Kiti cha Spika wa Muda Bunge Maalumu Kinatumika Vibaya

Kiti cha Spika wa Muda Bunge Maalumu Kinatumika Vibaya

Miimo

Senior Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
106
Reaction score
49
Wa Tanzania wenzangu,

Sipendi kuamini hata kidogo, kwa mamlaka aliyopewa Sipika wa muda kuongoza hili bunge katika kuunda kanuni anashindwa kutumia mamlaka aliyo nayo. Nguvu ya kiti cha bunge ni mhimili mkubwa sana katika kuongoza njia iliyo sahihi.

Babu yangu Mzee kificho, kwa uzoefu wako wa muda mrefu katika shughuli za kibunge, na umri wako huwezi kutuaminisha watanzania kuwa umeshindwa kutoa kauli na kusimamia kauli yako tu na kumaliza mgogoro wote kuhusu kura ya wazi au ya siri katika kupitisha maamuzi. Kwa kweli babu, umeonyesha busara sana ila kwa hili utastahili kulaumiwa kwa kupoteza muda na kufanya wabunge waendelee kula pesa zetu bila hata kufikia mwafaka katika kukamilisha hizo kanuni zote.

Ndio maana babu, nasema kwa umahiri wako, kushindindwa kuchukua nafasi yako kama kiti inaonyesha wazi kuwa nawe niwalewale ambao hutumika kutokana na maslahi ya makundi yao. Hivi babu, kama wewe ulipigiwa kura zilizosababisha kutoa maamuzi ya wewe kuwa katika hicho kiti, nashindwa kuelewa kabisa unapata kigumizi toka wapi kushindwa kutumia malaka uliyo nayo sasa kulekeza wajumbe wote wapige kura kama ile iliyokuweka kwenye hicho kiti ili kura hizo zitoe maamuzi yakuwa na kura ya wazi au siri. Na kusingekuwa na majadala hapo bali kitakachofuatwa ni matokeo ya hizo kura kwa principle ya wengi wape. Hilo lingewezekana na lingeokoa muda mwingi ambao umekwisha potea na mwafaka hajafikiwa. Kutangaza nafasi ya mwenyekiti wa kudumu kabla ya kukamilisha kazi uliyopewa, ni sawa na funika kombe mwanaharamu apite na historia itakuhukumu kwa hili.

Babu malaka hayo bado unayo na uwezo huo bado upo mikononi mwako, lakini kwa kuwa umeshaprove failure kutumia mamlaka ya kiti chako, na kwakuwa nikikutazama siami kama wewe kama wewe umeshindwa kutumia mamlaka yako bali ni zile sauti unazosikilza nyuma yako zinakuburuza nakufanya hata ile busara yako kufifia kiasi hiki. Kama hao wana haki zaidi ya watanzania million 45 kuwasikiliza, basi babu hatuna jinsi tena maana wewe unaondoka kesho tu, na umeamua kututosa wajukuu zako, na many vitukuu to come in 100years ahead! Historia hii lazima itakuhukumu tu na hutaikwepa.

kuwa kiongozi ni kuonyesha njia ambayo watu wengine wanatakiwa kuifuata, hili unalijua barabara lakini kwakua umeamua kuwa dhaifu nakuacha wachache wachukue mamlaka yako, basi tegemea mambo muhimu na nyeti ya rasimu ya katiba yatapitishwa tu katika hali ya vuvuzela vuvuzela kwa kuwa tu ulishindwa kutumia nafasi yako.

Kila la heri babu najua wewe umeshaingiza siku nono na unatetea kitumbua chako.
 
Huyu kificho kafichwa mfukoni na magamba,ameshindwa kazi.
 
Ninachopongezea Mheshimiwa Kificho ni jinsi alivyomudu bila kuwa na hasira,kisirani na kuonyesha uvumilivua hata pale alipopigwa na matusi au kejeli,sidhani kama ingekuwa Mama yetu angeweza muhemuko huu.Siyo kila kitu tuwe tunalaumu kwa kiasi ameweza kuwa mvumilivu sana.Hongera Mzee wetu,I wish ungekuwa Spika wetu kwenye bunge letu .
 
Back
Top Bottom