Kenya 2022 Kitakachotokea baada ya Rais Mteule wa Kenya kutangazwa leo

Kenya 2022 Kitakachotokea baada ya Rais Mteule wa Kenya kutangazwa leo

Kenya 2022 General Election

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1. Mwenyekiti wa Tume wa Huru ya Uchaguzi, IEBC anatakiwa kumkabidhi Rais Mteule Cheti (Mshindi wa Urais lazima ajitokeze kupokea Cheti)

2. Mwenyekiti lazima awasilishe kwa maandishi taarifa ya Matokeo kwa Jaji Mkuu na Rais aliyepo Madarakani, (Uhuru Kenyatta)

3. Kama itatokea Pingamizi la matokeo, lazima liwasilishwe ndani ya siku 7 tangu kutangazwa kwa matokeo

Mahakama Kuu italazimika kusikiliza na kuamua ombi hilo ndani ya siku 14 baada ya kuwasilishwa na uamuzi wake utakuwa wa mwisho
Ikiwa Mahakama Kuu itakubaliana na pingamizi la upande wa mlalamikaji, Matokeo yatabatilishwa na Uchaguzi mpya kuamriwa ufanyike ndani ya siku 60
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2017, kwa mfano, uchaguzi wa Agosti 8 ulipingwa na Raila Odinga na kusababisha Mahakama kusitisha Matokeo. Uchaguzi wa marudio ulifanyika Oktoba 26 ambapo Rais Kenyatta alishinda

4. Ikiwa hakuna Pingamizi lililowasilishwa Mahakama Kuu, Rais Mteule ataapishwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu Jumanne ya kwanza, wiki mbili baada ya tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya Urais na IEBC

Rais mteule ataapa kiapo kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Urais, kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 141 (3) cha Katiba ya Kenya.
Baada ya Kiapo, Rais atasaini Cheti cha Kiapo, na Rais anayemaliza muda wake atamkabidhi Rais Vyombo vya Mamlaka na Mamlaka yenyewe (Upanga na Katiba).
 
Back
Top Bottom