Kitengo cha Ukusanyaji Madeni CRDB bank wanakula rushwa

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,108
Reaction score
1,132
Habari wadau,

Kumetokea sitofahamu hivi karibuni kati ya wakusanya madeni na waendesha minada ya CRDB BANK kitengo cha kukukusanya madeni baada ya CRDB benki kutoa kazi kwa madalali hao kisha kuingilia kati mchakato huo kwa kuwasiliana moja kwa moja na wadaiwa na kuwaomba rushwa ili kusitisha zoezi husika.

Hii imekuwa ni kawaida ya maofisa hao walioko CRDB makao makuu kitengo cha kurejesha mikopo kupokea rushwa na kusitisha uuzwaji wa mali za wadaiwa bila kufuata taratibu na kuwataka madalali nao walipwe na wanunuzi au mwenye mali kinyume na mikataba ya kazi.

Nashauri vyombo husika vilimulike hili kwani rushwa imetawala CRDB kitengo cha urejeshaji mikopo na kusababisha mikopo isilipwe kwa wakati kwa kukwamisha madalali kufanya kazi zao kwa kutolipwa 10% za madalali ambazo huzichukua wao kutoka kwenye fedha za mnada na kuwaelekeza madalali wakalipwe na wadaiwa au wanunuzi wa dhamana husika.
 
Duhhh naona unawachoma!

Afu Rushwa imejaa karibia kila sehemu!

Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
 
Hakuna hata cha kuhangaika, rushwa ndo style ya maisha, wale nchi hii, huo ndo urefu wa Kamba, wanakula ndani ya shughuli zao, mi nawapongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…