Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,772
Mtunzi wa kitabu hiki maridhawa si mwingine bali ni mchambuzi na mwandishi mahiri wa makala,Mwalimu Nkwazi Nkuzi Mhango,Mtanzania mwenye makazi yake nchini Kanada.Licha ya ualimu na uandishi wa habari,Mhango pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu.Miongoni mwa safu maarufu za Mwalimu Nkwazi ni zile zinazopatikana katika gazeti la Tanzania Daima,ambapo hutumia jina la MPAYUKAJI MSEMAOVYO.Kadhalika,mwandishi huyu ni hodari katika fani ya kublogu,na "uwanja wake" unafahamika kama Free Thinking Unabii .Vilevile,unaweza kusoma makala za Mwalimu Nkwazi katika jarida la The African Executive