Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
======
UPDATE: Waliochukua fomu hadi leo, Julai 17, wamefikia 176
======

Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema

Hiyo namba nne yako ndio inakwenda kutokea, watashindwa na mwanamke halafu hawataweza hata kuangaliana usoni. Huo wingi wa waliochukua fomu hautawaacha salama, lazima wapasuke makundi.

Japo wao wanaona sifa wengi kujitokeza kwenda kuchukua fomu, utadhani hizo fomu wanazichukulia mwezini.
 
Hiyo namba nne yako ndio inakwenda kutokea, watashindwa na mwanamke halafu hawataweza hata kuangaliana usoni. Huo wingi wa waliochukua fomu hautawaacha salama, lazima wapasuke makundi.
Makundi ndani ya CCM YALIKUFA RASMI 2015 usitarajie kuyaona tena.AKISHAPITISHWA MMOJA WOTE WANAUNGANA KUMUUNGA MKONO

Hapo ni demokrasia tu iko kazini,KILIMAJARO WAMEOMBA WATU 241 kuomba kuteuliwa na CCM .CHADEMA wengi wahawajaomba sababu hawaitaki chadema .Ushahidi majimbo ambayo Chadema wamweka wagombea ni asilimia tano tu ya majimbo yote ya uchaguzi Tanzania
 
Dah...kibongobongo...kazi ya ubunge ndiyo kazi rahisi kukiko zote ....inahitaji sifa mbili tu ..kujua kusoma na kuandika...wakati Konda wa daladala lazima ajue na kuhesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Makundi ndani ya CCM YALIKUFA RASMI 2015 usitarajie kuyaona tena.AKISHAPITISHWA MMOJA WOTE WANAUNGANA KUMUUNGA MKONO

Hapo ni demokrasia tu iko kazini,KILIMAJARO WAMEOMBA WATU 241 kuomba kuteuliwa na CCM .CHADEMA wengi wahawajaomba sababu hawaitaki chadema .Ushahidi majimbo ambayo Chadema wamweka wagombea ni asilimia tano tu ya majimbo yote ya uchaguzi Tanzania

Bashite vp
 
Unaishi wp mkuu mpk unajitoa ufahamu hv?? Hakuna uchaguzi usio na makundi hata ss huku chadema makundi yapo,.lkn tofauti yetu na ninyi ni kuyalea...sisi chaguzi ikiisha na kundi linavunjika rasmi...ccm yanalelewa hadi uchaguzi ujao...ndo pale sisi wapinzani tunaponufaika nayo kwn huja na tukose wote
 
Unaweza kuwa sahihi maana halima 2010 aliupata baada ya Katibu wa Mkoa wa CCM kuingiza jina la Kizigha kinyemela wanaCCM wakanuna na kumpa mdee.
 
Back
Top Bottom