvu”
Wakristo weusi “tuliowavua” walishtushwa sana baada ya kuwaambia yaliyokuwa yanawatokea wakati wakiabudu Mungu mwenye nywele za rangi ya dhahabu na macho ya bluu. Nilijua Hekalu nitakalojenga litakavyokuwa iwapo nitaweza kuwafikia wakristo wale. Niliyaweka mafundisho kwa namna ya kuwafaa wao zaidi. Wakati mwingine niliongea kwa mzuka hadi ikanibidi kujieleza, “Mnaona machozi yangu ndugu na dada zangu . . . Sijawahi toa machozi tokea nilipokuwa mvulana mdogo. Lakini siwezi kujizuia pale ninapoguswa na jukumu nililonalo la kuwasaidia kuelewa jinsi dini ya mzungu tunayoiita Ukristo ilivyotutendea. . . .

‘Ndugu na dada naomba msishtuke. Nafahamu kuwa hamkutarajia hili. Sababu karibu watu weusi wote hakuna aliyefikiria kuwa pengine tulikuwa tunakosea kwa kutotafakari kuwa kuna dini yetu mahali fulani-dini maalumu kwa ajili ya mtu mweusi. ‘Basi dini hiyo ipo. Inaitwa Uislamu. Acha niwatajie herufi zake, u-i-s-l-a-m-u! Uislamu! Lakini nitawaeleza kuhusu Uislamu hapo baadaye kidogo. Kwanza tunatakiwa kuuelewa huu Ukristo kabla ya kuelewa kwa nini Uislamu ndiyo unaotufaa.
‘Ndugu na dada zangu, mzungu ametuchota akili watu weusi ili tumkodolee macho Yesu mwenye macho ya bluu na
nywele za rangi ya dhahabu. Tunamuabudu Yesu ambaye hata hafanani na sisi. Ndivyo ilivyo, sasa nisikilizeni kwa makini, sikilizeni mafundisho ya Mtume wa Allah, Mtukufu Elijah Muhammad. Tafakari hili. Mzungu mwenye macho ya bluu na nywele za rangi ya dhahabu katufundisha mimi na wewe kumuabudu Yesu ambaye ni mzungu. Kuimba na kupiga kelele kwa Mungu huyu, Mungu wake, yaani Mungu wa Mzungu. Mzungu katufundisha kupiga kelele na kuimba hadi tutakapokufa—kusubiri mpaka tutakapokufa ili kuingia mbinguni wakati yeye mzungu akipata asali na maziwa yake kwenye mitaa iliyosakafiwa kwa dola za dhahabu hapa hapa duniani.
“Hamtaki kuamini ninachowaambieni? Basi nitawaambieni cha kufanya. Nendeni na chunguzeni vizuri mahali mnapoishi. Usiangalie tu unavyoishi, bali pia angalia kila unayemfahamu anavyoishi—kwa namna hiyo utatambua kuwa jinsi unavyoishi si bahati mbaya. Ukishaangalia unapoishi nenda ufanye matembezi meneo ya chini ya Central Park na ujionee jinsi ambavyo Mungu mweupe amemtendea mtu mweupe. Namaanisha nenda kaangalie mzungu anavyoishi.
“Na usiishie hapo. Hata hivyo huwezi kukaa sana kabla walinzi wa mlangoni kwake hawajakwambia ‘Ondoka!’ Panda treni na tembelea maeneo mengine ya mjini-kati. Angalia makazi na biashara za mzungu. Nenda mpaka mwisho wa kisiwa cha Manhattan, kisiwa ambacho shetani huyu wa kizungu aliwaibia Wahindi waliomuamini kwa kuwalipa dola
ishirini na nne. Angalia makao yake makuu ya jiji; angalia sehemu yake ya biashara ya Wall Street! Jiangalie mwenyewe! Muangalie Mungu wake!”

Kuna jambo moja muhimu sana nililojifunza mapema, kwamba siku zote ninatakiwa nifundishe kwa namna ambayo watu wataelewa. Wengi tuliowavua kwenye mikutano ya Wataifa walikua ni wanaume, na wale tuliowapata kwenye makanisa madogomadogo wengi wao walikuwa wanawake. Nilikuwa na kitu kwa ajili ya wanawake hao, mwanamke mweusi mzuri! Mtukufu Elijah Muhammad anatufundisha kuwa mwanaume mweusi anaenda huku na kule akipiga kelele kuwa anataka heshima yake; ukweli ni kuwa mwanaume mweusi hatapata heshima kutoka kwa yeyote mpaka pale atakapoanza kumheshimu mwanamke wake! Mwanaume mweusi anatakiwa kusimama leo na kutupilia mbali udhaifu aliowekewa na bwana-watumwa wake wa kizungu. Mwanaume mweusi anatakiwa kuanza leo kumtunza, kumlinda na kumheshimu mwanamke wake mweusi.”

Wote walisimama bila kusita niliposema, “Wangapi wanaamini waliyosikia?” lakini kwa mara nyingine ni wachache sana waliosimama niliposema, “Wasimame wale wanaotaka kumfuata mtukufu Elijah Muhammad.”
Nilifahamu kuwa sheria zetu kali za maadili na nidhamu ya hali ya juu ndivyo vilivyowazuia wengi kujiunga. Nikalazimika kuongelea sababu ya sheria zetu za maadili. “Mzungu anataka mtu mweusi aendelee kuwa asiye na
maadili, mchafu na mjinga. Kadri tutakavyoendelea kuwa katika hali hizo, tutaendelea kuwa ombaomba kwake naye atatutawala. Hatutaweza kupata haki na uhuru mpaka pale tutakapokuwa tunajifanyia mambo yetu wenyewe.”

Sheria na taratibu zilifafanuliwa kwa wale waliopendezwa na kujiunga na Uislamu. Maneno yangu yalifika kwenye makanisa yao madogo, ndiyo sababu walikuja kunisikiliza, lakini bado hawakutaka kuwa wafuasi wa bwana Muhammad. Uasherati wa aina yeyote ulikuwa ni mwiko katika Taifa la Kiislamu. Ulaji wowote wa nyama chafu ya nguruwe na vitu vingine vyenye kudhuru au visivyofaa kwa afya; matumizi yoyote ya tumbaku, pombe au madawa ya kulevya. Hakuna Muislamu aliyemfuata Elijah Muhammad ambaye aliruhusiwa kucheza dansi, kamari, kuwa na wapenzi, kwenda kuangalia filamu au michezo na kuchukua likizo ndefu kazini. Waislamu hawalali zaidi ya inavyopaswa kiafya. Ugomvi wa namna yoyote nyumbani na dharau kwa wanawake havikuruhusiwa. Uongo na wizi havikutakiwa, na ilikuwa ni marufuku kupingana na mamlaka isipokuwa kwa vigezo vya kidini.

Sheria zetu za maadili zilisimamiwa na wanaume wa Fruits of Islam—watu waliofunzwa vizuri na wenye kujitoa hasa. Ukosefu wowote wa maadili ulisababisha mtu asimamishwe na bwana Muhammad au kutengwa kwa muda fulani, au kufukuzwa kabisa kwa wale waliofanya makosa makubwa, “kufukuzwa kutoka kwa watu pekee waliokujali.”

***
 
Sura ya 13 inaendelea

Hekalu Namba Saba lilizidi kukua kwenye kila mkutano. Tatizo ni kuwa sikuridhika na ukuaji wake wa polepole. Kila siku za juma nilikuwa nikisafiri kwa treni na basi. Kila Jumatano nilifundisha katika Hekalu Namba Kumi na Mbili huko Philadelphia. Pia nilienda huko Springfield Massachusetts kujaribu kuanzisha Hekalu jipya. Hekalu ambalo bwana Muhammad aliliita Namba Kumi na Tatu lilikuwa limeanzishwa huko kwa msaada wa ndugu Osborne. Osborne aliusikia Uislamu kwa mara ya kwanza kutoka kwangu tulipokuwa Gerezani. Mwanamke mmoja aliyehudhuria mikutano ya Springfield alinialika kutembelea Hartford alikoishi; alisema iwe ni Alhamisi ijayo na kuwa ataalika baadhi ya rafiki zake. Nilifika bila kukosa.

Alhamisi ilikuwa ni siku ya wafanyakazi wa majumbani kupumzika. Dada yule alikuwa na watu kama kumi na tano nyumbani kwake, wahudumu wa majumbani, wapishi na wanaume waliofanya kazi kwa wazungu wa eneo la Hartford. Mmesikia msemo usemao “hakuna mtu mtakatifu mbele ya mtumishi wake.” Basi watu weusi wale waliofanya kazi zilizowaweka karibu na wazungu walifungua macho haraka kuliko wengine. Hata walipoenda kufanya “uvuvi” walipata wahudumu na watu weusi wengine wengi kutoka eneo la Hartford, ndani ya muda mfupi Bwana Muhammad akawa ameanzisha Hekalu Namba Kumi na Nne huko Hartford, na kila Alhamisi nilifanya mikutano huko.
Bwana Muhammad alikuwa akinikaripia kila mara nilipoenda kumtembelea kule Chicago. Sikuweza kujizuia kuonyesha kuwa Taifa linatakiwa kukua kwa haraka zaidi, maana maimam wake wameiva vya kutosha. Upole na hekima yake wakati akinionya vilininyenyekeza sana. Siku moja alisema kuwa hakuna kiongozi mzuri anayewatwisha watu wake mizigo mizito kuliko wanayoweza kubeba, hakuna kiongozi mzuri anayewalazimisha wafuasi wake waende kwa kasi kuliko wawezavyo.

“Watu wengi wakiona mzee anaendesha gari polepole wanafikiri hataki kwenda kwa kasi,” alisema bwana Muhammad. “Lakini mzee yule anafahamu kuwa kuendesha kwa kasi kutaharibu gari yake nzee. Atakapopata gari yenye kasi ataendesha kasi.” Pia nakumbuka wakati fulani nilipolalamika kuhusu maimam wasio na uwezo kwenye baadhi ya misikiti yake, alisema, “Ni bora niwe na punda ninayeweza kumtegemea kuliko farasi mwenye kasi lakini nisiyeweza kumtegemea.”

Nilijua kuwa bwana Muhammad alitaka lile gari la kwenda kasi. Na hata leo sidhani kama unaweza kupata ndugu na dada kutoka Taifa la Kiislamu ambao wanaweza kufanya “Uvuvi” kushinda wale waliofanikisha kukua kwa Mahekalu ya Boston, Philadelphia, Springfields, Hartford na New York. Nawazungumzia wale niliowajua vyema sababu nami nilihusika moja kwa moja. Wakati huo ilikuwa ni mwaka 1955. Ni mwaka huo ndipo nilifanya safari yangu ya mbali. Ilikuwa ni kwenda kusaidia kufungua Hekalu Namba Kumi na Tano huko Atlanta Georgia.

Muislamu yeyote ambaye alihama mji mmoja kwenda mwingine kwa sababu za kibinafsi alitarajiwa kupanda mbegu za mafundisho ya bwana Muhammad. Ndugu James X, mmoja wa ndugu zetu hodari kutoka Hekalu Namba Kumi na Mbili alikuwa amewavutia watu kadhaa wa Atlanta kiasi kwamba bwana Muhammad aliposhauriwa aliniambia niende Atlanta na kufanya mkutano wa kwanza. Nafikiri mkono wangu ulihusika kwenye karibu Mahekalu yote ya bwana Muhammad, lakini katika yote siwezi kusahau ufunguzi ule kule Atlanta.
Nyumba ya mazishi ndiyo eneo pekee kubwa ambalo ndugu James X aliweza mudu kukodisha. Kila kitu ambacho Taifa la Kiislamu lilifanya wakati huo, kuanzia kwa bwana Muhammad hadi kushuka chini kilikuwa chini ya bajeti kali na kwa kujibana sana. Tulipofika kulikuwa na mazishi ya Mkristo fulani mweusi, yalikuwa ndiyo yanamalizika, ilitubidi kusubiri kidogo na kuangalia waombolezaji walipokuwa wanatoka.
“Mmeona jinsi wanavyolia kwa kufiwa,” niliwaambia watu tulipokuwa tunaingia. “Lakini Taifa la Kiislamu linafuraha juu yenu mliokufa kiakili. Hilo linaweza kuwashtua lakini ni kwa sababu bado hamjatambua jinsi ambavyo jamii yote ya watu weusi hapa Marekani imekufa kiakili. Leo tupo hapa na mafundisho ya bwana Elijah Muhammad yatakayomfufua mtu mweusi kutoka katika wafu. . . .” Na kuongelea kuhusu mazishi-inabidi niseme kuwa hatukuwa kosa kupata Waislamu wapya pale ambapo ndugu wa Muislamu aliyekufa, lakini wao wenyewe wakiwa siyo Waislamu walipohudhuria ibada yetu fupi ya mazishi iliyogusia mafundisho ya bwana Elijah Muhammad, “Wakristo wanafanya ibada ya mazishi kwa ajili ya walio hai, sisi tunafanya kwa ajili ya aliyekufa.”

Nikiwa kama Imam wa mahekalu kadhaa, kuendesha ibada za mazishi lilikuwa jukumu lililoniangukia mara nyingi. Kama ambavyo bwana Muhammad alivyokuwa amenifundisha, nilianza kwa kusoma dua kwa Allah juu ya jeneza la ndugu au dada aliyefariki. Kisha nikasoma historia fupi ya marehemu. Baada ya hapo nilikuwa na kawaida ya kusoma aya mbili kutoka kitabu cha Ayubu. Nilisoma kutoka sura ya saba na ya kumi na nne sehemu ambayo Ayubu anazungumzia kuwa hakuna maisha baada y kifo. Pia nilisoma kutoka sehemu ambayo Daudi anazungumzia kutokuwepo kwa maisha baada ya kifo baada ya kufiwa na mwanawe.

Niliwafafanulia wahudhuriaji kwa nini hatulii, na kwa nini hatuna maua, nyimbo wala kupiga vyombo vya muziki. “Tunamlilia ndugu yetu, na kumpigia muziki anapokuwa hai. Kama hatukumpigia muziki, kumpa maua na kumtolea machozi wakati huo, kufanya hivyo sasa hakuna maana yoyote kwa sababu haelewi chochote. Pesa ambazo tungeweza kutumia kwa mambo hayo tunaipatia familia yake.”

Hapo dada wa Kiislamu walioandaliwa walipitisha sahani ndogo zilizokuwa na pipi kwa waombolezaji. Nilitoa ishara nao waliweka pipi hizo mdomoni. “Sasa tutajipanga ili kumuangalia ndugu yetu kwa mara ya mwisho. Hatutalia kama tu ambavyo hatutalii pipi inavyoyeyuka mdomoni. Kama ambavyo utamu wa pipi unavyoyeyuka ndiyo utamu wa ndugu yetu tuliofurahia alipokuwa hai utakavyokuwa unayeyuka kuingia kwenye kumbukumbu zetu.”

