Kitendawili katika kutunuku majina ya mitaa ya Dar es salaam kwa wapigania uhuru wa Tanganyika

Kitendawili katika kutunuku majina ya mitaa ya Dar es salaam kwa wapigania uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITENDAWILI KATIKA KUTUNUKU MAJINA YA MITAA YA DAR ES SALAAM KWA WAPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Ysxwq6h0vUafe2oaBXeGmbFwW2114Nv91X0D2g2TorX9DVf7g-9pFwZwb60PRP08jr1qfm0Mj85GU0Zxd1WVZlQOYzSap0VwFWqCMB-qdlaJKSBziSvpMHjyrwK-y5n9seQuT5ieTQVeu0jTFLDMdXvpustJGkSI_6gYHlc5PrC68Bqf36_1OAwS1veQI3kgaVPQEwctm6lITMvDm8oPc-BIS9RuXWpsw1FYhijRDFf3oKOghSygOPFhliS3unE8ZpdMvkJVliUShosKj1FtosNOzofmbj-ZL9P1JyFNSMDOyZdB8NW2ZVFZaMbpQbPKgaf-dxyz_2aXJ-cpAkv_QlHKfgDzL7fbCYb8xieGOJdRJVWv7I8kTxp-AJYs3KfWnSnk5o3CA5sS9A2pg3NohEgiYHKHl3prN08uOkPCHvgXjK43HNGRZWlkeJoLRCakpF-1oylc7liLQ5wC2FnjdC4h23vpscPgYIOFTUmlLPVqeJ33Se7wZElPgi32_T3bhJvkWpz9aXY_BJKZwbOiNRUuugtyaIbV0CGmSW5GpMGSXmMCQYz8DUOZpWNk2AcqaXaIW3r7GoqMVWojasVvIe40zDi8AdCC-D43jnr__NF-BFI8YA=w493-h657-no


Mtaa huo hapo kwenye hiyo picha hapo juu zamani ukijulikana kama Somali Street. Katika miaka ya 1990 wakati Kitwana Selemani Kondo ni Meya wa Jiji alibadili baadhi ya majina ya mitaa na kuipa majina ya wazalendo walioacha alama katika historia ya kupigania uhuru wa Tangnayika.

Lilikuwa wazo zuri isipokuwa kwa jambo moja nalo ni kule kutoa majina kwa baadhi na kuacha baadhi. Baya zaidi ni kule kuwaacha wale ambao michango yao ilikuwa mikubwa sana na kutunuku majina mitaa kwa wengine ambao michango yao haikuwa kwa kiwango kuzidi hao walioachwa.

Mtaa wa Somali katika miaka ya 1950 wakati wa kudai uhuru wakiishi wazalendo wawili katika harakati za TANU – Omari Londo na Zuberi Mtemvu. Mchango wa Mtemvu ulikuwa mkubwa kuliko wa Londo lakini jina la mtaa amepewa Londo.

Yawezekana Mtemvu kanyimwa heshima ile kwa kuwa alitoka TANU mwaka wa 1958 na kuanzisha chama chake cha Congress alipotofautiana na Nyerere katika suala la Kura Tatu.


2016%2B-%2B1

Mtaa wa Somali kama ulivyokuwa katika miaka ya 1950/60

image001.jpg

Aliyekaa mbele anatabasamu ni Omari Londo na nyuma yake ni Abdallah
Kassim Hanga na juu ya jukwaa ni Julius Nyerere

Gerezani ulipo Mtaa wa Omari Londo kuna Mtaa wa Mbaruku. Mtaa huu ndiyo Mtaa aliokuwa akiishi Dossa Aziz mmoja wa waasisi wa TANU na mfadhili mkubwa wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Jina la mtaa halikubadilishwa na mtaa kupewa jina la Dossa.

Lakini kitu cha ajabu na cha kusikitisha ni kuwa mtaa wa mbele yake uliokuwa ukijulikana kama Kisarawe Street umepewa jina la Yusuf Makamba. Mimi sijui mchango wake katika historia ya Tanganyika na wala sielewi kwa nini mtaa ule asipewe mzalendo yeyote yule katika wazee wa Dar es Salaam waliotoa mchango mkubwa katika kupinga ukoloni.

Ndugu msomaji hebu soma kisa cha Mtaa wa Mshume Kiyate ambao alitunukiwa Mzee Mshume lakini mamlaka imekataa kuntunuku.

MTAA WA MSHUME KIYATE ZAMANI MTAA WA TANDAMTI
Ukweli ni kuwa Mtaa wa Mshute Kiyate haupo kwa sababu wahusika wamekataa kubadili kibao cha jina sasa yapata zaidi ya miaka 20. Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ndiye aliyefanya mabadiliko ya majina ya mitaa kuwaenzi wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa kuipa majna yao ile mitaa waliokuwa wakiishi.

Hivyo ndivyo Mtaa wa Kipata ujabadilishwa na kuitwa Mtaa wa Kleist Sykes, Mtaa wa Somali ukaitwa Omari Londo, Mtaa wa Aggrey ukaitwa Max Mbwana, Pugu Road ikaitwa Barabara ya Mwalimu Nyerere, Bi. Tatu binti Mzee akapata mtaa Ilala na Mtaa wa Tandamti ukabadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Mshume Kiyate. Lakini palizuka malalamiko kuwa kilichomsukuka Kitwana Kondo kubadili majina ni hisia za udini.

