Kitabu: The great Mortality

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
kati ya mwaka 1330 hadi 1355 duniani kuliibuka plague au tauni kali sana maarufu kama black death. Kitabu hiki kinaelezea chanzo, madhara na matokea ya Tauni hii huko ulaya. Tauni hii inasemekana iliua watu milioni 75 hadi milioni 100.
Kipindi hicho wayahudi walichinjwa sana wakituhumiwa kuweka sumu kwenye visima na wengine wakisema makabila ya kiyagudi yaliyopotea, Gogu na Magogu wamerudi na kuleta hayo maafa. Ni kakitabu kazuri ukitaka kujua hii ishu na ishu za magonjwa ya mlipuko.

mitale na midimu , Malcom Lumumba , Wick , James Comey , Alisina king kan
 
The Bubonic Plague. Baada ya hii tauni kutokea jamii ya watu wa Ulaya ilibadilika sana, mara nyingine ni lazima majanga yatokee ili nchi itie akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa aisee. Mwandishi anasema bila ile ulaya ingeendelea kuwa maskini na jinga.
Anasema kwa namna fulani ilichangia watu kutoamini sana kanisa maama lilishinda kuwalinda na hivyo kuchangia kuanzishwa kwa hizi ishu za waprotestant na ile imani kuwa kanisa lina ukweli wote ikaanza kuondoka. Kanisa zamani lilikuwa linakataza kufanyika kwa autopsy lakini hii ikafanya ianze kufanyika na kuleta mapinduzi kwenye elimu ya afya.
Pia mambo ya ukabaila yakaanza kukoma na hili ndilo lilikuwa badiliko kubwa sana.

Saizi nimeanza kuwaelewa wale mavillain ambao misheni zao ni kupunguza watu duniani 😁😁
 
The Bubonic Plague ya mwaka 1656 ilikuwa ni mwanzo tu. Mwaka uliofuatia 1666 kulikuwa na The Great Fire of London ambao ulinguza nusu ya mji wa London na ulishindwa kuzimwa kabisa. Maelfu ya watu walikosa makazi ya kuishi.

Moto walishindwa kuuzima kwasababu unaambiwa kipindi hicho mji wa London ulikuwa umeshonana kama uyoga. Kulikuwa na uchafu mwingi sana ambao ulichangia kuenea kwa ugonjwa wa tauni.

Hivyo wao wanakiri kwamba bila tauni na huu moto kutokea kusingejengwa London mpya ambayo wakazi wake walikuwa na uelewa mpana na wa tofauti kuhusu ulimwengu.

Mji uliojengwa baada ya hapo, ndiyo London ya leo tunayoijua, ambayo miaka michache baadae ilikuja kuwa kitovu cha mapinduzi ya viwanda dunia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je Africa au Tz in particular inahitaji this kind of purge?


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Rwanda ipo tofauti sana na Burundi japo zinafanana sana kuanzia ukubwa wa watu wake. Nchi zote zina wahutu kama 80%. Je yale mauaji ya kimbari yatakuwa yalichangia Rwanda kuwa ilivyo leo?
 
Aisee swali gumu kidogo lakini mbona waliokuwa wanalalamikiwa yaani wachache kutawala wengi ndiyo hali halisi inayoendelea mpaka sasa huko

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Watu wamepungua lakini haikusolve the core problem

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Safiii sana kwa kutujuza.

Black death,Nilipata au niliifahamu kwa uchache sana kupitia katika kitabu cha A brief history of humanKind kilichoandikwa na Noah Harari.

Itabidi nikipata muda niipitie vyema..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda ipo tofauti sana na Burundi japo zinafanana sana kuanzia ukubwa wa watu wake. Nchi zote zina wahutu kama 80%. Je yale mauaji ya kimbari yatakuwa yalichangia Rwanda kuwa ilivyo leo?
Bahati hakuna mtu anayeweza omba majanga, lakini ukweli mmoja jamii yoyote ile iliyopitia misukosuko kama manyanyaso, vita, mauaji, magonjwa, n.k huchukua hatua kubwa na za makusudi ambazo huijenga upya jamii hiyo.

Tanzania yetu hii bado tuna hangover ya ujamaa, lakini pia bado hatujapitia jambo ambalo limetutesa wote kama jamii (watalawa na wataliwa) ikafika mahala tukasema sasa tumenyooka na tuheshimiane, hebu tuweke mazingira fair kwa kila mtu kuendelea.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…