Kulikuwa na Waislamu mia kadhaa walioniambia kuwa ni kupitia kuhudhuria moja ya ibada zetu za mazishi ndipo walipougeukia Uislamu. Lakini baadaye nilikuja kujifunza kuwa mafundisho ya bwana Muhammad juu ya kifo na mazishi ya Kiislamu ni tofauti sana na mafundisho ya Uislamu wa huko Mashariki.

Kufikia mwaka 1956 tulikuwa tumekua kiasi cha kutosha. Kila Hekalu lilikuwa limefanya “uvuvi” wa kutosha kiasi kwamba kwenye miji mikubwa kama Detroit, Chicago na New York kulikuwa na Waislamu wengi kuliko mtu wa nje alivyoweza kudhania. Lakini kama unavyojua, kwenye miji mikubwa unaweza kuwa na kikundi kikubwa lakini kama hakipigi kelele wala kujionyesha kwa umma si rahisi kugundulika kama kipo.

Mbali na kuongezeka kwa Waislamu, pia mafundisho ya Kiislamu ya bwana Muhammad yalianza kuwaingia watu weusi wa aina nyinginezo. Sasa tukaanza kupata watu wenye elimu, wote wenye elimu za ufundi na za kitaaluma. Na hata wengine waliokuwa na “nafasi” kwenye ulimwengu wa mzungu, haya yote yalianza kutupeleka kwenye gari liendalo kasi ambalo bwana Muhammad alitamani kuliendesha. Tulikuwa na watumishi wa serikali, manesi, makarani na maafisa mauzo wa maduka. Na jambo zuri zaidi ni kuwa baadhi ya ndugu hawa walikuwa wanajitoa na kuwa maimam hodari na wenye bidii wa bwana Muhammad.

Nililala muda mchache sana kutokana na bidii yangu ya kusaidia kujenga Taifa letu la Kiislamu. Mwaka huo wa 1956 ndipo bwana Muhammad aliruhusu Hekalu Namba Saba kuninunulia gari ya kutembelea. (Gari ilikuwa mali ya Taifa si yangu. Sikumiliki chochote zaidi ya nguo zangu, saa na sanduku la safari. Kama ilivyokuwa kwa maimam wengine, nililipiwa gharama za kuishi na kupewa pesa ya mfukoni. Zamani hakukuwa na kitu ambacho sikuweza kufanya kwa ajili ya pesa, lakini sasa pesa ilikuwa kitu cha mwisho kabisa kuniingia akilini.) Wakati wa kunijulisha kuwa nitapata gari, bwana Muhammad alisema alifahamu jinsi nilivyopenda kwenda huku na kule kupanda mbegu kwa Waislamu wapya na kwenye Mahekalu mapya, hivyo hakutaka nibanwe sehemu moja.

Ndani ya miezi mitano, kabla ya kupata ajali nilikuwa nimesafiri maili 30,000 na gari ile kwenda kufanya “Uvuvi” Siku moja usiku nilikuwa na ndugu mmoja huko Weathersfield Connecticut niliposimama kwenye taa nyekundu na gari ikaja kutugonga nyuma. Sikuumia, nilipata tu mshtuko. Shetani aliyetugonga alikuwa na mwanamke aliyekuwa akimficha sura, nilitambua kuwa hakuwa mke wake. Tulianza kubadilishana taarifa(Aliishi Meriden, Connecticut), polisi walivyofika ndipo nilitambua kuwa atakuwa mtu mkubwa kwa jinsi walivyomnyenyekea. Baadaye nilikuja kugundua kuwa alikuwa ni mmoja wa wanasiasa wakubwa wa Connecticut; sitamtaja jina. Kwa ushauri wa mwanasheria, Hekalu Namba Saba lilikubali kulipwa fidia na pesa hiyo ikaenda kununua gari aina ya Oldmobile ambayo nimekuwa nikiiendesha hadi leo.

***

Siku zote nilikuwa makini kutokuwa karibu dada yeyote wa Kiislamu. Kujitoa kwangu kabisa kwenye Uislamu kulinitaka kutokuwa na mambo mengine, hasa wanawake. Kwenye karibu kila Hekalu kulikuwa na walau dada mmoja aliyegusia waziwazi kuwa anadhani ninahitaji kuwa na mke. Basi niliweka wazi kuwa sina uhitaji wa ndoa, nilikuwa na shughuli nyingi sana.

Kila mwezi nilipoenda Chicago nilikuta kuna dada amemuandikia Elijah Muhammad, akilalamika kuwa niliongea vikali kuhusu wanawake nilipofundisha darasa maalumu lililohusu tofauti za kinjinsia. Uislamu unamafundisho na sheria kali kuhusu wanawake. Msingi wake ni ukweli kuwa kiasili ya mwanaume ni nguvu na mwanamke ni udhaifu, japokuwa mwanaume anatakiwa kumheshimu mwanamke wake siku zote, lakini kama anatarajia kuheshimiwa naye, kuna wakati anatakiwa kuelewa kuwa anatakiwa kumuongoza.

Lakini wakati ule nilikuwa na sababu zangu binafsi. Sikuwahi wazia uwezekano wa mimi kumpenda mwanamke yeyote yule. Nilikuwa na uzoefu wa kutosha ulionionyesha kuwa wanawake ni viumbe walaghai, wenye hila na
wasioaminika. Nilishuhudia wanaume wengiwakiharibiwa maisha yao na wanawake. Nilikuwa na mtazamo kuwa wanawake wanaongea sana. Kumwambia mwanamke asiongee sana ni kama kumwambia Jesse James asibebe bunduki, au kuku asipige kelele. Inakuingia akili Jesse James bila bunduki au kuku asiyepiga kelele! Na mtu yeyote aliye kiongozi, kama nilivyokuwa, kosa baya zaidi analoweza kufanya duniani ni kuwa na mwanamke asiyefaa. Hata Samsoni, binadamu mwenye nguvu kuliko wote aliangamizwa na mwanamke aliyelala kwenye mikono yake.

Nilikuwa na uzoefu wa kutosha. Nilikuwa nimeongea na makahaba na vimada wengi sana. Walijua mengi kuhusu waume kuliko hata wake wa wanaume hao. Mara zote wake walijaza masikio ya waume zao kwa malalamishi, hivyo si wake bali makahaba na vimada ndiyo waliosikia matatizo na siri za ndani kabisa za wanaume. Walimfikiria mwanaume na kumliwaza na kumsikiliza, naye aliwaambia kila kitu.

Wakati huo ilikuwa imepita miaka kumi toka nifikirie kuwa na mwanamke. Sikuwa na mawazo ya kuwa na mke, naye bwana Muhammad linitia moyo kuendelea kuwa mseja.

Dada wa Hekaluni waliozoea kuwaambia ndugu, “Hamuoi kwa sababu ndugu Malcom haonyeshi kuvutiwa na mtu yeyote.” Haikuwa hivyo hata kidogo, sikuwahi kuwaficha dada wale jinsi ninavyohisi, na ni kweli kuwa niliwaambia ndugu wale wawe makini sana.

Kuna huyu dada alijiunga na Hekalu Namba Saba mnamo mwaka 1956. Nilikuwa tu nimemuona lakini sikuwa na lengo lolote juu yake, kamwe hangeingiwa na mawazo kuwanilikuwa namfikiria. Pengine hata usingeweza kumuaminisha kuwa nilifahamu jina lake. Alikuwa ni dada Betty X. Alikuwa ni mrefu, rangi yake maji ya kunde na macho ya kahawia.

Nilifahamu kuwa alikuwa mwenyeji wa Detroit na wakati huo alikuwa akisoma shahada ya elimu huko chuo kikuu cha Tuskegee, Alabama. Alikuja New York kwenye chuo cha unesi cha hospitali moja kubwa. Alifundisha darasa la afya na usafi kwa wanawake na wasichana wa Kiislamu.

Inabidi kufafanua kuwa kila siku ya juma usiku kulikuwa na darasa au tukio fulani la Kiislamu lililoendeshwa. Jumatatu kulikuwa na mafunzo ya Fruit of Islam. Watu hudhani huwa ni mafunzo tu ya kivita, judo, karate na mambo kama hayo. Hayo ni sehemu tu ya mafunzo ya Fruit of Islam. Fruit of Islam hutumia muda mwingi zaidi wakijifunza na kujadiliana jinsi ya kuwa wanaume hasa. Walijifunza wajibu wa mume na baba; mambo ya kutarajia kutoka kwa wanawake; haki za mwanamke ambazo hazitakiwi kuingiliwa na mumewe; umuhimu wa uwepo wa baba kwenye nyumba imara; matukio ya karibuni; kwa nini uaminifu na maadili ya kingono ni muhimu kwa mtu mmoja mmoja, nyumbani, kwenye jamii, katika nchi na kwa ustaarabu mzima; kwa nini ni muhimu kwa mtu kuoga walau mara moja kila baada ya saa ishirini na nne; kanuni za biashara; na mambo kama hayo.

Kila Jumanne usiku ilikuwa ni Usiku wa Umoja kwenye mahekalu yote. Usiku huo ndugu na dada walifurahia mazungumzo na viburudisho kama biskuti, juisi za matunda nk.

Jumatano usiku ilikuwa ni siku ya kuandikisha wanafunzi; ni siku ambayo misingi ya Kiislamu ilijadiliwa; ni kama darasa ya katekisimu kwa Wakatoliki.

Alhamisi usiku ilikuwa ni siku ya mafundisho kwa wasichana wa Kiislamu na ustaarabu kwa ujumla. Hapo wasichana na wanawake wa Kiislamu walifundishwa kutunza nyumba, jinsi ya kulea watoto, kumhudumia mume, jinsi ya kupika, kushona na mambo mengine ya muhimu katika kumfanya mtu kuwa dada, mama na mke bora wa Kiislamu.
Ijumaa ilikuwa ni usiku wa Ustaarabu, dada na ndugu walifundishwa mambo kuhusu uhusiano wa nyumbani, walisisitizwa jinsi ambavyo wote mke na mume wanatakiwa kuelewa na kuheshimu uhalisia wa mwingine. Jumamosi usiku ilikuwa ni siku huru kwa Waislamu wote, kawaida walitembeleana majumbani. Na Jumapili ilikuwa ni siku ambayo kila Hekalu lilifanya ibada yake rasmi.

Kuna baadhi ya Alhamisi nilihudhuria darasa la wasichana, labda moja ya madarasa ya dada Betty X kama tu ambavyo nilihudhuria madarasa ya siku nyingine pia. Mwanzoni nilimuuliza tu vitu kama mafunzo yanaendeleaje, naye alijibu , “Vyema Ndugu Imam.” Nami nilisema, “Ahsante sana dada.” Hivyo tu. Baada ya muda nikaanza kuwa na maongezi mafupi tu ya kirafiki.

Siku moja niliwaza kuwa itakuwa vyema kwa darasa la wanawake iwapo nikimpeleka dada Betty X kwenye jumba la
makumbusho ya historia ya asili—akiwa kama mkufunzi. Nilitaka kumuonyesha habari za mageuzi ya binadamu ambazo nilionelea zitamsaidia kwenye mafundisho yake. Nilitaka kumuonyesha ushahidi wa mafundisho ya bwana Muhammad, kama ushahidi kuwa nguruwe ni panya mkubwa tu. Bwana Muhammad alitufundisha kuwa nguruwe ni mchanganyiko wa panya, paka na mbwa. Nilipomwambia dada Betty X wazo hilo, niliweka wazi kuwa ni kwa ajili ya kusaidia darasa lake. Hata niliweza kujiaminisha kuwa hiyo ndiyo sababu hasa.

Mchana wa kwenda ulipofika nilimpigia simu; nilimwambia kuwa nimeahirisha safari kwa sababu jambo fulani la muhimu limejitokeza. Alisema, “Umechelewa sana kuniambia ndugu Imam, ndiyo nilikuwa natoka. Basi nikamwambia aje nitajitahidi twende lakini sitakuwa na muda wa kutosha.

Tulipokuwa kule nilimuuliza kila aina ya maswali. Nilitaka kujua namna yake ya kufikiri. Nilivutiwa sana na uelewa wake. Wakati huo alikuwa ni mmoja wa watu wachache sana tuliokuwa nao ambao walikuwa wamefika chuo.
Muda mfupi baada ya hapo, dada mmoja mtu mzima alinieleza juu ya tatizo binafsi lililokuwa linamkabili dada Betty X. Nilishangaa sana kuwa dada Betty X hakunieleza chochote alipokuwa na nafasi ya kutosha kufanya hivyo. Kila Imam alikuwa akisikia matatizo ya vijana ambao walikuwa wanasakamwa na wazazi wao kwa kuwa Waislamu. Basi hata dada Betty X alipowaambia wazazi wake walezi waliokuwa wakilipia masomo yake kuwa amekuwa Muislamu walimpa machaguao mawili; aachane na Uislamu au waache kumlipia masomo ya unesi.

Ilikuwa ni karibu na mwisho wa muhula-lakini aliendelea kushikamana na Uislamu. Alianza kufanya kazi za uyaya kwa madaktari walioishi eneo la hospitali alikosoma ili apate pesa ya kujilipia masomo.
Kulingana na nafasi yangu, sikuweza kuchukua hatua yoyote kabla ya kufikri jinsi hatua hiyo itakavyoathiri Taifa la Kiislamu.

Nikaanza kufikiria itakuwaje iwapo nitaoa? Labda kumuoa dada Betty X—ningeweza kumuoa dada yoyote kutoka Hekalu lolote lakini dada Betty X angekuwa na urefu unaomfaa mtu wa urefu wangu, na pia umri wake ungefaa sana kwa mtu wa umri wangu.

Bwana Muhammad alitufundisha kuwa mwanaume mrefu kuoa mwanamke mfupi sana au kinyume chake haipendezi. Na kuwa umri sahihi wa mwanamke ni nusu ya umri wa mwanaume jumlisha miaka saba. Alitufundisha kuwa wanawake wanawahi kukomaa kuliko wanaume. Aliongeza kuwa hakuna ndoa inayoweza kudumu iwapo mke hajinyenyekezi na kumheshimu mumewe, na kwamba mume anatakiwa kumzidi mke vitu fulani ili mke aweze kumtegemea kisaikolojia.

Nilishtushwa sana na mawazo yangu hayo, niliacha kabisa kumkaribia dada Betty X au kukaribia popote pale nilipojua atakuwepo. Kama aliingia kwenye mgahawa wetu na mimi nimo humo, niliondoka kwenda sehemu nyingine. Nilifurahi kujua kuwa hakuwa na wazo lolote juu ya niliyokuwa nafikiria kichwani mwangu. Kutoongea naye kusingemfanya ahisi jambo lolote maana hatukuwa na mazoea ya kuongea mambo binafsi.

Nilifikiria atanijibu nini iwapo nikimwambia? Nimesikia wanawake wengi wakijisifu, “Nilimwambia yule mpumbavu anikome.” Nilikuwa na uzoefu wa kutosha kumfanya mwanaume kuwa na tahadhari.

