Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kulia: Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi, 1962
Leo Mtaa wa Congo Barzani kwa Mzee Kissinger kwa muda paligubikwa
na mtikisiko kwa Wana-Barza kusimamisha dhumna na mazungumzo kwa
muda kuangalia na kupekua kurasa za kitabu, ''Shajara ya Mwana Mzizima,''
kilichoandikwa na mwandhishi maarufu Abdallah Tambaza.
Kitabu kina sura nyingi zinazoeleza historia ya Dar es Salaam ya 1950 historia
ambayo kwa hakika mtu huchoki kuisikia kwani ni historia ya wanamji wenyewe
waliofanya mengi ya kukumbukwa.
Je, unawajua vizuri wazalendo hawa: Mohamed Jumbe Tambaza, Mwinjuma
Mwinyikambi, John Rupia, Zubeir Mtemvu, Dossa Aziz, Haidar Mwinyimvua
ambao majina yao hawa mabwana wakubwa yanavuma hadi leo?
Kubwa katika historia ya mabwana hawa ni kuwa huwezi kumtaja wala
kumwandika Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama
hujatambuka vizingiti vya nyumba za mabwana hawa wa Mzizima na wao
wakakukaribisha ndani ukumbini wakakuweka kitako jamvini na kukupa
simulizi zao nani alikuwa Mwalimu Nyerere na nini kaifanyia Tanganyika
na watu wake.
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre, Mtoro na Manyema (Kariakoo)
na Tanzania Publishing House (TPH) (Samora Avenue).
Bei ni T.Shs: 10,000.00 tu.