Kiteto: Wamuua bodaboda na kunyofoa viungo vya mwili

Kiteto: Wamuua bodaboda na kunyofoa viungo vya mwili

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Watatu wakazi wa Kiteto mkoani Manyara akiwemo mwalimu wa sekondari Lesoiti, wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kiteto, kwa tuhuma za kumuua dereva bodaboda na kunyofoa baadhi ya viungo vyake kwa imani za kishirikina.

Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Novemba 28, 2022, baada ya jitihada ya Jeshi la Polisi Kiteto kufuatilia mawasiliano yao toka awali kabla ya mauaji hayo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 21, 2022, ambapo baada ya kutekeleza mauaji yao walinyofoa viungo hivyo vya mwili wake.

Shtaka hilo limetajwa na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uezo wa kusikiliza kesi hiyo na kesi imeahirishwa hadi Desemba 12, 2022.

muua.jpg
 
Kwa haraka haraka hapo, mwalimu ni huyo wa upande wa kushoto na aliyekaa peke yake!
Ila mwalimu ametia aibu sana. Mambo kama hayo yanawakuta watu wasio na elimu/maarifa ya kutosha kichwani!

Sasa mwalimu wa sekondari, tena mwenye elimu ya stashahada/shahada! Unaamini vipi katika mambo ya kishirikina kama hayo!!

All in all, mahakama ndiyo itakayo toa majibu ya mwisho. Iwapo ulishiriki kweli, au umetengenezewa zengwe.
 
Ushirikina! Umekuwa ugonjwa mbaya sana. Unadumaza akili na kuongeza umaskini kwa washirikina
 
watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa #mahakama hiyo haina uezo wa kusikiliza kesi hiyo na kesi imeahirishwa hadi Desemba 12, 2022.#

Mahakama imejuaje kama hawa jamaa ni watuhumiwa wa mauaji ya bodaboda? Sometime kodi zinatumika vibaya
 
Back
Top Bottom