Nilifahamu jambo moja zuri kumhusu. Alikuwa na ndugu wachache. Mawazo yangu juu ya ndugu wa upande wa mke ni kuwa walikuwa watata tu. Palepale kwenye Hekalu Namba Saba nilishuhudia ndoa nyingi zikivunjwa na wakwe, mashemeji na mawifi, mara nyingi wale wenye chuki dhidi ya Uslamu.

Sikutaka kuongea mambo yoyote ya mahaba ambayo wanawake wamejazwa vichwani na filamu za Hollywood na kwenye luninga. Nilidhamiria kuwa kama nitachukua hatua basi nitaenda moja kwa moja kwenye lengo. Na chochote nitakachofanya nitafanya kwa namna ninayotaka mimi, na kwa sababu nimeamua mwenyewe kufanya. Si kwa sababu niliona mtu fulani akifanya. Au kukisoma kitabuni. Au nilikiona kwenye filamu mahali fulani.

Nilipomtembelea bwana Muhammad mwezi huo kule Chicago nilimjulisha kuwa nilikuwa nikichukua hatua fulani. Alitabasamu aliposikia jambo lenyewe.

Nilimwambia nilikuwa nikilifikiria tu. Bwana Muhammad aliniambia kuwa atapenda kuonana na dada huyo.
Wakati huo Taifa lilijiweza kidogo kipesa kiasi kwamba liliweza kuwasafirisha wakufunzi wanawake kwenda makao makuu kwenye Hekalu Namba Mbili huko Chicago, kuhudhuria mafunzo ya wanawake na kuonana na Mtukufu Elijah Muhammad ana kwa ana. Dada Betty X alifahamu jambo hili vyema hivyo hakuwa na sababu ya kushuku jambo lolote mipango ya yeye kwenda Chicago ilipofanywa. Na kama wakufunzi wote, naye pia alikuwa mgeni nyumbani kwa Mtume na dada Clara Muhammad.

Bwana Muhammad aliniambia kuwa anadhani kuwa dada Betty X ni mtu mwenye tabia njema sana.
Kama unafikiria kufanya jambo, inatakiwa kuamua kama utalifanya au la. Jumapili moja usiku, baada ya mkutano Hekaluni, niliendesha gari kwenda kuonana na kaka yangu Wilfred huko Detroit. Mwaka mmoja uliopita, yaani 1957, Wilfred alikuwa amefanywa kuwa Imam wa Hekalu Namba Mbili la huko Detroit. Nilikuwa sijaonana naye au na mwanafamilia wangu mwingine yeyote kwa muda mrefu kidogo.

Nilifika Detroit saa kumi alfajiri. Nilipokuwa najaza mafuta kituoni, nikaamua tu kwenda kwenye simu yao na kumpigia dada Betty X. Ilinibidi kutafuta namba ya makazi ya manesi kwenye hospitali aliyosoma. Niliweka namba nyingi kichwani lakini kwa makusudi sikutaka kuweka namba ya Betty X. Mwishowe nikampata hewani. Alisema, “Oh, Hello,
Ndugu Imam-“ Nilimwambia bila kuuma maneno, “Vipi, unataka kuolewa?”

Kwa asili alifanya kushtuka na kushangaa sana. Kila ninapowaza jambo lile ndivyo hadi leo hii ninavyoamini kuwa alikuwa anaigiza tu. Sababu wanawake huwa wanajua, wanajua vizuri kinachoendelea.

Kama nilivyotarajia, alisema “ndiyo.” Kisha nikasema kwamba sina muda mwingi hivyo apande ndege na aje Detroit.
Basi akachukua ndege ya Detroit. Nilionana na wazazi wake walezi walioishi Detroit. Wakati huo walikuwa wameishaelewana. Walikuwa wakarimu sana na wenye furaha, walau walionekana hivyo.

Baada ya hapo nikamtambulisha dada Betty X nyumbani kwa kaka yangu mkubwa Wilfred. Nilikuwa nimeishamuuliza juu ya mahali ambako watu wanaweza kufunga ndoa bila mambo mengi wala kusubiri. Aliniambia ni huko Indiana.

Mapema asubuhi iliyofuata nilimpitia Betty X nyumbani kwa wazazi wake. Tuliendesha hadi kwenye mji wa kwanza kuukuta tulipoingia jimbo la Indiana. Huko tulikuta kuwa kumbe siku chache zilizopita jimbo lilikuwa limebadili sheria yao ya ndoa, hivyo kulikuwa na kipindi kirefu cha kusubiria.

Hii ilikuwa ni Jumanne ya tarehe kumi na nne, mwezi wa kwanza wa mwaka 1958. Hatukuwa mbali na Lansing alikoishi kaka yangu Philbert. Tulienda huko. Philbert alikuwa kazini nilipofika na kumtambulisha dada Betty X. Betty X alikuwa akiongea na mke wa Philbert nilipojulishwa kwa njia

ya simu kuwa kama tukiharakisha mambo tunaweza kufunga ndoa ndani ya siku moja.
Tulifanya vipimo vya damu vilivyotakiwa kisha tukapata leseni. Nilijaza “Muislamu sehemu ya dini” kisha tukaenda kwa Hakimu wa Amani(Justice of Peace). Mwanamme mmoja wa kizungu, mzee mwenye kibyongo ndiye alitufungisha ndoa. Mashahidi wote walikuwa wazungu. Tulisema viapo vyetu. Hatimaye shetani yule mzee akasema, “Nawataja kama mke na mume, unaweza kumbusu mkeo.”

Tuliondoka mara moja. Hakukuwa na mambo yote yale ya kwenye filamu! Mambo kama wanawake kutaka wanaume wawabebe, na wengine wakiwa wazito kuliko mwanaume. Sijui ni ndoa ngapi zinavunjika kwa sababu ya wanawake waliokuwa waraibu wa filamu na luninga kutaka mambo ya kukumbatiana, kubusiana, kucheza dansi na kubebana lakini wakaishia kukasirika pale ambapo mume anapotoka kazini kachoka na kajaa jasho kwa kufanya kazi kama mbwa siku nzima, akitaka tu chakula.

Tulipata chakula chetu nyumbani kwa Philbert. Aliporudi kutoka kazini na kusikia kuwa nilikuja kumtambulisha dada wa Kiislamu, alitambua kuwa nilikuwa nimeoa au naenda kuoa.

Chuoni kulimtaka Betty arudi New York mara moja, angeweza kurejea tena Detroit ndani ya siku nne. Alidai kuwa hajamjulisha yoyote kwenye Hekalu Namba Saba kuwa tumeoana.

Jumapili ya juma hilo, bwana Muhammad alikuwa anakuja Detroit kufundisha Hekalu Namba Moja. Wakati huo New York nilikuwa na Imam msaidizi. Nilimwambia kuwa aendeshe ibada badala yangu. Jumamosi Betty akawa amerudi. Baada ya mafundisho ya Jumapili, Mtume akatangaza ndoa yetu. Hata watu wa Michigan walifahamu vyema kuwa nilikaa mbali na wakina dada, hawakuamini kusikia nimeoa.

Tuliendesha kurudi New York. Habari za ndoa yetu zilimshangaza kila mtu kwenye Hekalu Namba Saba. Baadhi ya ndugu vijana walinitazama kama vile nimewasaliti. Lakini kila mtu alikuwa anakenua kama paka wa Cheshire. Dada hawakuacha kumzonga Betty. Sitasahau kumsikia mmoja wao akisema kwa mshangao, “Umempata!” Kama tu nilivyokuwa nakwambia wanawake walivyo. Alinipata. Hiyo ndiyo moja ya sababu sijawahi acha kuamini kuwa alijua kuna kitu kinachoendelea. Pengine ni kweli alinipata!

Miaka miwili iliyofuata tuliishi Queens, tukishirikiana nyumba ndogo na ndugu John A. H na mke wake wa wakati huo. Sasa hivi ni Katiba wa Taifa huko Chicago.

Binti yetu mkubwa, Atallah alizaliwa mwezi wa kumi na moja ya mwaka 1958. Alipewa jina la Attilah the Hun(Mtu aliyeuteka mji wa Roma). Mara tu baada ya Attalah kuzaliwa tulihamia kwenye eneo la watu weusi huko Long Island, Queens-kwenye nyumba yetu ya vyumba saba tunayoishi mpaka sasa.

Binti yetu mwingine, Qubillah (Jina la Qubilah Khan) alizaliwa siku ya Krisimasi ya mwaka 1960. Kisha akaja Yasah(Elijah kwa kiarabu ni Ilyas) alizaliwa mwezi wa saba mwaka 1962. Mwaka 1964 alizaliwa binti yetu wa nne Amilah alizaliwa.

Nadhani sasa naweza sema kuwa nampenda Betty. Ni mwanamke pekee niliyewahi fikiria kumpenda. Na ni mmoja kati ya wanawake wanne tu niliowahi kuwaamini. Jambo zuri ni kuwa Betty ni Muislamu mwema na mke mwema. Iko wazi kuwa Uislamu ndiyo dini pekee inayowafanya mke na mume waelewe upendo ni nini. Ukiuchunguza upendo wa kimagharibi utaona kuwa ni tama za ngono tu. Upendo unapita ni zaidi ya mambo ya kimwili. Upendo ni fikra, tabia, mtazamo, mapendezi-mambo yanayomfanya mwanamke kuwa mzuri. Huu ndiyo uzuri usiochuja. Kwenye ustaarabu wa magharibi utaona kuwa mke anapopoteza uzuri wake na mvuto kwa mume wake unapotea. Lakini Uislamu unatufundisha kumuangalia mke kama alivyo ndani yake na yeye kutuangalia hivyohivyo.

Betty anafanya hivyo, na hivyo ananielewa vyema. Naweza kusema kuwa sipati picha wanawake wengine wakiweza kuishi nami. Betty anaelewa kuwa kazi yangu ya muda wote ni kumuamsha mtu mweusi aliyeshikwa akili na kumwambia shetani wa kizungu ukweli wake. Nikiwa na kazi ya kufanya kwa muda mfupi ninapokuwa nyumbani, ananipa utulivu wa kuifanya. Ni mara chache sana nimekuwepo nyumbani kwa zaidi ya nusu juma; wakati mwingine sikuwepo nyumbani kwa miezi mitano. Sijawahi pata muda wa kutosha kutoka naye, na nafahamu kuwa anapenda kuwa karibu na mumewe. Ameshazoea kupokea simu zangu nikiwa viwanja vya ndege kotekote Marekani, kutoka Boston hadi San Franscisco au Miami hadi Seattle, au hivi karibuni nilivyompigia kutoka Cairo, Accra au kutoka mji mtakatifu wa Mecca. Siku moja tulipoongea kwa simu nikiwa mbali, Betty aliniambia anavyohisi kwa namna nzuri sana. Alisema, “Unakuwa pampoja name unapokuwa mbali.”

Baadaye katika mwaka ule tuliooana, nilifanya kazi kwa nguvu sana—nikijaribu kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja, nikijaribu kusaidia kukuza Taifa. Nilipokuwa nikifundisha kama Imam mgeni kwenye Hekalu la Boston, nilimalizia kwa kusema kama kawaida, “Nani kati yenu anataka kuwa mfuasi wa Elijah Muhammad?” nilistaajabu sana nilipoona kati ya wale wanaosimama alikuwepo dada yangu, Ella! Tulikuwa na msemo kuwa wale ambao ni wagumu zaidi kuwasilimisha ndiyo huwa Waislamu bora kabisa. Na kumsilimisha Ella ilichukua miaka mitano.

Unakumbuka nimesema kuwa kwenye jiji kubwa kikundi kinaweza kuwepo bila kujulikana kabisa mpaka kitokee kitu kitakachofanya jamii ikitazame. Basi hakuna yeyote ndani ya Taifa la Kiislamu aliyetarajia jambo lililotokea Harlem usiku mmoja.

Polisi wawili wa kizungu waliokuwa wanaamulia ugomvi wa watu weusi waliwaamuru waliokuwa wanashuhudia kuondoka. Kati ya hawa waliokuwa wanashuhudia

walikuwepo Waislamu wawili, ndugu Johnson Hinton na ndugu mwingine kutoka Hekalu Namba Saba. Hawakutawanyika na kukimbia kama polisi walivyotaka. Ndugu Hinton alipigwa fimbo na akapasuka kichwani, kisha gari ya polisi ikaja na akachukuliwa hadi kituo cha polisi cha karibu.

Ndugu yule wa pili akapiga simu mgahawani kwetu. Simu zikapigwa na ndani ya nusu saa wanaume kama hamsini wa Fruit of Islam Kutoka Hekalu Namba Saba wakawa wamejipanga nje ya kituo cha polisi.

Watu weusi wengine ili kuona kinachoendelea walikuja na kujipanga nyuma ya Waislamu. Polisi waliotoka mlango wa mbele na wale waliochungulia kupitia madirishani hawakuamini walichokiona. Niliingia ndani kama Imam wa Hekalu Namba Saba na kuomba kuonana na ndugu yetu. Mwanzoni polisi walisema hayupo pale. Kisha wakakubali yupo lakini wakasema sitaweza kumuona. Niliwaambia kuwa Waislamu wataendele kubaki pale mpaka tutakapomuona na kuhakikisha kuwa anapata matibabu stahiki, Waliingiwa na wasiwasi juu ya umati uliokuwa umekusanyika pale nje. Nilipomuona ndugu yetu Hinton nilijitahidi sana kujizuia. Alikuwa hajielewi sawa sawa. Damu ilimtapakaa kichwani, mabegani na usoni. Natumaini kutokuja kuona tena ukatili wa polisi kama ule.

Nilimwambia luteni kuwa “Mtu huyu anatakiwa kuwa hospitali.” Waliita gari ya wagonjwa. Lilipofika na kumpeleka ndugu Hinton hospitali ya Harlem, Waislamu tulilifuata kupitia barabara ya Lenox. Watu weusi ambao hawakuwahi kuona kitu kama kile, walitoka madukani na kwenye migahawa na kutufuata, umati ulizidi kuongezeka.
Nje ya hopsitali ya Harlem umati uliokuwa nyuma ya Waislamu ulikuwa mkubwa na uliojaa hasira. Kwa muda mrefu watu weusi wa Harlem walikuwa wamechoshwa na ukatili wa polisi. Kamwe hawakuwahi kuona wanaume weusi wakionyesha msimamo kama tulioonyesha.

Polisi mmoja mwenye cheo alinifuata na kusema, “Waondoe hao watu hapo nje.” Nilimuambia kuwa ndugu zetu walikuwa wamesimama kwa amani, kwa nidhamu na hawakuwa wakimdhuru yeyote. Aliniambia kuwa wale wengine nyuma yao hawakuwa na nidhamu nami nilimwambia kuwa wale wengine ni jukumu lake.

