Kitabu Mzingile cha Kezilahabi kinahusu nini hasa?

Kitabu Mzingile cha Kezilahabi kinahusu nini hasa?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wandugu. Nimemaliza kusoma kitabu cha muandishi Euphrase Kezilahabi; Mzingile. Naona kama nimekielewa nusunusu. Kama kuna aliyewahi kukisoma naomba anielezee kinahusu nini hasa.
 
Ninacho hapa home ila kila siku naishia ukurasa wa pili.

Kile cha Dunia Uwanja wa Fujo nacho kinahitaji utulie sana!

Vitabu pekee vya Mwanafalsafa huyu wa "Udhanaishi" nilivyovielewa ni Rosa Mistika na Kichwa Maji
hahaaa, eti udhanaishi, kipige taratibu, kuna mambo yanafurahisha humo. Gamba la Nyoka pia ni rahisi kueleweka. Dunia uwanja wa fujo nilikisoma zamani, nilikipenda ila sikumbuki vizuri kama nilikielewa. Kuna mtu alisema Mzingile na Nagona ni vigumu, sikumuamini; kitabu cha kiswahili kinakuwaje kigumu🙂
 
Ndugu yangu Mzingile na Nagona mwandishi ametumia mkondo wa kifalsafa katika uandishi wake kwahiyo ni vigumu kweliii.

Japo kusema kweli Mzingile kurasa Tano za mwanzo ndo kinaeleweka kuanzia panapofuata mtafutano unaanza.

Kwa upande wa Dunia uwanja wa fujo ni moja ya kazi bora Sana za Kezilahabi kwani anazungumzia Maisha kwa ujumla ya wanadamu ambayo mwandishi ameyetaja Kama ni fujo za hapa duniani na anasema kila binadamu hapa duniani amekuja kufanya fujo zake kabla ya kufariki.

Akimaanisha kuwa Kama ni mwalimu fujo zake atazifanyia darasani kwa maisha yake yote Kisha anajiondokea zake hapa duniani, daktari fujo zake atazifanyia katika kutibu watu, wapo watakaofanya fujo za ujambazi, uzinzi nk.

Zaidi amemtumia mhusika mkuu aitwaye Tumain ameonesha namna alivyoonesha fujo zake kuanzia Maisha yake ya masomo, kuishi na wazazi wake, mapenzi, ulevi, kujihusisha na kilimo, kuua kiongozi, kupelekwa jela na hatimaye kunyongwa.

Dunia uwanja wa fujo ya Kezilahabi ni Bonge moja la hadithi, ikifuatiwa na Rosa Mistika.

Naomba kuwasilisha Tafadhari.

ASANTE.
 
Back
Top Bottom