Kiteto: Tembo wamtoa utumbo aliyetaka kupiga nao ‘selfie’

Mtiti wowote wa mnyama akiuanzisha ni balaaa
Mm nilishakutanaga na mtiti wa mbuni .....
Ilikuwa chupuchupu

Ova
 
Pikipiki imemuokoa ila wanyama ni wakorofi sana kwenye vyombo vya moto hasa kama hawajavizoea.
 
Nasikia tembo anakimbia sana.. Wanasema ukikimbizana na tembo humalizi hata mita 20 amekudaka
Yaani acha tu kaka! Niliwahi ona kijana mmoja kule Lindi Liwale anakula ile pembe ya tembo! Jamaa alikua anawaswaga, sasa ule upepo ukarudi, tembo akanyanyua juu lile konga lake,kumbe ndo akanasa harufu, yule jamaa aligeuka kuanza kukimbia, dakika 1 ni nyingi mno! Jamaa alikula ile pembe! Akamshika na ule mkonga wako pigiza chini, kanyaga jamaa alikufa vibaya sana aiseee

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mpaka leo najiuliza na ule ukubwa na mwili mbio anazitoa wapi sipati jibu aisee
 
Amekoma angekufa kabisa umri huo hajui madhara anayoweza pata baada ya kumsogelea tembo
 
Nasikia tembo anakimbia sana.. Wanasema ukikimbizana na tembo humalizi hata mita 20 amekudaka
Tembo anakimbia zaidi ya kilomita 35 kwa saa Mkuu ni almost mara mbili ya spidi ya mwanadamu.

Na hautasikia kishindo wala nini zaidi ya sauti tu. Tembo ni kama paka anaweza kupita nyuma yako na usijue kama amepita hapo.

Adui wa Tembo ni kelele, ila ukitaka mfukuza ni pili pili tu kiboko yao
 
Yes nasikia pilipili au ukichoma maganda ya korosho ile harufu hapatani nayo kabisa. Kule Tunduru nilikuwa naona mashamba wamezungushia kamba imepakwa pilipili
 
Imejibiwa kisiasa sana, tembo wakiharibu shamba lako utalipwa fidia ndogo sana ila jaribu kuua tembo
 
Basi namuona kama mkubwa na mzito sana hawezi kukimbia, kumbe ni tofauti
 
Udom hilo eneo ilikuwa njia ya tembo miaka nenda rudi,wanadam ndy tumevamia maeneo yao
Mwanadam anajifanyaga kama yeye ndiyo Ana haki ya kuishi duniani pekee yake

Ova

Tembo bana ukiona wamekuja sehemu ujue yalikua mapito yao miaka nenda, miaka rudi na vizazi vyao wanakua wanajua kabisa yale ni mapito yao, sema binadamu ndio tumejikuta tunamaliza maeneo na kuwavamia wanyama
 
Yes nasikia pilipili au ukichoma maganda ya korosho ile harufu hapatani nayo kabisa. Kule Tunduru nilikuwa naona mashamba wamezungushia kamba imepakwa pilipili
hizo ndio njia ya asili ya kuwazuia, tatizo watu wanataka kufukuza Tembo kama wanafukuza mbuzi shambani 😂😂 Tembo hapendi kelele kabisa nafikiri na hao walileta shida sababu ya kelele za raia.

Japo kuna wataalamu wa kuwafukuza Tembo kwa kelele, yani anakerwaa hadi mwenyewe anasepa. Hao unaweza kukuta kijiji kizima yupo mmoja tena mzee kinoma
 
Unazijua zile mashine za kusaga za diesel. Zile zikiwashwa nasikia hakai tena hapo lazima asepe.. Sasa kwenye kukimbia ndio ukutane nae hapo balaa unalo
 
hii imekaa kama uongo mwaka ambao tembo walikuja UDOM ilikuwa 2017 kama sikosei ila hawakudhuru mtu zaid na zaid mali asili walikuja wakawatoa nilikuwa last year HUMANITIES
 
Utapigaje selfie na tembo?
Haya sasa mwana kulitaka mwana kulipata.
Apone haraka
"Mchuma janga hula na wa kwao".

Ujinga amefanya yeye wanaohangaika ni ndugu zake.
Hili ni fundisho kwa wengine.
 
Tembo ni balaa, mwanadamu hawezi kimbizana naye akamshinda lazima akuache mbali sana.

Tembo ni kibonge mwepesi 😂😂😂
Dah basi kumbe namchukulia poa, kuna nguruwe pori.... huyu mnyama ndio namuona balaa ana mbio huyo angekua ni binadamu basi ni mwanariadha kutoka Kenya 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…