Madaktari walipotuhakikishia kuwa ndugu yetu anapata huduma anayostahili, nilitoa amri na Waislamu wakaondoka. Watu weusi wengine walijawa na hasira lakini nao waliondoka pia mara tulipoondoka. Hapo baadaye tukaja kujua kuwa ndugu Hinton alitakiwa kuwekewa chuma kwenye fuvu. (Baada ya kufanyiwa upasuaji, Taifa la Kiislamu likamsaidia kufungua mashtaka na akalipwa dola 70,000, ilikuwa ni fidia kubwa kabisa kuwahi kulipwa na jiji la New York kwa sababu ya ukatili wa polisi)

Kwa mamilioni ya watu wa New York waliosoma magazeti kutoka mjini-kati , tukio hilo lilikuwa ni moja tu ya vurugu nyingi zilizotokana na ubaguzi wa rangi katika Harlem. Haikuwa habari kubwa, lakini kwa hakika idara ya polisi
ilichukua na kusoma kwa makini jalada lililohusu Taifa la Kiislamu na kuanza kututazama kwa jicho la tofauti. La muhimu zaidi, Huko Harlem, eneo la maghetto ya watu weusi lenye watu wngi zaidi duniani-gazeti la Amsterdam News liliandika kisa kizima, na kwa mara ya kwanza watu weusi- wanawake kwa waume na watoto mitaani wakaanza kusema, “Waislamu wale-”

Mwisho wa sura ya 13
 
Hatari sana
 
Sura ya 14

WAISLAMU WEUSI​


Wakati wa majira ya kuchipua ya mwaka 1959, miezi kadhaa kabla kesi ya ndugu Johnson Hinton haijawaamsha watu weusi wa Harlem kuwatambua Waislamu-mwanahabari mweusi aliyeitwa Louis Lomax ambaye wakati huo alikuwa akiishi New York, aliniuliza asubuhi moja iwapo Taifa la Kiislamu litakubali kuchukuliwa video kwa ajili ya documentary, kwa ajili ya kipindi cha Mike Wallace kilichokuwa kikizungumzia masuala yeye utata. Nilimwambia Lomax kuwa kwa kawaida jambo kama hilo linatakiwa kupitia kwa Mtukufu Elijah Muhammad. Lomax alipanda ndege hadi Chicago kwenda kuongea na bwana Muhammad. Baada ya bwana Muhammad kumhoji Lomax na kumtahadharisha juu ya mambo ambayo hangependezwa nayo, alimpa ruhusa.

Wachukua picha za video wakaanza kuchukua video za Taifa la Kiislamu kwenye misikiti yetu ya New York, Chicago na Washington D. C. Rekodi za sauti za bwana Muhammad, na baadhi ya maimam, nikiwepo mimi zilichukuliwa. Tukifundisha ukweli juu ya mtu mweusi aliyeshikwa akili na shetani wa kizungu.

Wakati huo huo kulikuwa na msomi mweusi aliyekuwa akifanya masomo ya uzamivu katika chuo kikuu cha Boston,
aliitwa C. Eric Lincoln. Bwana huyu alikuwa amechagua kufanya utafiti juu ya Taifa la Kiislamu. Lincoln alikuwa amechochewa kufanya utafiti mwaka mmoja uliopita alipokuwa akifundisha chuo cha Clark huko Atlanta, Georgia. Mwanafunzi wake mmoja mshika dini aliwasilisha kazi yake ya muhula ambayo leo naweza kuinukuu kutoka katika kitabu cha Lincoln. Lilikuwa ni tamko kutoka kwa wanafunzi wengi weusi wa chuo katika eneo la Atlanta waliohudhuria Hekalu letu Namba Kumi na Tano. Waliandika:
“Dini ya Kikristo haiendani na matakwa ya mtu mweusi ya kujiheshimu na kutaka usawa katika Marekani,” aliandika mwanafunzi yule. ‘Imekwamisha mahali ilipotakiwa kusaidia; imewagawa waumini kulingana na rangi zao japokuwa inatangaza kuwa lengo lake ni kuleta undugu wa kidunia chini ya Yesu Kristo. Upendo wa Kikristo ni upendo wa mzungu kujipenda mwenyewe na jamii yake. Kwa mtu ambaye si mzungu, Uislamu ndiyo tumaini lake kwa ajili ya haki na usawa wa dunia ya kesho tunayotaka kuijenga.’

Baada ya tafiti za mwanzo kumuonyesha professor Lincoln ukubwa wa jambo hilo, na baada ya kutiwa moyo na kupata udhamini, aliweza kupanua utafiti wake kuwa kitabu.

Mambo haya mawili makubwa, kuandikiwa kitabu na kuonekana kwenye luninga zilikuwa habari kubwa kwa Taifa letu dogo. Kila Muislamu alisubiria kwa furaha kwamba kupitia vyombo vikubwa vya habari vya mzungu, ndugu na dada weusi walioshikwa akili Marekani kote pamoja mashetani-wataenda kusikia, kuona na kusoma mafundisho
ya bwana Muhammad, mafundisho yaliyokata kama upanga wenye makali kuwili.

Tulikuwa tumejitahidi kwa uwezo wetu kutumia nguvu ya uchapishaji. Mwanzoni, huko nyuma kidogo nilikuwa nimefanya miadi ya kuonana na mhariri wa gazeti la Amsterdam News, James Hicks. Gazeti hilo lilichapishwa Harlem. Hicks alisema maoni yake ni kuwa kila sauti katika jamii inahaki ya kusikika. Baada ya muda mfupi, kila juma kulikuwa na makala fupi niliyoandika kwenye gazeti la Amsterdam News. Baadaye bwana Muhammad akakubali kuandika yeye mwenyewe makala kwenye nafasi ile adimu kwenye gazeti la Amsterdam News, na mimi makala zangu zilihamishiwa kwenye gazeti lingine la watu weusi, Herald Dispatch la huko Los Angeles.

Pamoja na hayo, bado nilikuwa nataka tuwe na gazeti letu wenyewe lililojaa habari za Kiislamu.

Mwaka 1957 bwana Muhammad alikuwa amenituma Los Angeles kuanzisha Hekalu huko. Nilipokamilisha hilo, nilienda ofisi za Herald Dispatch. Waliniruhusu kuona jinsi magazeti yanavyoandaliwa. Siku zote nimebarikiwa uelewa kiasi kwamba nikiona kitu kinafanywa mara moja tu, basi nami naweza kukifanya. Pengine kudaka vitu haraka ndiyo ilikuwa kanuni kuu ya kuweza kuishi mtaani wakati nilipokuwa mpambanaji.

Niliporudi New York nilinunua kamera, sijui nilipiga picha ngapi mpaka nilipoweza kupiga picha nzuri. Kila nilipopata nafasi niliandika habari fupi kuhusu mambo yanayotokea kwenye Taifa la Kiislamu. Nilitenga siku moja kila mwezi na kupanga vizuri maandiko yangu na picha kwa ajili ya kuchapicha kwenye mashine Niliiita gazeti hilo Muhammad Speaks na ndugu wa Kiislamu waliliuza kwenye maeneo ya maghetto. Sikuota kabisa kuwa hapo baadaye wivu ulipoingia, hakuna jambo langu lolote litakuja kuchapishwa kwenye gazeti nililolianzisha. Tukiachana na hilo, bwana Muhammad aliponituma Afrika kwa ziara ya majuma matatu. Pamoja na udogo wetu lakini kulikuwa na baadhi ya watu kutoka Afrika na Asia waliomtumia bwana Muhammad ujumbe kumwambia kuwa walipendezwa na jitihada zake za kuwaamsha na kuwainua watu weusi wa Marekani. Nyakati nyingine jumbe hizo zilitumwa kupitia mimi. Nikiwa kama muwakilishi wa bwana Muhammad nilienda Misri, Arabia, Sudan, Nigeria na Ghana.
Leo hii utawasikia viongozi wengi wa watu weusi wakilalamika kuwa kilichowapa Waislamu umaarufu kimataifa ni magazeti, redio, luninga na vyombo vingine vya habari vya mzungu. Sibishi hilo hata kidogo. Sababu ni kuwa hakuna hata mmoja wetu kwenye Taifa la Kiislamu aliyetarajia kilichoenda kutokea.

***

Mwishoni mwa mwaka 1959 kile kipindi cha televisheni kilichokuwa kinaandaliwa kiliruka hewani. “Chuki iliyozalishwa na chuki-” kichwa chake kilisema.Kilihaririwa kwa kuwekwa picha za kutisha huku bwana Muhammad, mimi na wengine tukisikika tukiongea. Waislamu walionekana kwenye migahawa na biashara zetu zingine . . . Waislamu na watu weusi wengine wakiingia na kutoka kwenye misikiti yetu. . . .
Kila sentesi ilihaririwa ili kuongeza ukali. Nadhani watu walikaa wakiwa wameishiwa nguvu mara kipindi kile kilipoisha, nadhani hilo ndilo lilikuwa lengo la mtayarishaji.
Kwa namna fulani, muitikio wa jamii ulikuwa kama ule uliotokea miaka ya 1930 pale Orson Welles alipoitia hofu Marekani kupitia kipindi chake cha redio kwa kuelezea kama vile ni kweli Marekani ilikuwa inavamiwa na watu kutoka Mars.
Wakati huu hakuna aliyeruka kutoka madirishani lakini katika jiji; la New York kulitokea kelele kubwa sana. Maoni yangu ni kuwa kichwa cha kipindi, “Chuki. . . Chuki. . .” kilichangia sana mlipuko ule. Mamia elfu ya watu wa New York, weupe kwa weusi walipiga kelele, “Umesikia? Umeona? Wanahubiri kuchukia wazungu!”

Hapa ilionekana tabia ya kawaida ya mzungu anayoonyesha kuelekea mtu mweusi. Mzungu anajipenda sana kiasi kwamba hushtuka pale anapogundua kuwa wahanga wake hawana maoni kama yake katika kujikweza kwake na kujiona mtu bora. Kwa karne nyingi hapa Marekani kumekuwa hakuna tatizo kadri ambavyo watu weusi wanaonyonywa na kukandamizwa wamekuwa wakikenua na wakiomba na “ku-ndiyo Bwana.” Na matendo mengine ya ukibaraka. Lakini sasa mambo yalikuwa tofauti. Kwanza yalianza kutoka magazeti ya kizungu ambayo ndani yake
kulikuwa na makala “zilizotahadharisha” juu ya uwepo wa “mitume waenezao chuki . . . watu tishio juu ya uhusiano mzuri uliopo kati ya watu wa rangi tofauti . . . watu weusi wanaohubiri utengano . . . weusi wenye kujikweza, “ na mambo mengine kama hayo. Kabla hata ya wino wa magazeti hayo haujakauka, jarida moja kubwa la habari nchini linalotoka kila juma likaanza: “Walimu wa chuki”. . . “Wachochea vurugu:”. . . “Wabaguzi wa rangi weusi:” “Mafashisti weusi:” “Wapinga Ukristo:”. . . “Kuna uwezekano wamechochewa na wakomunisti ”
Baada ya machapisho hayo, mzungu aliyechochewa na habari hizi akachukua hatua.

Tokea wakati wa utumwa mzungu alikuwa amechagua manegro wachache ambao aliwatunza vizuri kuliko watu weusi wengine waliotaabika na kuteseka kwenye joto mashambani. Mzungu aliwatumia manegro hawa wa “Nyumbani na uani” kama watumishi wake maalumu. Hawa aliwatupia makombo mengi zaidi kutoka mezani pake kuliko wale wengine waliofanya kazi shambani, hata aliwaruhusu wale jikoni mwake. Alijua kuwa siku zote hawa watamfurahisha kwa kusifia sifa nzuri alizojipa, “Kwamba ni mwema na mwenye haki.” Siku zote “bwana mwema” alisikia mazuri tu kumhusu kutoka kwa manegro hawa. “Wewe ni bwana mwema sana!” au “Oh, bwana, wale watu weusi wanaofanya kazi mashambani wanafurahia kazi yao na maisha yao vilevile yalivyo; hawana akili za kutosha hata ukisema uwafanyie kitu kuboresha maisha yao ni kazi bure-”

Basi watu weusi hao wa “nyumbani na uani” wa enzi zetu wamekuwa wajanja tu ukilinganisha na wale wa enzi za utumwa, huo ndiyo ukweli. Leo mzungu ananyanyua tu simu na kumpigia mnegro wake wa “nyumbani na uani.” Hahitaji hata kumfundisha kibaraka wake huyu ch kusema. Tayari walikuwa wameona kipindi cha televisheni na wamesoma magazeti. Tayari walikuwa wanaandaa majibu. Walijua cha kufanya.

Sitawataja kwa majina, lakini kama ukitengeneza orodha ya “viongozi”wakubwa kabisa wa watu weusi wa mwaka 1960, basi utakuwa umewataja wale waliotushambulia sisi watu weusi wa “Shambani” tuliokuwa tunaonekana tumerukwa na akili kwa kumuongelea namna ile “Bwana mwema.”

“Waislamu hawa hawawakilishi umma wa watu weusi-” hilo ndilo lilikuwa jambo la kwanza walilomhakikishia “bwana mwema,” kwamba hakuwa na sababu ya kuwahofia wa “Shambani” hawa walioishi maghettoni. “Kikundi cha wenye chuki wasiojali”. . . “Kuchafua taswira ya mtu mweusi wakati ambao suala la ubaguzi wa rangi linaanza kutokomea.”
Walikuwa wanagongana wao kwa wao ili wanukuliwe. “Ubaguzi wa rangi uliogeuzwa”. . . “Waislamu feki”. . . “Wakufuru na wapinga ukristo-”
Simu kwenye Hekalu letu dogo la Namba Saba iliita muda wote. Ilikuwa sikioni mwangu saa tano kwa siku. Nilikuwa nikisikiliza na kuandika kwenye kitabu changu cha kumbukumbu yale waliyoniuliza watu wa magazeti, redio na televisheni walipokuwa wakinipigia simu mfululizo, wote wakitaka kusikia majibu ya Waislamu kutokana na mashambulizi ya “viongozi” wa watu weusi, na wakati mwingine nikiwa naongea na bwana Muhammad, nikimsomea kutoka kwenye kitabu hicho, nikiomba muongozo wake.
Sikuweza kuelewa bwana Muhammad aliwezaje kuwa mtulivu na mwenye subira nilipomsomea mambo niliyoandika. Mimi mwenyewe nilikuwa mtulivu kwa taabu sana. Kwa namna fulani simu yangu ya nyumbani nayo ikawa imejulikana. Mara tu mke wangu Betty alipoweka simu chini, iliita tena. Ilionekana kuwa kila ninakokwenda simu ziliita.

