Kitendawili {malenga wapya}

Kitendawili {malenga wapya}

Viper

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2007
Posts
3,666
Reaction score
1,404
Jogoo lina mafamba, linatamba kiamboni,
Kwa kiburi lajigamba, hadi kiambojirani,
Hili jogoo la shamba, sasa lawika mjini,
Kitendawili na tega, mteguzi ategue.


Mbawa linavyozipiga, wengine hawasogei,
Shuti nejawa na woga, wote wamekuwa hoi,
Kama wenyewe mwafuga, kitoweo halifai,
Kitendawili na tega, mteguzi ategue.


MALENGA WAPYA
 
Jogoo hilo khatari,sasa ilmeelevuka.
Linasambaza khabari, kula kona laitika,
Wakati huu shubiri, maradhwi yameitika,
Haraka apewe jiko, ulinusuru na baa.

Kuungana walimwengu, ni neno lenye mwafaka,
Linapendeza kwa Mungu, pamoja na malaika
Kukwambia fanya langu, Jiko haraka kamata,
Haraka apewe jiko, ulinusuru na baa.

Dr Hamza Yousuf Al Naamani( Barubaru)
1523 Umm Hays
Doha. Qatar
 
Back
Top Bottom