SMU
Hapana hili si lengo zima la KP ingawa maana halisi siku hizi imepotea......
Lakini siku zilivyozidi kwenda ikageuka kuwa sherehe ya kumpongeza binti kwa kumpata mwenzi wake au kumletea mama/mzazi wa kike heshima nyumbani (na ndio maana wahusika wakuu huwa ni wanawake zamani ilikuwa wamama watu wazima kisha na wasichana wakaanza kualikwa kukidhi sehemu ya marafiki wa binti)
Ila siku zinavyozidi kwenda ndio maana halisi ya KP inavyozidi kupotea.......... kwa sasa hivi nyingi hazina tofauti na send offs.
Wanapewa mafunzo ya ndoa na mapenzi kwenye mikusanyiko inayoitwa "kitchen Parties". Katika mafunzo hayo wanaambiwa mambo ya mapenzi na hususan jinsi ya kufanya mambo fulani fulani na kuhusiana na mwenza. Matarajio ya mafundisho hayo ambayo hukusanya wanawake wengi ni kuwa mfundwa (kama tunaweza kuita huko ni kufundwa) ni kwamba atakuwa amejiandaa kwa maisha ya ndoa na mapenzi.
Kitchen Parties kimsingi imechukua nafasi ya utamaduni wa unyago ambapo wamama watu wazima ambao wanaheshima katika jamii hutoa mafunzo ya maisha ya ndoa kwa mabinti mara kwa mara (kama siyo mara zote) ni mabikira au ambao hawajawa katika mahusiano ya muda mrefu (wachanga wa mapenzi). Unyago uliongozwa na wale tuliowaita Makungwi. Siri za unyago kwa wamama zetu ni siri wanazoenda nazo kaburini. Mambo ya KP yamekuwa ni gumzo na yanarekodiwa kwenye video siku hizi.
Miaka hii michache iliyopita dada zetu na wadogo zetu wamepelekwa huko (au wamejipeleka wenyewe) na kufanyiwa hizo kitchen parties. Kwa upande wetu sisi wanaume sijui kama tumefaidika na mafunzo hayo au ndio tumepata ubutu wa kisu cha kina dada kujua kuwa na "vidumu" au kuwa promiscuous au kutojali mapenzi ya mume.
Hata hivyo ninabakia kujiuluiza kama maisha ya ndoa na mahusiano kati ya mume na mke yamejengwa au kufaidika na haya mambo ya KP au ni bora njia bora ya kutumia wamama watu wazima kufundisha mambo haya? Ni mama gani leo ambao ana ujuzi wa mambo ya mapenzi kama hawa vijana? Sehemu nyingine tumeona kuwa KPs inahusiana na mambo ya ngono zaidi kuliko mahusiano ya wapendanao kiasi kwamba wadogo zetu na dada zetu wanafikiria mahusiano ya ndoa ni mambo ya ngono tu.
Kitchen parties ni sehemu ya suluhisho ya matatizo ya ndoa au ni sehemu ya tatizo?
Carmel, ni kweli unayosema ila bado sidhani kama KP ni suluhisho la mahusiano bora kati ya watu wawili ambao wanaenda kuishi pamoja. KP inafanyika siku moja na haizidi lisaa limoja la hayo mashauri utakayopewa na baada ya hapo ni kula, kunywa, kucheza na zawadi. So ukiangalia muda uliotumika katika kumfunda huyo bibi harusi katika hiyo party haizidi one hour. Unadhani huyu aliyefanyiwa KP atakuwa amefaidika zaidi ya yule ambaye hakufanyiwa?
Hayo yote ni mawazo ya wanaume.Kwa wanawake wamekuwa wanatumia kucheza uchi.Ninayo video moja jamaa alinitumia hilikuwa kitchen party kinondoni.Uwezi amini ni kama danguro,walianza taratibu mara wakavua brauzi,mara siketi ,wakabaki na kufuli mziki ulipokolea wakafua hizo kufuli.sasa hapo bibiharusi mtarajiwa anafundishwa nini?
ah ah ah anafundwa mziki ukikolea avue lol
Sizinga nisamehe loh nilikuwa najaribu kukumbuka jina lako nikasahau kabisa.
party ya jikoni kwa kiswahili... maana yake ni kupeana vyombo vya kukusaidia kumpikia mumeo
naskia siku hizi wanafundishwa maujuzi ya kitandani
Na kwa mtazamo wangu mie zinachangia pia katika kuvunja ndoa kwa sababu hata ile maana haisi ya baba kuwa kichwa cha nyumba kinapotea kwa sababu kwa vizazi vyetu vya dot com ambavyo heshima na maadili ni vya kuvuta na kamba kama binti wa dot com kaingia nyumbani kwako na kiiiiila kitu mpaka kitanda, makochi dijui dining sets, deepfreeza n.k. siku mkikorofishana hakawii kukwambia anakuweka mjini .............au kukunyima kwani utamfanya nini maana mpaka uwanja wa mazoezi kauleta yeye ni mali yake ................hahahahaaaaaaaaaaaa wakaka wa siku hizi kazi mnayoKitchen party siku hizi ni kama party zingine tu! Bibi harusi anapata vyombo vya ndani vinaenda kumsaidia huko kwake mafunzo anakuwa keshapewa akiwa ndani kwa wiki mbili wengine mwezi mzima, kwa hiyo siku hizi mkeo akienda kp ukae home usubiri maujuzi imekula kwako
huwa najiuliza kama kila wanachofundwa wadada ni kwa mujibu ya mahitaji ya waume zao. Kwa mfano anafundishwa kukata kiuno, kuvaa shanga kiunoni, kumnyenyekea mume, sijui na mengine mengi. Lakini hawajawahi kuwauliza wanaume wanafurahishwa na nini katika ndoa.
pia najiuliza kama huwa wanafanya ufuatiliaji kiwango ambacho mafunzo yao yameboresha mahusiano na ndoa za waliopigwa KP. Au kutafuta kutoka kwa wanaume kwamba wanapenda nini hasa na matatizo ya ndoa ni ya aina gani na ni kwa namna gani yanakabiliwa kwa tija.
otherwise, it is a belief that mwanaume anataka haya na haya which is not necessarily the case