Simu nyingi zilielekezwa kwangu, New York ni makao makuu ya mashirika mengi makubwa ya habari na mimi nilikuwa Imam wa Muhammad ndani ya jiji la New York. Simu zilitoka kila kona, kutoka San Francisco hadi Maine . . . hata zingine kutoka London, Stockholm na Paris. Ilinibidi kuwa naenda kumuona ndugu wa kwenye mgahawa wetu au kurudi nyumbani kwa Betty ili kupata utulivu; sikuamini nao walipokuwa wananikabidhi simu. Kitu kimoja cha kufurahisha, katika pilikapilika zile zote ni kuwa niligundua kitu kimoja: wazungu wa Ulaya hawakutilia mkazo suala la “chuki.” Ni wazungu wa Marekani tu ndiyo walihangaika nalo na kutilia mkazo kuhusu “Kuchukiwa.” Niliona wazi jinsi dhamira juu ya uhalifu wa kumchukia mtu mweusi ilivyowasuta.

“Bwana Malcom X, kwa nini unafundisha chuki na ukuu wa mtu mweusi?” Kila niliposikia hilo niliona bendera ya hatari na kitu fulani kilitokea ndani yangu. Waislamu tulipoongea juu ya “shetani wa kizungu” ilikuwa kwa namna fulani kijuu juu tu, Mtu ambaye hatukukutana naye kwa ukawaida, lakini tazama hapa, shetani katika mwili, akiongea kwenye simu kwa hila zote. Sauti zilizokuwa zikinihoji kwangu zikawa kama shetani halisi.

Nami nilijaribu kurudisha moto vilevile. ‘Mtu mweupe akiwa amejaa hatia kwa kuamini ukuu wa mtu mweupe, hawezi kuficha hatia hiyo kwa kumshutumu Mtukufu Elijah Muhammad kuwa anafundisha chuki na ukuu wa mtu mweusi! Anachojaribu kufanya bwana Muhammad ni kuinua mtazamo wa mtu mweusi na hali yake ya kijamii na kiuchumi katika nchi hii.

‘Mzungu mwenye hatia na ndumakuwili ameshindwa kuamua anataka nini. Mababu zetu wa kitumwa wangeuawa iwapo wangetoa hoja ya kuchangamana na wazungu. Lakini sasa bwana Muhammad anapoongelea ‘utengano’ mzungu anatuita ‘walimu wa chuki’ na ‘Mafashisti’!
“Mzungu hataki watu weusi. Hataki watu weusi wanaomnyonya! Hamtaki mtu mweusi nchini mwake ambaye hali ya maisha yake inamchongea mzungu duniani kuwa yeye ni mtu wa aina gani! Sasa kwa nini mnamshambulia bwana Muhammad?”
Sauti yangu ilikuwa kali.

‘Kwa mzungu kumuuliza mtu mweusi iwapo anamchukia ni sawa na mbakaji kumuuliza aliyebakwa, au mbwa mwitu kumuuliza kondoo, ‘Unanichukia?’ Mtu mweupe hana haki ya kumshutumu yeyote kuwa ana chuki!
“Iwapo wazazi wangu waling’atwa na nyoka, nami nikang’atwa na nyoka, kwa nini ninapowaonya watoto wangu kuepuka nyoka inaonekana kama nyoka huyo ananishutumu kuwa nahubiri chuki?”
Shetani hao waliniuliza, “Bwana Malcom, kwa nini Fruits of Islam wanafundishwa judo na karate?” Inaonekana taswira ya mtu mweusi akijifunza kitu chochote kinachohusu kujilinda inamuogopesha sana mzungu. Niliwageuzia swali hilo, “Kwa nini ghafla judo na karate vimeanza kuonekana ni vitu vya kutisha mara tu watu weusi walipoanza kujifunza? Marekani kote, vijana wa skauti, YMCA, hata YWCA, CYP, PAL—wote wanafundisha judo, hakuna tatizo lolote mpaka pale mtu mweusi anapoanza kuifundisha. Hata wasichana wadogo wanafundishwa kujilinda-’
“Kikundi chenu kina watu wangapi bwana Malcom X? Mchungaji na Askofu T. “Bawa la Kuku” anasema unawafuasi wachache tu-”
“Anayekuambia kuna Waislamu kadhaa hajui ukweli, na anayejua hawezi kukuambia-”
Maaskofu “Mbawa za Kuku” walinukuliwa sana wakisema kuwa tulikuwa “Wapinga Ukristo.” Nilijibu hilo bila kumung’unya maneno:

“Ukristo ni dini ya mzungu. Biblia mikononi mwa mzungu na jinsi anavyoielezea, imekuwa ni silaha kuu ya kiitikadi ambayo ameitumia kufanya mamilioni ya watu wasio weupe kuwa watumwa wake. Kila nchi ambayo mzungu ameiteka kwa bunduki alifungua njia na alijisafisha kwanza kwa kubeba biblia na kuitafsiri kwamba wenyeji wa nchi hiyo ni washenzi na ‘wapagani’; kisha alituma bunduki, na baada ya hapo wamisionari wake nyuma ya bunduki ili kufagia-”
Kwa sauti za hasira, waandishi wa habari wa kizungu walituita “Demagogues” (Wanasiasa wanaocheza na hisia za watu). Nilikuwa najaribu kujiandaa vyema baada ya kuwa nimeulizwa swali fulani mara mbili au tatu.
“Hebu turudi kwenye kigiriki, pengine utajifunza maana hasa ya neno ‘Demagogue.’ Maana halisi ya ‘Demagogue’ ni ‘Mwalimu wa watu.’ Na acha tuchunguze baadhi ya demagogues. Mkuu kuliko wote kati ya Wagiriki, Socrates, aliuawa kwa kuitwa Demagogue. Yesu Kristo alikufa msalabani kwa sababu Mafarisayo wa wakati wake walishikilia kuongozwa na sheria na si roho. Mafarisayo wa leo wanataka kumshukia bwana Muhammad kwa kumwita Demagogue, mpumbavu na “mnazi.” Vipi kuhusu Gandhi? Mtu ambaye Churchill alimwita ‘Fakir mdogo aliye uchi’ anayekataa kula kwenye gereza la Waingereza? Lakini wakati huo huo watu nusu bilioni, Bara-Hindi lote lilikuwa nyuma ya Gandhi na waliweza kuunyonga mkia wa simba wa Uingereza! Vipi kuhusu Galileo, amesimama mbele ya washtaki wake akiwaambia kuwa dunia inazunguka! Vipi kuhusu Martin

Luther, akipigilia andiko lake kwenye milango, maandiko yaliyo kinyume na kanisa Katoliki lenye nguvu ambalo lilimuita ‘mkufuru’? Leo hii sisi wafuasi wa Mtukufu Elijah Muhammad, tupo kwenye maeneo ya maghetto kama tu ambavyo waumini wa Ukristo kuna wakati walikuwa kama mchwa kwenye mapango na makaburi yaliyojengwa chini, wakiandaa kaburi la Miliki yenye nguvu ya Roma.

Ninakumbuka mazungumzo makali ya simu na waandishi wale kama vile imetokea jana tu. Waandishi walikuwa na hasira, nami pia nilikuwa na hasira. Nilipoanza kuzungumzia historia walijaribu kunirudisha wakati wa sasa. Waliacha mahojiano, waliacha kazi yao ili kutetea ushetani wao. Walifukua habari za Lincoln na kuachilia kwake watumwa. Nami niliwaambia mambo ambayo Lincoln alisema kwenye hotuba zake dhidi ya watu weusi. Walileta maamuzi ya mwaka 1954 ya Mahakama Kuu juu ya kukomesha kutenga watu shuleni kwa sababu ya rangi.

“Hilo lilikuwa moja ya jambo la kisanii zaidi kuwahi kufanyika katika Marekani,” niliwaambia. “Mnataka kuniambia kuwa majaji tisa wa Mahakama Kuu ambao ni manguli wa lugha ya sheria hawakuweza kufanya uamuzi wao uwe sheria? Ule ulikuwa ni uhuni na kiini macho kuwaaminisha watu wetu kuwa utengano ulikuwa unaondolewa na wakati huo huo kuwaambia wazungu fuateni njia hii kuendeleza utengano.”
Waandishi walijitahidi kadri wawezavyo kumleta mzungu “mwema” ambaye nisingeweza kuwabishia. Sitasahau jinsi
mmoja wao alivyokaukwa na sauti. Aliniuliza iwapo ninahisi kuna wazungu ambao walifanya jambo zuri kwa watu weusi wa Marekani. Nilimwambia ndiyo, naweza kutaja wawili. Hitler na Stalin. Mtu mweusi hangeweza kupata kazi ya kiwandani mpaka pale Hitler alipoiweka Marekani katika hali tete. Na Stalin aliendeleza hali tete hiyo-’
Lakini sijali juu ya hoja nilizotoa wakati wa mahojiano, hazikuwahi chapishwa kama nilivyozitoa. Nilijifunza kwa uchungu jinsi ambavyo magazeti, yanapotaka, yanaweza kupindisha maneno. Kama ningesema “Mary had a little lamb(Maria kapata mwanakondoo),” pengine ambacho kingeandikwa kingekuwa, “Malcom X Lampoons Mary(Malcom X amdhihaki Maria).”
Lakini pamoja na hayo yote, hasira zangu hazikuwa kali kuelekea magazeti ya wazungu kama zilivyokuwa kwa wale “viongozi” wa watu weusi walioendelea kutushambulia. Bwana Muhammad alisema kuwa tujaribu tuwezavyo kutowarudishia mashambulizi hadharani “viongozi” hao sababu moja ya hila ya mzungu ni kufanya jamii ya watu weusi igawanyike na wapigane wao kwa wao. Aliendelea kusema kuwa kwa muda mrefu jambo hili limewafanya watu weusi washindwe kufikia umoja ambao ndiyo lilikuwa hitaji kuu la watu weusi wa Marekani.
Lakini badala ya kupoa vibaraka weusi walizidi kumshambulia bwana Muhammad na Taifa la Kislamu hadi ikaanza kuonekana kama tulikuwa tunaogopa kuwajibu watu weusi hawa “wa maana” Hapo ndipo uvumilivu wa bwana
Muhammad ulipokoma. Kwa ruhusa yake nikaanza kurudisha mashambulizi.
Uncle Tom(Kibaraka mweusi) wa leo havai kitambaa kichwani. Uncle Tom huyu wa karne ya ishirini mara nyingi huvaa kofia ndefu. Na kawaida huvalia nadhifu na ni msomi mzuri. Anawakilisha utamaduni mzuri na kustaarabika. Wakati mwingine Uncle Thomas huyu anaongea kwa lafudhi ya Yale na Harvard. Wakati mwingine anajulikana kama Profesa, Jaji, Mchungaji, Doctor na hata Mchungaji-Askofu- Doctor. Uncle Thomas huyu wa karne ya ishirini ni mnegro mwenye taaluma . . . kwa kusema hivyo namaanisha taaluma yake ni kuwa mnegro wa mzungu. “
Katika marekani haijawahi tokea kwa hawa wanaojiita “Viongozi” kushambuliwa namna ile hadharani. Waliuchukulia ukweli kwa hasira kuliko hata shetani wa kizungu. Sasa wakajipanga na kuanza kutushambulia wakiwa wamoja. Badala ya kila “Kiongozi” kujiongelea sasa wakajiunga na kumshukia bwana Muhammad.
“Watu wenye miili myeusi lakini wenye vichwani ni wazungu!” Niliwaambia ukweli wao. Kila moja ya kikundi cha viongozi wale weusi kilikuwa kimeundwa kwa mtindo unaofanana. “Viongozi” weusi walikuwa mstari wa mbele ili kuonekana na watu weusi ambao walidai wanapambana na mzungu kwa niaba yao. Lakini nyuma ya pazia kulikuwa na bosi wa kizungu-akiwa na cheo cha rais, mwenyekiti wa bodi nk, na huyo ndiye aliyeendesha mambo.

Ilikuwa ni mada ya moto, moto hasa, kwenye magazeti na majarida yote; ya wazungu na watu weusi. Life, Look, Newsweek na Times, yote yaliandika kutuhusu. Magazeti mengine hayakuandika habari moja tu, bali yaliandika mfululizo wa makala mbili, tatu hadi tano za “kufichua” Taifa la Kiislamu. Jarida la Reader’s Digest ambalo huuza nakala milioni ishirini na nne duniani kote, katika lugha zaidi ya kumi na tatu; liliandika kichwa “Bwana Muhammad aongea,” Makala hiyo iliandikwa na muandishi ninayemsimulia simulizi hii; jambo hilo lilifanya majarida mengine makubwa yaliyotoka kila mwezi nayo yatuandike.

***
 
Hii sura ina nondo balaa...shukrani sana mdau...lete na.15 tafadhali
 
Sura ya kumi na nne inaendelea. kondoowasufi LUKAMA Siogye

Haukupita muda mrefu, vituo vya luninga na redio vikaanza kuniomba kwenda kutetea Taifa la Kiislamu kwenye mijadala na malumbano. Nilikuwa naenda kupambanishwa na wasomi waliochaguliwa, wote, wazungu na manegro wa “Nyumbani” na “uani” wenye PhD, wale waliokuwa wakitushambulia. Kila siku zilivyopita ndivyo nilivyozidi kukasirishwa na jinsi mafundisho ya bwana Muhammad yaliyotafsiriwa vibaya na kupotoshwa. Kwa kweli sikufikiria kabisa kwamba sijawahi ingia kwenye kituo cha redio au television; achilia mbali kushika kipaza auti na kuongea na mamilioni ya watu. Uzoefu pekee niliokuwa nao ni kupitia mijadala ya gerezani na kuongea na Waislamu.
Nilijifunza kwenye maisha ya upambanaji niliyoishi kuwa kila kitu kina mbinu zake. Na kwenye mijadala ya gerezani nilijifunza mbinu za kuwakwaza wapinzani wangu ili kuwakamata mahali wasipotarajia kukamatwa. Nilijua lazima kutakuwa na mbinu na ujanja ujanja kwenye mijadala ya redioni na kwenye televisheni lakini sikujua chochote juu ya kubishana nikiwa hewani.

Lakini nilifahamu kuwa iwapo nikichunguza kwa makini jinsi wengine wanavyofanya basi naweza kujifunza haraka jinsi ya kumtetea bwana Muhammad na mafundisho yake.

Nilipokuwa nikiingia kwenye studio zile niliona mashetani na vibaraka weusi, wale wenye PhD; wakijidai marafiki na wamoja. Wakicheka na kuitana kwa majina ya kwanza na mambo kama hayo. Ulikuwa unafiki mkubwa uliofanya tumbo linichafuke. Hata walijidai kunitendea kama rafiki yao wakati sote tulijua kuwa wamenikaribisha pale ili kupambana nami. Walinikaribisha kahawa nami niliwajibu tu “Ahsante nashukuru” na kuomba wanionyeshe ninapopaswa kuketi. Wakati mwingine kinasa sauti kiliwekwa mezani mbele yako, na wakati mwingine kinasa sauti kidogo kilifungwa shingoni mwako. Toka mwanzo nilivipenda sana vinasa sauti vya shingoni, haikunilazimu kuwazia umbali kutoka nilipo na kinasa sauti.