Hii ni baada ya kuonekana wazalendo wengi waliopewa majina ya mitaa ni Waislam. Magazeti yakahoji ni michango gani wazalendo hawa walitoa? Kitwana Kondo katika mahojiano aliyofanya na marehemu Sarah Dumba wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alijibu kwa kusema, ''Ikiwa hamjui michango ya watu hawa ulizeni mtaelezwa.''

WAZEE+WA+TANU.jpg

Kulia wa pili ni Mshume Kiyate

tAZ7Q0CbeIpy9U9VrFhQRXVT3KiZoLVWyGRWVQGRN9MQ2MWqQTn6Pdw3hADo7z3DvALdD5Hr-xQ=w724-h567-no

Kushoto: Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere na Mshume Kiyate
Uchaguzi Mkuu wa 1962

kZ5LlMCgqPD9R9E5MUJWPN7_q0YkFwuZ732t0R3I0t0syOWSj010wSWEJ86ITul2cP47F7129sUqM_HUpVtOZjmFQio9OsxRtKebLa_HpMKZKvafFEQbCGKmZVMIAIy__ySItYdDqt7qArsJxhbL94SDaa8gHX6hoZpGwr_BZWnKCfRt5w9jmYUazcP2VmGSkm0cQcl_24UlzGW6nurImglkiFErzw2lThH2yfJqBaR1NQbLykO7Jj5X7oQ9f5mUtNQGRalLpkbPXz2fltNHdud0_qd4z41aJRz71KAJw7QNF3TBcArqWCduGyG9rZ_pmKzuTNdJwH1-8RGPhoFE2op62QgcQ4VMElKTyYSS0J_WUnDuQfHnDiy0z_NmziEGDLv400xMrWNXpeShnklbBKYS-WBI0O1mCax5BpkS7yZXOH74IUl8Iv6c1uVoDei5gxhl9uBNMnDjfNJyvnBPe9n6SLIKGbKkogeWR_0J3s0Zckv0FkQBAqwDp_5lnIg_M-bUlyjn1wfjCdxL7sX4aTo9__UZNTAt8dtxiEQwDl6wcJBmROaxXXAqfD1mFmUhz2s4644v8HFr6Ac_kVCyU9uUqngP49U=w360-h480-no


Mzee Mshume Kiyate akimfariji Mwalimu Nyerere baada ya maasi ya wanajeshi
20 Januari 1964
2016%2B-%2B1

Mtaa wa Mshume Kiyate katika mihangaiko ya kutafuta rizki nyakati za mchana wakati wa kutafuta rizki

20160524_142811.jpg

Mtaa wa Mshume Kiyate karibu na Soko la Kariakoo kama unavyoonekana hivi sasa
 
Endelea kutujuza wataelewa tu.

Uongo huja na rift wakati ukweli huja kwa ngazi
 
Mkuu Mohamed Said , hautakaa uridhike kamwe, sasa unaanza kulalamika nani alikiwa mpiganaji mkuu, kwa nini kapewa Londo badala ya Mtemvu,

Dossa na Takadiri wana mitaa yao mirefu tu pale Magomeni inaanzia mapipa ya Sunna mpaka Mapipa ya Mzimuni, Ziota na wengine wengi wana mitaa yao pia hayo maeneo, na majina hayo yalitolewa wakati wa Nyerere
 
Mkuu Mohamed Said , hautakaa uridhike kamwe, sasa unaanza kulalamika nani alikiwa mpiganaji mkuu, kwa nini kapewa Londo badala ya Mtemvu,

Dossa na Takadiri wana mitaa yao mirefu tu pale Magomeni inaanzia mapipa ya Sunna mpaka Mapipa ya Mzimuni, Ziota na wengine wengi wana mitaa yao pia hayo maeneo, na majina hayo yalitolewa wakati wa Nyerere
Kituko,
Sijui unakusudia nini kwa kusema ''siridhiki.''
Labda nikuulize siridhiki na kitu gani?

Mimi silalamiki maana kulalamika kwanza uwe mlalamishi.

Mie nikiona jambo halijakaa vyema kwangu hutafiti kisha
naandika kama hivi.

Zuberi Mtemvu anastahili mtaa kwa kazi aliyofanya kwa
TANU.

Huo mtaa wa Takadiri wa Magomeni si kwa heshima ya
Sheikh Suleiman Takadir hii ukae ukijua.

Huo mtaa unaosemwa ni ''Dossi,'' siyo ''Dossa The Bank,''
aliyekuwa mfadhili mkuu wa TANU.

Dossa hadi leo hana mtaa.
Hili nalo ukae ukilifahamu.

Ingia hapo chini kwa historia za wazalendo hawa:
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Mohamed Said: Dossa ‘’The Bank’’ Aziz: Tajiri Aliyefilisika Kwa Kupigania Uhuru wa Tanganyika: Sehemu ya Kwanza
Mohamed Said: JINAMIZI LA UDINI TANZANIA: UTABIRI WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR
 
Back
Top Bottom