Mkirua asante ila tunarudi pale pale kwamba kama ni utamaduni unaenda ukibadilika na muda...yani nao unaenda na wakati.Hivyo basi huu nao umeenza kujiingiza kwenye utamaduni wetu...hata kama sio wa Kitanzania bali ni wa kundi fulani ndani ya Tanzania ...kama ambavyo mila na tamaduni za baadhi ya makabila zikivyo. Kwasababu tu baadhi ya mila na tamaduni za makabila mengine hazinihusu mimi siwezi kukataa kwamba nazo ni sehemu ya utamaduni wetu japo sio taifa zima linazozikubali na kuzifuata.
Hivyo hivyo kwa hawa watu...ndio maana siku hizi hata nguo wanaweza vaa vile wanavyopenda..kutembea tofauti na inavyoaminika mwanaume anatakiwa atembee...kuongea kwa madaha ya kike n.k mbele za watu...mitaani na hata majumbani.
Inawezekana wakawa hawakubaliki kwa asilimia kubwa ya Watanzania ila wapo watu wanaowakubali...na wao kama kundi wameufanya huu utamaduni kua wao.Kadiri kundi litakavyoongezeka ndivyo na utamaduni wao utavyoshika kasi ya kua kwenyr chati sawa na tamaduni zetu nyingine.