Muendeshaji wa kipindi alianza kwa kunitambulisha. Alianza na-leo tuna mtu mwenye hasira na mkali, chifu Malcom X kutoka kwa Waislamu wa New York. . . . ’ Nilikuwa nimeandaa utambulisho wangu mwenyewe nilipokuwa nyumbani au nikiwa kwenye gari, nilimkatiza muendesha kipindi na kujitambulisha mwenyewe.

‘Ninamuwakilisha bwana Elijah Muhammad, kiongozi wa kiroho wa kundi la Waislamu linalokua kwa kasi zaidi katika nchi za Magharibi. Sote tunaomfuata tunafahamu kuwa amefundishwa na kutumwa kwetu na Mungu mwenyewe. Tunaamini kuwa mateso wanayopitia watu weusi milioni ishirini ndani ya Marekani ni utimizo wa unabii. Pia tunaamini uwepo wa Mtukufu Elijah Muhammad, mafundisho yake kwa watu weusi, na onyo lake la wazi kwenda kwa Marekani kutokana na jinsi inavyomtendea mtu mweusi huyo-yote ni utimizo wa unabii. Nina bahati ya kuwa Imam wa Hekalu letu Namba Saba lililopo hapa New York, Hekalu ambalo ni sehemu ya Taifa la Kiislamu chini ya uongozi wa kiroho wa Mtukufu Elijah Muhammad-’
Baada ya utambulisho niliwaangalia mashetani wale na kasuku wao weusi walivyokuwa wakinishangaa. Nilipokuwa natulia na kuvuta pumzi waliruka na kushindana wenyewe kwa wenyewe katika kunishambulia, kumshambulia bwana Muhammad na Taifa la Kiislamu. Kwa nini Waislamu hawaoni kuwa kuondoa utengano wa kijamii ndiyo jibu pekee la matatizo ya watu weusi wa Marekani? Nilijaribu kuvunja hoja yao hiyo vipandevipande.
“Hakuna mtu mweusi mwenye akili timamu anayehitaji jamii za rangi zote kuishi pamoja! Hakuna mzungu mwenye akili timamu anayetaka jamii za rangi zote kuishi pamoja! Hakuna mtu mweusi mwenye akili timamu anayeamini kuwa mzungu atakubali kuchangamana zaidi ya kuchangamana kwa geresha tu. Hilo halipo! Mtukufu Elijah Muhammad anafundisha kuwa suluhisho pekee kwa mtu mweusi wa Marekani ni kujitenga na mzungu!”
Yoyote ambaye amewahi kunisikia redioni au katika televisheni atafahamu kuwa mbinu yangu ni kutonyamaza mpaka nimalize kuongea kile nilichotaka kuongea. Wakati huo ndiyo nilikuwa naanza kutumia mbinu hiyo.
“Mtukufu Elijah Muhammad anatufundisha kuwa, sababu jamii ya magharibi inaangamia na kujaa ukosefu wa maadili, Mungu ataenda kuihukumu na kuiharibu. Na njia pekee kwa watu weusi waliomo katika jamii hii kuokoka ni kujitenga na jamii hiyo iliyopotoka na si kuchangamana nayo, kwenda kwenye nchi yetu wenyewe, mahali tunapoweza kujifanyia mabadiliko, kujiinua kimaadili na kuwa watu wa Mungu. Wanadiplomasia nguli wa magharibi wameshindwa kutatua tatizo la ubaguzi wa rangi. Wanasheria nguli wameshindwa. Viongozi wake wa kijamii wameshindwa, wataalamu wa masuala ya kijamii wameshindwa. Viongozi wake wanaoheshimika nao wameshindwa. Kwa kuwa wote hawa wameshindwa kutatua tatizo hili, ni wakati sasa tukae chini na kutafakari! Nina hakika wote tutakubaliana kuwa ni Mungu pekee ndiye anaweza kutatua utata huu mkubwa.”

Kila mara nilipotaja “Utengano” baadhi yao walipiga kelele kuwa Waislamu tulikuwa tunaunga mkono kitu kilekile ambacho wabaguzi wa rangi na Demagogues wa kizungu waliunga mkono. Nilifafanua tofauti. ‘Hapana! Tunakataa ubaguzi(Segregation) wa watu kulingana na rangi zao kwa nguvu kuliko hata nyinyi! Tunachotaka sisi ni utengano(Separation), ambao ni kitu tofauti. Mtukufu Elijah Muhammad anatufundisha kuwa kwenye ubaguzi maisha na uhuru wako vinakuwa chini ya mtu mwingine. Kubagua inamaanisha kutawala. Ubaguzi huwekwa na wenye nguvu dhidi ya wanyonge. Lakini utengano hufanywa kwa hiari na watu wenye haki sawa kwa ajili ya faida ya wote. Mtukufu Elijah Muhammad anatufundisha kuwa, kadri ambavyo watu wetu katika Marekani wanavyomtegemea mzungu, siku zote tunamuomba kazi, chakula, nyumba na mavazi, basi siku zote atatawala maisha yetu na kuwa na nguvu ya kutubagua. Mtu mweusi katika Marekani ametendewa kama mtoto. Mtoto anakaa ndani ya mama yake mpaka wakati wa kuzaliwa. Wakati wa kuzaliwa unapofika lazima mtoto ajitenge na mama yake la sivyo atamuua mama yake na yeye mwenyewe. Mama hawezi kuendelea kuwa na mtoto ndani yake baada ya muda wa kuzaliwa kufika. Mtoto analilia na anahitaji ulimwengu wake!’
Mtu yeyote ambaye amewahi kunisikiliza atakubali kuwa nilimuamini na kumuwakilisha bwana Muhammad kwa asilimia mia moja. Kamwe sikujaribu kujikweza na kujipa sifa. Sikuwahi kushiriki mijadala ile bila ya mmoja waa kunishutumu kuwa “nawachochea watu weusi kufanya​
vurugu.” Sikuhitaji hata kujisomea ili kujiandaa kujibu hilo. “Muujiza mkubwa ambayo Ukristo umefanya ndani ya
Marekani ni kwa mtu mweusi chini ya mzungu kutokuwa mtu wa vurugu. Ni muujiza kwa watu milioni ishirini na mbili kutoinuka juu ya watesi wao wakati wana sababu zote za kufanya hivyo, hata desturi za kidemokrasia zingewaunga mkono! Ni muujiza kuwa taifa la watu weusi kuendelea kuamini falsafa ya kugeuza shavu la kushoto na mbingu baada ya kifo kwa moyo mmoja! Ni muujiza kwa watu weusi wa Marekani kubaki kuwa watu wa amani kwa karne kadhaa wakiishi kuzimu-hapa hapa kwenye mbingu ya mzungu! Muujiza ni kwa vibaraka wa mzungu, “viongozi” wa watu weusi, wachungaji, watu weusi waliosoma na kujaa shahada, na wale walioruhusiwa kuwanyonya ndugu zao weusi kufanikiwa kuunyamazisha umma wa watu weusi hadi sasa.”

Nakuhakikishia jambo moja, kila mara nilipokuwa kwenye studio zile pamoja na vibaraka weusi wale walioshikwa akili, “wahusudu uchangamano” pamoja na shetani wale wakijaribu kunichanachana-lakini kadri ambavyo “taa nyekundu ilivyoendelea kuwaka” kuonyesha kuwa tupo hewani, nilijaribu kila niwezavyo kumuwakilisha bwana Muhammad na Taifa la Kiislamu.

Kitabu cha Dr. C. Eric Lincoln kilichapishwa wakati ambao sintofahamu juu yetu Waislamu ilipokuwa inakua kila uchao, na wakati huo huo ndiyo tulikuwa tunaanza kufanya mihadhara yetu mikubwa.
Kama tu ambavyo kichwa cha kipindi cha televisheni, “Chuki iliyozalishwa na chuki” kilivyofanywa isemwe “tunahubiri chuki,” Ndivyo ilivyokuwa kitabu cha Dr Lincoln kilichokuwa na kichwa The Black Muslims of America(Waislamu weusi wa Marekani.) Vyombo vya habari vilichukua neno “Waislamu Weusi” na kulitumia kuelezea kitabu chote.

Vyombo hivyo vilinukuu tu sehemu za kitabu zilizotushutumu na kwa ujumla walisifia uandishi wa Dr. Lincoln.
Akili ya watu wote ilikazia fikra kwenye “Waislamu Weusi” Jina hilo “Waislamu Weusi” liliwakera sana Waislamu, kutoka Muhammad mwenyewe hadi wengine wote katika Taifa la Kiislamu. Nilijaribu kwa si chini ya miaka miwili nikijaribu kuua jina hilo. Kila nafasi ya kuongea na waandishi wa habari niliyopata nilikazia, “Hapana! Sisi ni watu weusi wa Marekani. Dini yetu ni Uislamu. Jina letu rasmi ni Waislamu! Lakini jina lile la “Waislamu Weusi” halikufa.

Mikutano yetu ya hadhara ilikuwa na mafanikio makubwa sana. Wakati zamani Hekalu Namba Moja la Detroit lililosuasua lilikuwa na msafara wa gari kumi kwenda Chicago kumsikiliza bwana Muhammad, sasa kutoka Mahekalu ya Pwani ya Mashariki-mahekalu makongwe na mapya kulikuwa na msafara wa mabasi makubwa ya kukodi 150, 200 na hadi 300 kwenda kumsikiliza bwana Muhammad kokote alikokuwa anaongea. Kwenye kila basi kulikuwa na wasimamizi wawili kutoka Fruit of Islam. Mabango makubwa ya futi tatu kwa tisa yalining’inia ubavuni mwa mabasi ili yasomwe na watu kote mabasi yatakakopita.

Mamia mengine ya Waislamu na watu weusi waliopendezwa waliendesha magari yao wenyewe. Bwana Muhammad alitoka Chicago na ndege yake binafsi, msafara wake kutoka uwanja wa ndege ulisindikizwa na ving’ora vya polisi. Kuna wakati vyombo vya dola viliwahi kudhihaki taifa letu kwa kutuita “vichaa weusi”; lakini sasa walihangaika kutulinda dhidi ya “vichaa wa kizungu” ili wasije kuleta “matata” au kusababisha “Ajali.”
Mikutano ya watu weusi kama ile haijawahi kutokea katika Marekani. Ili kumsikiliza bwana Muhammad, watu weusi karibu elfu kumi walijaza kumbi kubwa tulizokodi, kumbi kama St. Nicholas Arena katika jiji la New York. Coliseum huko Chicago na Uline Arena huko Washington D. C.

Mzungu hakuruhusiwa kuhudhuria-ilikuwa mara ya kwanza kwa mtu mweusi wa Marekani kufanya hivyo. Jambo hilo lilituletea mashambulizi mapya kutoka kwa mzungu na vibaraka wake weusi, “Wabaguzi weusi. . . Wabaguzi wa rangi!” Wakitushutumu kwa ubaguzi! Marekani kote mzungu kumzuia mtu mweusi ilikuwa ndilo jambo lililozoeleka.
Mamia ya watu walifika kwa kuchelewa na hatukuwa na nafasi ya pakuwaweka. Mara zote ilitubidi kuweka vipaza sauti nje. Shauku na shangwe vilionekana waziwazi kwenye umati wa watu weusi. Mistari mirefu, mitatu hadi minne ya kuingia ukumbini ilisimamiwa vizuri na wanaume wa Fruit of Islam waliokuwa wakiwasiliana kwa redio call. Kwenye vyumba vya mapokezi wanaume wengine kutoka Fruit of Islam na dada watu wazima wa Kiislamu waliovalia magauni meupe na ushungi waliwakagua wanaume, wanawake na watoto walioingia. Pombe na tumbaku havikuruhusiwa, pia waliangalia vitu ambavyo vingeweza kutumika kumdhuru bwana Muhammad. Siku zote bwana Muhammad aliishi kwa hofu kuwa kuna mtu atamdhuru, na alisisitiza kila mtu akaguliwe ili kuzuia hilo. Leo naelewa vizuri kwa nini.

Mamia ya wanaume wa Fruit of Islam walifika mapema asubuhi kutoka Mahekalu ya majiji ya karibu. Wengine walikuwa wakaribishaji walioelekeza watu sehemu za kukaa. Ghorofani na sehemu ya nyuma ya ukumbi walikaa watu weusi wengine ambao si Waislamu. Mbele yao walikaa ndugu na dada Wakiislamu wakiwa wamevalia magauni meupe na wanaume walivalia suti nyeusi na mashati meupe. Sehemu maalumu karibu na jukwaani walikaa “Wageni maalumu”, wengi wao walikuwa wamealikwa rasmi. Kati yao walikuwemo vibaraka na kasuku weusi waliotushambulia, watu weusi wasomi na wanataaluma, watu ambao bwana Muhammad aliwasikitikia sana, maana hawa walikuwa ndiyo wasomi waliotakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaongoza ndugu zao kutoka kwenye mateso na dhiki. Hatukutaka wakose kusikia hata neno moja la ukweli kutoka kwa bwana Muhammad mwenyewe. Mistari miwili au mitatu ya mbele ilijazwa na waandishi wa habari na wapiga picha weusi, kutoka vyombo vya habari vya watu weusi, au wakiwa wameajiriwa na vyombo vya habari vya wazungu.

Waandishi wa habari weusi wanatakiwa kumfanyia sherehe bwana Muhammad. Kuandika habari juu ya Taifa la Kiislamu ilikuwa njia iliyowainua waandishi wengi weusi wanaojulikana leo.

Mbele jukwaani, maimam tuliingia kupitia mlango wa nyuma ya jukwaa na kukaa kwenye mistari mitano hadi sita,
nyuma ya kiti kikubwa cha bwana Muhammad. Baadhi ya maimam walisafiri mamia ya maili ili kufika kwenye shughuli ile. Tulikuwa tukigeukiana na kupeana mikono kwa tabasamu, tukisema, “As-Salaam-Alaikum” na “Wa- Alaikum Salaam” tukiwa tumejawa na furaha kwa kuonana.

Kila wakati kulikuwa na maimam wapya kutoka mahekalu mapya madogo. Kaka zangu, Wilfred alikuwa Imam huko Detroit na Philbert alikuwa Imam huko Lansing. Ndugu Jeremiah X alikuwa kiongozi wa Hekalu la Atlanta, John X alikuwa Imam wa Hekalu la Los Angeles. Mtoto wa Mtume, Wallace Muhammad, alikuwa Imam wa Hekalu la Philadelphia. Imam Woodrow X alikuwa kwenye Hekalu la Atlantic City. Baadhi ya Maimam wetu walikuwa na historia za kushangaza sana. Imam wa Hekalu la Washington D.C., Imam Lucius X huko nyuma alikuwa mchungaji wa Wasabato na Mmasoni wa digrii 32. Imam George X wa Hekalu la Camden, New Jersey alikuwa mwanapatholojia. Imam David X alikuwa mchungaji wa kanisa la Kikristo huko Richmond, Virginia. Kanisa hilo liligawanyika na walio wengi wakaligeuza kanisa hilo kuwa Hekalu letu. Louis X, Imam kijana hodari wa Hekalu la Boston, alikuwa ni mwanamuziki chipukizi anayekuja kasi, akijulikana kwa jina la “The Charmer,” aliandika wimbo wetu wa kwanza maarufu ulioitwa, “White man’s heaven is Black man’s hell,”(Mbingu ya mzungu ni kuzimu ya mtu mweusi). Pia aliandika mchezo wetu wa kwanza wa kuigiza ulioitwa Orgena, maneno “A Negro” yakiwa yameandikwa kwa kinyume” Ulihusu majaji weusi wakimhukumu mzungu kwa makosa aliyowafanyia watu wasio wazungu duniani; alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo, aliburuzwa kwenda kuhukumiwa huku akipiga kelele juu ya mambo mazuri aliyowafanyia watu weusi.

