Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Of all the people ndani ya chama cha mapinduzi eti CCM wanamleta Stephen Wassira. Mzee wa miaka 80 eti awe ndiyo makamu mwenyekiti wa chama hicho. Hili ni jambo la kustaajabisha sana kwa viwango vyovyote vile. Na hii ni kwa sababu zifuatazo.
1. Tulitegemea CCM ijifunze kwa Kujiuzulu Kinana.
Kinana aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CCM mara kibao alisikika akisema kuwa amechoka anaomba apumzike. Kinana yeye ana miaka 74, Huku Stephen Wassira ana miaka 80. Katika hali ya kawaida tulitegemea CCM ijiulize mara mbilimbili kuwa kama huyu mwenye 74 anaona kazi inamuelemea (kwa changamoto za mambo mengi zikiwemo za uzee), Je huyu wa miaka 80 ana nafuu gani kumshinda mdogo wake wa miaka 74?.
2. Mzee siyo kweli kuwa yuko fit kiafya
Mzee Wassira anaishi Mbweni, watu wanazijua changamoto zake za kiumri, ikiwemo hata kufanya mazoezi kwa kusaidiwa. Kwa nini CCM isilione hili?. Huyu mzee anayehitaji utulivu ili angalau aweze kutumia nguvu zake ndogo uzeeni, kwa nini CCM inakuwa na ubinafsi kiasi hiki, haionei huruma wazee, kwa nini isimuache mzee wa watu kupumzika?
3. Yumkini CCM imepungukiwa na pool ya watu wenye uwezo.
Mzee Wassira ni mtu aliyehudumu katika chama na serikali tangu miaka ya 1970's wakati huo Rais ni Nyerere, na wakati huo Makongoro Nyerere akiwa shule ya Sekondari. Mtu kama huyu ana kipya gani kwa CCM ya sasa na ana mawazo gani ya kuendana na nyakati za sasa.
Soma Pia: Stephen Wassira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara
Hili jambo linatupa ishara moja, kuwa CCM ya sasa haina watu wenye gravita kubwa ya kisiasa, wenye uwezo na kwa hiyo inaenda kukopa kwa watu wa zamani wa enzi za Nyerere. Hii ni aibu na fedheha kwa CCM ya hivi karibuni kushindwa kutengeneza viongozi. Ukianhalia safu za makada wa CCM walio wengi ni wepesiii hakuna manguli wa kisiasa.
4. Huenda Samia anataka aendelee na mazungumzo na Upinzani anadhani Wassira atamsaidia.
Ni kweli, katika watu ndani ya CCM waliokuwa na Intellectual prowess (uwezo mkubwa wa kiakili) wa kudeal na Wapinzani na kwenda nao hoja kwa hoja ni Wassira. Kwa hiyo kama mazungumzo ya maridhiano yatahuishwa, Wassira ndo atachukua nafasi ya Kinana ktk mazungumzo hayo. Nadhani ni matumaini ya Samia kufikiri kuwa Wassira ataweza. Hata hivyo Samia amesahau kuwa Wassira wa sasa, siyo Wassira wa enzi za Jakaya miaka 10 iliyopita. Huyu wa sasa ni mzee sana. Na ukizeeka sana hata akili inaslow.
5. Ni kudhihaki waasisi wa CCM waliohudumu na kuamua kung'atuka uongozi wa chama ili chama kipate uelekeo mpya.
Kawawa alistaafu siasa za CCM akiwa na umri mdogo tu kulinganisha na Wassira, akiwa chini ya miaka 70. Nyerere akaacha siasa za uongozi wa CCM mwaka 1990 akiwa na miaka 68 (Wakati huo kofia za mwenyekiti na rais zilikuwa tofauti). Sasa huyu mzee wa miaka 80 wa nini, alete nini?
6. Mwenyekiti wa CCM haonyeshi umakini kwenye kuunda timu za kumsaidia kazi.
Hili limedhihirika katika teuzi anazozifanya kama rais, teua tengua zisizoisha, recycling isiyoisha, na sasa amefanya kituko cha karne kwa kumleta mtu wa mwaka 45 ili eti awe makamo wake. Inashangaza sana!