Kitchen Party za siku hizi ndio chanzo cha usaliti ndani ya ndoa

nitonye

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
7,342
Reaction score
3,885
Mimi najiulizaga hivi mwanamke asipofanyiwa sherehe kitchen party hawezi kuwa mke mwema kwa mmewe. Maana siku hizi kwenye kitchen party kuna misemo kama vile ''sufuria haikai kwenye figa moja'' au ''ubebapo ndoo sharti ubebe na kidumu mkononi kwa ajili ya balance'' haya maneno yanaongeza usaliti kwenye ndoa
 
Tatizo lako umezidi kupiga chabo hata mkeo unampiga chabo

Ndiyo maana ndoa za siku hizi ni kama fasheni tu, Kuna haja sasa serikali kuingilia kati maana yanayofanyika huko mhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!
 
Mkuu afadhali umenena maana sikuhizi kwenye kitchen party kuna msemo maarufu wenyewe wanasema "Mwanamke anauza Utumbo haogopi inzi" sasa mkuu hapo jibu unalo!!!
 
hakuna kicheni pati bora kama ya nyumbani
 
Mkuu afadhali umenena maana sikuhizi kwenye kitchen party kuna msemo maarufu wenyewe wanasema "Mwanamke anauza Utumbo haogopi inzi" sasa mkuu hapo jibu unalo!!!

Umeona eh sasa kweli kuna ndoa hapo baada ya huyu mwanamke kutoka hapo
 
duh... Utumbo siku hizi dili eeh.....
Nilipata kusikia kuwa ukiopoa mdada zama hizi (sasa sijui bongo pekee au na mikoa mingine..) Kuwa usipoomba upewe utumbo mdada wa kileo anakuona ****.... Ila nilizipokea kwa fadhaa kubwa sana taarifa hizo...!
 
mie zote nilizohudhuria sijawahi kusikia kuhusu mafiga matatu, na ndoo na kidumu ila nimesikia kumuhusisha sana mungu kwenye ndoa ili akupe hekima ya kuijenga ndoa yako kwa msingi imara na mengine mengi ya busara zaidi kiujumla kitchen party nilizohudhuria zinanijenga na kunikumbusha mambo mbalimbali nayotakiwa kufanya as woman.
 
duh... Utumbo siku hizi dili eeh.....
Nilipata kusikia kuwa ukiopoa mdada zama hizi (sasa sijui bongo pekee au na mikoa mingine..) Kuwa usipoomba upewe utumbo mdada wa kileo anakuona ****.... Ila nilizipokea kwa fadhaa kubwa sana taarifa hizo...!
utumbo ndo nini?
 
Jamani haya mambo ya mafiga matatu hawa wanaume sijui wanayapata kitchen party ya wapi., mi huwa nayasikia mtaani tu!!!
 
Jamani haya mambo ya mafiga matatu hawa wanaume sijui wanayapata kitchen party ya wapi., mi huwa nayasikia mtaani tu!!!

Tatizo kitchen party mnatuzuia kuingia halafu mnarecord sisi tunaangalia kupitia mikanda na tunajua kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…