Maimam vijana kuliko hata Louis X walikuwa ni Imam Thomas J. X wa Hekalu la Hartford na mwingine ni Imam Robert J. X wa Hekalu la Buffalo.

Mengi ya mahekalu hayo nilikuwa nimeyaanzisha au kuratibu uanzishaji wake, kuwasalimia ndugu hawa kuliniletea kumbukumbu za “uvuvi” wa mtaani na wa nyumba kwa nyumba kotekote walikokuwepo watu weusi. Nilikumbuka mikutano mingi tuliyofanya kwenye sebule za watu ambayo wahudhuria wengi zaidi hawakuzidi saba; ukuaji polepole hadi kufikia kukodi viti na fremu za maduka ambazo Waislamu walizisafisha hadi zikang’aa kabisa.
Sasa tulikaa pamoja mbele ya jukwaa ndani ya ukumbi mkubwa, mbele yetu kukiwa na umati mkubwa, ilikuwa ni muijiza, nilikuwa nashuhudia nguvu isiyoelezeka ya Allah. Kwa mara ya kwanza nilielewa kitu fulani alichokuwa amenieleza bwana Muhammad: alidai kuwa alipokuwa anapitia majaribu ya kuwakimbia wanafiki weusi, akienda mji na mji, mara nyingi Allah alikuwa akimtumia maono ya umati mkubwa ambao siku moja utasikiliza mafundisho yake; bwana Muhammad alisema kuwa maono hayo yalimsaidia kuvumilia alipokuwa amefungwa kwenye gereza la mzungu.

Mara minong’ono ya umati ule mkubwa ilikoma. . . .

Kwenye kinasa sauti alikuwepo John Ali, katibu wa taifa wa Taifa la Kiislamu, au Imam wa Hekalu la Boston, Louis X. Waliuchangamsha umati ule wa watu weusi. Wakiongea kuhusu jinsi dunia mpya inavyowafungukia watu weusi kupitia Taifa la Kiislamu. Dada Tynetta Dynear aliongeleaa mchango muhimu wa wanawake wa Kiislamu, nafasi ya wanawake katika jitihada za Taifa la Kiislamu kuinua hali za kimwili, kimaadili, kijamii na kisiasa zinazowakabili watu weusi wa Marekani.

Kisha nilifuata mimi, kazi yangu hasa ilikuwa kuuandaa umati kwa ajili ya kumsikiliza bwana Muhammad ambaye alikuwa amefunga safari kutoka Chicago kuja kutufundisha.
Niliinua mkono wangu, “As-Salaikum-Salaam-”
“Wa-Alaikum-Salaam!”
Umati wa Waislamu ulijibu kwa kuunguruma.
Kulikuwa na utaratibu fulani ambao niliufuata kwenye shughuli kama hizi:
“Ndugu na dada zangu weusi wa dini zote na wale wasio na dini, sote tuna kitu kimoja kikubwa kinachotuunganisha . .
. sote ni watu weusi!
‘Sitaenda kuchukua siku nzima kuwaambia mazuri ya Mtukufu Elijah Muhammad. Nitakwenda tu kuwaambia jambo alilofanya ambalo ni kubwa kupita yote! Yeye ndiye kiongozi pekee na wa kwanza katika viongozi weusi kumtambua na kutujulisha adui yetu ni nani!

‘Elijah Muhammad ndiye kiongozi wa kwanza mweusi mwenye ujasiri wa kutuambia hadharani jambo ambalo ukienda nyumbani na kutafakari, utaona kuwa watu weusi tumekuwa tukiishi nalo, tumekuwa tukiliona na kuteseka nalo maisha yetu yote!

“Adui yetu ni mzungu! Na kwa nini kwa bwana Muhammad kutufundisha suala hilo ni jambo zuri sana? Kwa sababu kama mkimjua adui yenu, hawezi kuwafanya msiwe na umoja na kufanya mpigane ndugu kwa ndugu! Kwa sababu ukimtambua adui yako hataweza tena kutumia hila, ahadi, uongo, unafiki na matendo yake maovu ili kuendelea kukufanya kuwa kiziwi, mjinga na kipofu! Unapomtambua adui yako, hawezi tena kukuchota akili. Hawezi tena kukuziba macho na utaona waziwazi kuwa unaishi kuzimu hapa hapa duniani wakati yeye anaishi kwenye mbingu ndani ya dunia hiyohiyo! Adui huyu anayekuambia kuwa wote mnatakiwa kumuabudu Mungu mmoja wa Kikristo ambaye ni mzungu- ambaye mnaambiwa anawajali watu wote kwa usawa! Shetani huyo ndiye adui yenu. Nitatoa ushahidi! Chukua gazeti lolote la kila siku. Soma shutuma za uongo ambazo wanatupiwa viongozi wetu wa dini. Ni ushahidi ulio wazi kuwa mzungu hataki mtu mweusi yeyote asiye kibaraka au kasuku atuwakilishe. Shetani na bwana-watumwa huyu wa kizungu hataki wala hatuamini kuweza kuturuhusu kutengana naye- lakini tunapokaa hapa pamoja naye anatukandamiza na kutuweka kwenye daraja la mwisho kabisa la kijamii. Mzungu anapenda sana kuwaweka watu weusi mbali naye! Mbali na macho yake. Siku zote mzungu amewapenda viongozi wa watu weusi ambao anaweza kuwauliza. “Watu wako wanaendeleaje huko?’ Lakini kwa sababu Mtukufu Elijah Muhammad hatetereki anapokabiliana na mzungu, mzungu anamchukia. Mnapomsikia mzungu akimchukia, nanyi pia, kwa kutoelewa unabii wa Biblia mnamshutumu bwana Muhammad kuwa ni mbaguzi wa rangi, mwalimu wa chuki, mchukia wazungu na anayefundisha ukuu wa watu weusi-”

Hapo umati ulianza kuonyesha kutotulia vitini. . . .

Bwana Muhammad alianza kuja mbele akitokea nyuma ya ukumbi, akipita katikati ya umati-kama ambavyo aliwahi ingia kwenye msikiti wetu mdogo pale zamani. Mtu tuliyemchukulia kama kondoo mnyenyekevu alitembea akiwa amezungukwa na walinzi wa Fruit of Islam aliowachagua. Alibeba Biblia yake Takatifu na Quran yake Tukufu. Kichwani alikuwa na baraghashia yake ndogo nyeusi iliyokuwa na bendera ya Kiislamu, jua, mwezi na nyota vilivyoshonwa kwa dhahabu. Waislamu walipiga kelele kwa shangwe na kumkaribisha wakisema. “Mwanakondoo!” “As-Salaikum- Salaam!” “Sifa kwa Allah!”

Watu wengi tulibubujikwa na machozi. Aliniokoa nilipokuwa mfungwa. Alinifundisha nyumbani kwake kama vile nilikuwa mwana wake. Nafikiri maishani mwangu sijawahi kujawa na hisia kama siku ile, labda inaweza kuzidiwa na yaliyonitokea hivi karibuni tu. Ghafla walinzi wa Fruit of Islam walisimama na Muhammad alipanda peke yake jukwaani. Maimam wake, nikiwemo mimi, tulimzunguka kumsalimu.

Baada ya salamu nilirudi kwenye kinasa sauti, sikutaka kuusubirisha umati ule mkubwa wa watu weusi waliokuja kumsikiliza.

‘Ndugu na dada zangu weusi, hakuna atakayejua sisi ni nani mpaka pale tutakapojijua sisi ni nani! Hatutaweza kwenda popote mpaka pale tutakapojua tuko wapi! Mtukufu Elijah Muhammad anatupatia utambulisho wa kweli na kutujuza tulipo-vitu ambavyo ni kwa mara ya kwanza vinajulikana na mtu mweusi wa Marekani.
“Unaweza kuwa karibu na mtu huyu lakini kutokana na matendo yake unaweza usiwazie kabisa juu ya nguvu na mamlaka aliyonayo-” (Amini nikwambiapo kuwa niliweza kuzihisi nguvu za bwana Muhammad)
‘Haonyeshi wala kutangaza nguvu zake lakini hakuna kiongozi wa watu weusi katika Marekani aliye na wafuasi ambao wako tayari kupoteza maisha yake iwapo akiwaambia wafanye hivyo! Na simaanisha kufa kwa amani huku ukiombaomba kwa mzungu-yaani kufa kinyonge.

‘Ndugu na dada zangu weusi, mmetoka majumbani mwenu kuja kusikiliza, sasa mtakwenda kumsikiliza mtu mweusi mwenye busara na jasiri zaidi katika Marekani! Mtu mweusi mwenye nguvu zaidi katika nyika za Marekani ya Kaskazini!’

Hapo bwana Muhammad alikuja kwenye kinasa sauti haraka. Aliutazama umati uliokuwa kimya kabisa, umejiandaa kumsikiliza. Kisha, ‘As-Salaikum-Salaam’
“WA-ALAIKUM-SALAAM!”

Waliitikia Waislamu kwa kuunguruma na kutulia. Walijua kuwa kwa saa mbili zijazo bwana Muhammad atatema ukweli wake mkali. Ukweli ni kuwa kila Muislamu alikuwa na wasiwasi kuwa atajiumiza kwa hotuba ndefu, hasa ukizingatia tatizo lake la pumu.

‘Sina shahada kama wengi wenu hapa. Lakini historia haijali chochote juu ya shahada yako.
‘Mzungu amewajaza hofu na kumuogopa tokea mkiwa watoto wachanga. Kwa hiyo juu yenu yupo adui mbaya kabisa kwa binadamu, hofu. Nafahamu baadhi yenu mnaogopa kusikiliza ukweli. Mmelelewa katika hofu na uongo. Lakini nitakwenda kuwahubiria ukweli hadi muwe huru kutoka kwenye hofu hiyo . . . .

‘Bwana-watumwa wenu aliwaleta hapa, na kila kitu juu ya maisha yenu ya nyuma kiliharibiwa. Leo hii hamfahamu lugha yenu ya asili. Mmetokea kabila gani? Hata leo mngesikia jina la kabila lenu msingelitambua. Hamjui chochote kuhusu utamaduni wenu wa asili. Hata majina yenu halisi ya ukoo hamyafahamu. Mmevaa majina ya mzungu! Bwana-watumwa mzungu anayewachukia!

‘Ninyi ni watu mnaodhani mnaijua vyema Biblia, na kuujua vyema Ukristo, hata mmekuwa wapumbavu kiasi cha kuamini hakuna kitu kingine kilicho sahihi zaidi ya Ukristo!

‘Katika dunia hii ninyi ni watu pekee msiojijua, msiyoijua jamii yenu, msiyoijua historia yenu na msiomjua adui yenu. Hamjui chochote zaidi ya kile ambacho bwana-watumwa wenu mzungu ameamua kuwaambia. Na amewaambia kile tu ambacho anajua kitamfaidisha yeye na jamii yake. Kwa faida yake amewafundisha kuwa nyinyi ni watu dhaifu na wanyonge, na eti mnaitwa ‘Negro.’

‘Nasema eti mnaitwa Negro kwa sababu nyinyi si Negro, hakuna jamii inayoitwa ya Wanegro. Nyinyi ni washiriki wa Taifa kutoka Asia, kutoka kabila la Shabazz. Negro ni jina bandia mlilolazimishwa kuitwa na bwana-watumwa wenu. Amekuwa akitupachika vitu tokea siku ile aliyoleta hapa meli ya kwanza iliyojaa watumwa-’

Muhammad alipopumzika kuongea, Waislamu walipiga kelele, “Mwanakondoo!”. . . “Sifa kwa Allah!”. . . “Fundisha Mtume!” Aliendelea.

‘Ujinga tulionao watu weusi wa Marekani, na jinsi tunavyojichukia ni mifano mizuri juu ya jinsi bwana- watumwa wa kizungu alivyopanga cha kutufundisha. Je, tunaonyesha akili ya kawaida kama watu wengine duniani kwa kuungana? Hapana, tunajinyong’onyeza, tumejikunyata na kuombaomba-tukijaribu kuchangamana na bwana- watumwa wetu. Sijawahi ona jambo la ajabu kama hili. Kila siku mzungu anawaambia kwa namna elfu, ‘hamuwezi kuishi hapa, hamuwezi kuingia hapa, hamuwezi kucheza hapa, hauwezi kula hapa, hauwezi kunywa hapa, hauwezi kusoma hapa.’ Bado tu hatuoni kuwa hana mpango wa kuchangamana nasi?

‘Umemlimia shamba lake! Umempikia chakula! Umemfulia nguo! Umemtunzia mke na watoto wake alipokuwa mbali. Ukweli ni kuwa hata umemnyonyesha kwa maziwa yako. Wewe ni Mkristo bora sana ukilinganisha na bwana-watumwa huyu aliyekufundisha Ukristo wake. ‘Kwa jasho na damu yako umemsaidia kujenga nchi tajiri sana kiasi kwamba anaweza kuwapa hata maadui zake mamilioni ya pesa! Na mara adui zake hao wanapopata pesa za kutosha na kuanza kumshambulia tena, wewe umekuwa askari wake shujaa, ukifa kwa ajili yake. Na siku zote umekuwa mtumishi wake muaminifu katika zile siku ziitwazo za amani-lakini Mkristo huyu wa Marekani bado hajaingiwa hata na utu kidogo kuweza kutambua na kukubali kuwa watu weusi waliomfanyia mambo mengi sana nao ni watu!”

“YAH, Man!”. . .”Um-huh!’ “Fundisha Mtume, fundisha!” .
. . “Yah” . . . “Waambie!”. . . “Sawa kabisa!”. . . “Usiwe na haraka mtume!” . . . “Ndiyo, ndiyo!”
Na wengine nao waliungana na Waislamu kupiga kelele. Kawaida sisi Waislamu si watu wa shangwe sana kama Wakristo weusi. Lakini sasa kelele zilikuwa juu.
“Basi acha sisi watu weusi tujitenge na bwana-watumwa mzungu huyu anayetudharau kupita kiasi. Mpo huko mkimuomba kitu kinachoitwa ‘Uchangamano’. Lakini, bwana-watumwa na mbakaji huyu wa kizungu anasema nini? Anasema hatachangamana kwa sababu damu nyeusi itachafua damu yake. Anasema hayo huku anatuangalia! Hebu geuka na muangalie mwenzako. Mzungu huyu ameishachangamana nasi kiasi kwamba si rahisi kumkuta mtu kati yetu mwenye rangi nyeusi ya asili kama ya mababu zetu.

