Usisahau nyumba ndogo......Hebu fafanua kwa lugha nyepesi hii kauli nielewe
Hebu fafanua kwa lugha nyepesi hii kauli nielewe
Usisahau nyumba ndogo......
Ok, well-noted!! Kwa sababu mi ndio nitakayeoa,nadhani nitakuwa na sauti hata kama sihusiki kwenye KP,so my voice will have effect on it....mi ninavyojua ndoa is not all abt KP,kama yy ataona hamna ndoa without KP...then nitacheki altenatives nyingine...na ndio maana nasema mpaka nijiridhishe.
So Carmel...ahsante kwa kuendelea kunichanganulia hii kitu.
Unajua, usipende kuwa dictator katika maisha ya ndoa yajayo au ambayo unayo, utabaki unanyooshewa vidole bila sababu za msingi. Huwezi in any how kumkataza mtarajiwa wako eti asifanyiwe kitchen party!!! Labda uniambie umevuta mwanamke ukakaa naye for sometime then unataka kuhalalisha kwa njia ya ndoa. Lakini kama binti unamuoa akiwa bado kwa wazazi wake, huwezi narudia tena kumkataza asifanyiwe kitchen party.KP kwa kawaida inaendeshwa kulingana na wanafamilia wanavyotaka na walivyo kwa asili yao.
MC au mtoa mada siku zote anaambiwa shughuli hii ni ya watu gani! kama mcharuko basi mwanzo mwisho shughuli itakuwa ya kimcharuko, kama ya kidini basi mwanzo mwisho sherehe itaendeshwa kidini, hakuna kitu kinacholazimishwa pale iwapo wahusika hawakitaki. Na ukweli ni kwamba KP siku hizi inakaribia kufuta send-off, na ukilinganisha hata ukifanya comparison ya zawadi alizopata binti kwenye send-off na KP utagundua kp ndo kapata zawadi nyingi, na za maana kuliko kwenye send-off japo na wanaume walishiriki. Kiukweli kp siku hizi lengo kubwa sio matusi, bali ni kupata vyombo hasa vya jikoni kwa binti, na mafundisho ya hapa na pale ingawa ya ndani hayafundishwi hadharani
Ushauri wangu wa bure kwako ni kwamba, wewe ukichagua binti mstaarabu basi tegemea kp atakayofanyiwa itakuwa ya kiistaarabu, ila ukichagua mswahili na mcharuko basi tegemea kp kuwa ya aina hiyo, lakini si wewe kuwapangia wazazi eti wasimfanyie kp binti yao!!!!!!!! utakosa mchumba kaka
Hii sio kitchen party, ni kufundishana uhuni....binti mmoja aliambiwa hivi kwenye kitchen party " mwanangu sufuria haikai kwenye mafiga mawili!!! shurti ili ikae uitengenezee mafiga 3, alafu mwanangu ukibeba ndoo kichwani jua kuna kujikwaa!! shurti mwanangu uwe na kidumu mkononi mama ili ndoo ikidondoka ubakie na kidumu!!! yule mfundaji akaongezea tena kusema, binti sikiaaaa jicho moja likipofuka mwanangu huitwa chongo sio jicho tena!!
nikashindwa kuelewa kama pale kunajengwa ama kunabomolewa!!!
Amaaaaaa hizo ndio kitchen party zetu za leo tunazokwenda kuchukua mitandio huko.
sasa KP ni kwa ajili ya vyombo vya ndani..
Hii mada ni nzuri sana............Carmel na Pearl michango yenu imekaa kirealistic zaidi kuliko wengi tunavyotizama............ aksanteni na mbarikiwe wote mliochangia humu.
KP inategemea inafanywa na watu wa familia gani na kivipi otherwise si KP zote ni ovu na si zote hufanyika kwa siku moja kuna ambazo zinakwenda ndani ya wiki nzima ambapo binti anapewa mafunzo ndani si adharani na wamama waliosafi na ndoa zao na kisha siku ya mwisho ndo sherehe ambapo hupatiwa na zawadi.
Sizinga nisamehe loh nilikuwa najaribu kukumbuka jina lako nikasahau kabisa.Hujanitaja??hahaaa...
Ni kweli utakosa mchumba kwa maana kwamba, kama ukipata mchumba then unampa masharti ya kutofanya kp, unadhani atakapoliwakilisha kwa wazazi wake responce itakuwaje? Imagine huyo akutolee nje just bcoz of that, ukapata mwingine the same si utapata tabu hata wewe mwenyewe tena itabidi urudishe nyuma maamuzi yako. Na mabinti wengi wa siku hizi wana-prefer kp zaidi kuliko send-offHaa!aine??nikose mchumba kwa ajili ya KP??Sidhani!!
Kuna swali sijibiwi...wanaume wanafuata nini kwenye KP??
Na kwanini KP nyingi zimebadilisha maana??na kwanini ziendelee kuitwa KP??
Kwanini wasiseme tunaenda kwenye mdundiko tu..??
Halafu inshu ya kusema eti kwenye KP anapata zawadi nyingi kushinda kwenye send-off is HolyCrap!!Imagine mke wangu hafanyi Kp bali anafanya Send-off tu,kwanza atakuwa amebalance bajeti, isitoshe wale ambao waliandaa zawadi za kp watazileta kwenye SO..kwahiyo percel zitakuwa maradufu!! u get the point??
Hii kitu si udikteta, bali ni ninyi wenyewe akina mama kuichakachua hii kitu KPs..u get that??
SMUAti lengo ni 'kupata zawadi tu'!....kama ni hivyo nadhani tuna matatizo makubwa sana vichwani mwetu...sijui tumerogwa na nani! Hivi kweli unaandaa sherehe kwa gharama kubwa ili upate zawadi tu? Ni umasikini wa aina gani unatusumbua?
Aksante AineNi kweli utakosa mchumba kwa maana kwamba, kama ukipata mchumba then unampa masharti ya kutofanya kp, unadhani atakapoliwakilisha kwa wazazi wake responce itakuwaje? Imagine huyo akutolee nje just bcoz of that, ukapata mwingine the same si utapata tabu hata wewe mwenyewe tena itabidi urudishe nyuma maamuzi yako. Na mabinti wengi wa siku hizi wana-prefer kp zaidi kuliko send-off
1. Wanaume kimsingi hawatakiwi kwenye kp, isipokuwa wao wanakuja kikazi zaidi, kupiga picha za mnato na video.Ukweli ni kwamba hatuna wataalam wa masuala ya video wengi na picha za mnato, ndiyo maana inalazimu kuita wanaume lakini si kusudio.
2. Kubadilishwa maana kwa kp narudi pale pale, inategemea na wahusika wa tukio ni wa aina gani
3. Kwamba aseme tunaenda kwenye mdundiko! yenyewe initwa kitchen party ( sherehe/pati ya jikoni)sasa watasemaje wanaenda kwenye mdundiko? ebu kuwa realistic Sizinga bwana