“Mungu mkubwa, mtu huyu yupo sahihi!”. . . “Fundisha Mtume, fundisha-” “Msikilizeni, msikilizeni!”

“Ametuachia weusi kidogo tu,” aliendele Muhammad. “Na sasa anatuchukia sana, lakini hilo linamaanisha anajichukia mwenyewe kwa aliyotufanyia-anatuambia kuwa; kisheria mtu akiwa hata na tone moja ndani yake basi huyo ni mtu mweusi kamili! Basi kama hicho ndicho kitu pekee tulichobaki nacho, basi tunataka kuwa hilo tone moja.
Kufikia hapo udhaifu wa bwana Muhammad ulianza kuonekana lakini aliendelea kufundisha:

‘Basi na tujitenge na mzungu huyu, na tufanye haraka ili tujiokoe na uchangamano wowote unaoweza kuongezeka. Kwa nini mzungu huyu, mtu anayependa kujiita mwema na mkarimu, mtu ambaye anawapatia pesa hata adui zake-kwa nini hataki kugharamia jimbo letu lililojitenga, jimbo la watu weusi ambao wamemfanyia kazi kwa uaminifu wakiwa kama watumwa na watumishi wake? Eneo letu wenyewe ambalo tunaweza kujikomboa kutoka kwenye haya mabanda ya mzungu na kupanga mstari ili kupata mkate. Hata yale mambo anayodai tunamgharimu sana tutafanya wenyewe. Hatujawahi fanya mambo yetu wenyewe! Hatujawahi kufanya tunayoweza kwa sababu tumechotwa sana akili na bwana- watumwa wa kizungu kiasi kwamba tunatakiwa kumuendea na kumuomba mambo yote tunayotaka na kuhitaji-”

Baada ya kama dakika tisini za hotuba, kila Imam kati ya tuliokaa nyuma alikuwa anajitahidi kujizuia kumuendea na
kumwambia kuwa inatosha. Alikuwa akishika kwa nguvu jukwaa la mzungumzaji ili kujitegemeza.
‘Sisi watu weusi hatujui uwezo wetu. Hauwezi jua uwezo wa kitu chochote mpaka pale kinapokuwa huru, huru kujifanyia mambo yake chenyewe! Kama una paka ndani kwako ambaye unamtunza na kumdekeza-lazima kwanza umuachie huru porini kama unataka kujua iwapo anaweza kujilisha na kujitafutia makao.

Watu weusi wa hapa Marekani hatujawahi kuwa huru kuweza kufahamu uwezo wetu!Tunamaarifa na uzoefu wakuweza kufanya mambo yetu wenyewe. Tumelima maisha yetu yote, tunaweza lima chakula chetu wenyewe. Tunaweza kuanzisha viwanda kuzalisha mahitaji yetu wenyewe! Tunaweza anzisha biashara, kufanya biashara na kuwa huru kama watu wengine waliostaarabika-
‘Tunaweza ondokana na kuchotwa akili na kujichukia, na kuishi kama ndugu . . .
‘Tuwe na ardhi yetu wenyewe . . . kitu tunazoweza ita chetu
. . . na kuachana ha huyu bwana-watumwa.

Kawaida bwana Muhammad alikata hotuba zake ghafla baada ya kuwa hawezi kuendelea kuongea tena. Umati ulisimama na kupiga kelele za shangwe.

Nilisimama na kuunyamazisha umati, na wakati huo watu wa mapokezi kutoka Fruit of Islam wakaanza kupita vitini na maboksi kukusanya sadaka. Niliongea.
‘Mmefahamu kutokana na mlioyosikia kuwa Mtukufu Elijah Muhammad hafadhiliwi na pesa za mzungu. Hivyo mzungu hawezi ingilia shughuli za bwana Muhammad. Shughuli za bwana Muhammad ni za watu weusi pekee!
‘Sisi ni taasisi pekee ya watu weusi ambayo inaendeshwa na kutegemezwa na watu weusi tu. Hizi taasisi zinazojiita “za kuendeleza watu weusi” kwa nini zinadharau akili zenu kwa kudai kuwa zinawapigania, ili mpate haki sawa mnazopambania . . . zinadai zinapigana na mzungu aliyekataa kuwapa haki zenu, lakini kwa nini mzungu anaunga mkono taasisi hizo! Kama wewe ni mshiriki wa taasisi hizo utakuwa unazichangia dola mbili, tatu au tano kwa mwaka-lakini ni nani anazichangia taasisi hizo dola elfu mbili, tatu au tano kwa mwaka? Mzungu ndiye anayezilisha taasisi hizo! Hivyo ndiye anayeziendesha! Ndiye anayezishauri, hivyo ndiye anayezidhibiti! Tumieni akili, je hautamshauri, muendesha na kumdhibiti mtu unayemtegemeza, mfano mtoto wako?

“Mzungu angependa kumtegemeza bwana Elijah Muhammad. Sababu kama bwana Muhammad atategemea misaada yake, ataweza kumshauri. Ndugu na dada zangu weusi, ni kwa sababu ya pesa zenu, pesa zenu nyeusi kumtegemeza bwana Muhammad ndiyo anaweza kufanya mikutano hii toka mji mmoja mpaka mwingine, akituambia watu weusi ukweli! Ndiyo maana tunahitaji mchango wa watu weusi wote!”

Kila noti iliingia kwenye maboksi, hasa noti ya dola moja. Maboksi yalienda kumwagwa na kujazwa tena, watu wa Fruit of Islam walipita kwa watu wote.

Umati ulikuwa ni kama vile umepigwa ganzi. Michango ile iligharamia gharama za mkutano na chochote cha ziada kilichopatikana kilisaidia kuendelea kujenga Taifa la Kiislamu.

Kila baada ya mikutano kadhaa mikubwa, bwana Muhammad alitoa maelekezo turuhusu vyombo vya habari vya kizungu. Watu wa Fruit of Islam waliwakagua kama ambavyo kila mtu alikaguliwa; madaftari yao, kamera zao, mikoba ya kamera na kila kitu walichobeba. Baadaye bwana Muhammad alisema kuwa mzungu yeyote anayetaka kusikia ukweli anaweza kuhudhuria mikutano yetu ya hadhara, wazungu walitengewa sehemu yao iliyochukua watu wachache na waliruhusiwa wa kutosha hapo tu.

Wazungu wengi waliohudhuria walikuwa ni wasomi na wanafunzi. Niliangalia sura zao zilizobadilika kuwa nyekundu zikimshangaa bwana Muhammad. “Mzungu anafahamu kuwa matendo yake ni matendo ya shetani!” Pia nilitazama sura zote za wasomi weusi, wale waliotushambulia. Walikuwa na elimu na ujuzi ambao ungesaidia kuongoza umma wa ndugu zao weusi. Lakini ilionekana wasomi wote hawa walichowaza ni kujinyenyekeza na kubembeleza kuchangamana na mzungu anayedaiwa kuwa ni mliberali, mzungu ambaye alikuwa akiwaambia, “Subira . . . siku moja kila kitu kitakuwa sawa . . . muwe na subira na wavumilivu.” Watu weusi hawa wasomi hawawezi kutumia maarifa yao kwa manufaa ya watu weusi wenzao sababu hata kati yao wenyewe hawana umoja. Iwapo wangekuwa wameungana wenyewe na kwa jamii yao pia, wangekuwa msaada kwa watu weusi duniani kote! Niliona nyuso za wasomi hawa weusi zikionyesha kufadhaika ukweli ulipokuwa ukiwaingia.

Taifa la Kiislamu tulikuwa tunachunguzwa sana. Simu zetu zote zilikuwa zikisikilizwa. Hata leo hii nikisema kupitia simu ya nyumbani kwangu, “Nitalipua jengo la Empire State kwa mabomu,” nakuhakikishia ndani ya dakika tano nyumba yangu itazingirwa na askari. Wakati mwingine nilipokuwa naongea hadharani, nilikuwa najaribu kuwatambua watu ambao ni F.B.I au wanausalama wengine. Wote, polisi na F.B.I walitutembelea na kutuhoji mara nyingi. “Siwaogopi,” alisema bwana Muhammad. “Nina kila kitu ninachohitaji, nina kweli.”

Mara nyingi usiku nilipitiwa na usingizi nikiwa nimejaa fikra jinsi ambavyo mafundisho yanayokata kama upanga wenye makali kuwili yalivyoiumiza, kuichanganya na kuishughulisha serikali iliyojaa watu waliofunzwa vilivyo na wenye ujuzi mkubwa wa sayansi ya kisasa. Niliona kuwa hilo halingeweza kutokea isipokuwa msomi kupita wote, Allah mwenyewe alikuwa amempatia kitu fulani Mtume yule aliyeishia darasa na nne.
***
 
Shukrani sana mdau...kitabu hiki kinasaidia kuondoa woga...
 
Moja kati ya vitabu nilivyovipenda sana.

Nilikisoma cha Kiingereza nikiwa Tambaza Secondary School miaka ya mwanzo ya 1990s.

Kwa muktadha mzuri zaidi, ukitaka kujua maisha ya Malcolm X vizuri, ukimaliza hiki tafuta "Malcolm X : A Life of Reinvention" cha Manning Marable.

 
Kama CRIPS BLOODLINE FROM BLACK PANTHER MOVEMENT.......HUYU MALCOM (PRO ARABS) NA LUTHER
( PRO EUROPEANS) WALIKUA SNITCH,Z OVER BLACK RACE KUANZIA KITAMADUNI NA KIIMANI MPAKA KISIASA....THAT'S WHY BIG HOMIEZ TAKE BOTH OUT...!!!!!
ELIJAH MUHAMMAD NA LOUIS WALIAMUA KUKAA PEMBENI NA KUOMBA CEASE FIRE
LONG LIVE CRIP,S.....BLOODLINE.....IN 60,S.......!!!!
WITHIN CRIP,S MALCOM X DESERVE TO BE SMOKED.......HE SELL OUT OUR RACE....!!!
 
umeandika hekaya pro-Hutu.
 
umeandika hekaya pro-Hutu.
WEWE SIO MEMBA WA CRIPS NA HUJUI LOLOTE KUTUHUSU BLUE BANDAMA WORLDWIDE UTAJUA NINI KUHUSU MALCOM X.......NA WATU WANAONA AIBU KUKIRI HADHARANI MAPUNGUFU YAKE KUA MALCOM ALIKUA PRO ARABS.....NA MWENZIE LUTHER ALIKUA PRO EUROPEAN......!!!
NDIO MAANA SETS ZA MWANZO KABISA ZA CRIPS ZILIZOFORM BLACK""P"" MOVEMENTS MIAKA YA SABINI ZILIDECIDE FATE ZAO.......WALA SIO ClA...!!!
Walikua wanaukana ubantu na kupromoti tamaduni na siasa na dini ambazo sio za kibantu ili kuendeleza ukoloni wa watu wa mashariki na magharibi dhidi ya wabantu.....wakijinufaisha kupitia harakati feki.........na mbaya zaidi walikua informer wa state.
ALL SELL OUTERS...THEY DESERVE TO BE SMOKED........
 
kumbe mkichokozwa mnaandika vizuri. uliandika kihunihuni mwanzo.
 
kumbe mkichokozwa mnaandika vizuri. uliandika kihunihuni mwanzo.
SIO KIHUNI ILE NI LUGHA YA CRIPS....SASA LAZIMA NIJIKUMBUSHIE LUGHA YETU YA KITAANI NAPOZUNGUMZIA ISSUE YOYOTE INAYOHUSU OUR ORGANIZATION YETU YA BLUE BANDAMA WORLDWIDE...!!
Babu Njunju huwezi kunichokoza OG CRIPS.....coz sinaga hisia hasi kwa watu wenye mtazamo tofauti na mimi.
 
Allah Amsamehe madhambi yake na Amrehemu ndugu yetu Malcolm X. Wewe wengine tushaanza kukujua. Ni mtu unayechukia Uislam na Waislam. Hapa unajificha kwenye weusi na wala unga wa Crips and Bloods.

MLK umemtaja kujificha tu.

Sifa zote njema zinamstahiki Allah aliyemtoa Malcolm X kutoka pote la Nation of Kufr na kumuongoza katika Uislam. Allah Amrehemu Malcolm X.
 
Mkuu samahani......allah ndio nani????
Mungu wa kiarabu au????
Waafrika tunaoamini katika mababu zetu hatumtambui huyo
NB: TATIZO LA WABANTU MLIOKANDAMIZWA NA KUPOKEA FIKRA ZA WAKOLONI WA KIZUNGU NA KIARABU HASA NYIE MNAOWAPENDA WAKOLONI WA KIARABU HAMPENDI KUAMBIWA UKWELI...!!!MALCOM GOT SMOKED BY BIG HOMIEZ COZ HE SELL OUT OUR RACE TO OTHER COLONIALISM CULTURE,S
Dont mention blood that's our opp,s....nobody mention red bandama its insult's to our dead homie,s.....!!!
 
Mkuu samahani......allah ndio nani????
Mungu wa wakoloni wa kiarabu au kizungu????
Waafrika hatumtambui huyo
NB: TATIZO LA WABANTU MLIOKANDAMIZWA NA FIKRA ZA WAKOLONI WA KIZUNGU NA KIARABU HAMPENDI KUAMBIWA UKWELI...!!!
Dont mention blood that's our opp,s bro!!!
 
Mkuu samahani......allah ndio nani????

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ هُوَ ٱلرَّحْمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ


He is Allah, than Whom there is La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He) the All-Knower of the unseen and the seen (open). He is the Most Beneficent, the Most Merciful.


هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْمَلِكُ ٱلْقُدُّوسُ ٱلسَّلَٰمُ ٱلْمُؤْمِنُ ٱلْمُهَيْمِنُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْجَبَّارُ ٱلْمُتَكَبِّرُ سُبْحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ



He is Allah than Whom there is La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He) the King, the Holy, the One Free from all defects, the Giver of security, the Watcher over His creatures, the All-Mighty, the Compeller, the Supreme. Glory be to Allah! (High is He) above all that they associate as partners with Him.


هُوَ ٱللَّهُ ٱلْخَٰلِقُ ٱلْبَارِئُ ٱلْمُصَوِّرُ لَهُ ٱلْأَسْمَآءُ ٱلْحُسْنَىٰ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

He is Allah, the Creator, the Inventor of all things, the Bestower of forms. To Him belong the Best Names. All that is in the heavens and the earth glorify Him. And He is the All-Mighty, the All-Wise.

(Qur'aan 59 : 22-24)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…