Juma Katolila
New Member
- Jun 1, 2020
- 4
- 10
Wakuu,
Inaonekana kuna mvutano mkubwa wa kisiasa katika Jimbo la Iramba Magharibi baina ya Profesa Kitila Mkumbo na Dk. Mwigulu Nchemba.
Kitila bado hajatangaza hadharani endapo kweli anataka nafasi hiyo. Mwigulu, angalau kashatangaza 'kiaina' kwa kujigamba kwamba anayetaka kupima urefu wa kina cha maji aende Iramba kushindana naye.
Hata kama Kitila mwenyewe hajatangaza hadharani nia yake, ripoti za vyombo mbalimbali vya habari vinatuelekeza katika dhana ya Lisemwalo lipo.
Kama kweli hatimaye Kitila ataamua kutangaza hadharani kwenda kushindana na Mwigulu, itaashiria vita kali ya kuwania nafasi hiyo.
Sioni ni kwa namna gani CCM itafaidika na mchuano wa wawili hawa. Vita itakuwa kali sana.
Hofu yangu ni kwamba, vita itakuwa kali kiasi kwamba mwisho wake CCM itashindwa.
Hii ni kwa sababu, kuna kila dalili kuwa wafuasi wa Kitila au Mwigulu wataamua kumsaidia mgombea wa upinzani ili kumkosesha ushindi aliyekuwa mshindani wake ndani ya CCM.
Ushindi wa Kitila au Mwigulu pale Iramba utakuwa ni ushindi wa ki pyrrhic. Kwamba gharama za ushindi ni kubwa kiasi sawa na kushindwa.
Kwa anayefuatilia siasa za Rais Magufuli, yeye ni mtu ambaye ushindani wa namna hii kwenye chama.
Mara zote anataka kuona chama kinachozungumza lugha moja.
Kwa sababu hii, ningeshauri Profesa Kitila, kama kweli ana nia ya ubunge, asogee kwenye Jimbo la Ubungo lililopo Dar es Salaam.
Jimbo hilo sasa ni la upinzani na halina mwenyewe ndani ya CCM wala hakuna dalili za mtu kujitokeza kulichukua toka Upinzani.
Kwa sababu Kitila anafahamika na watu wa Dar es Salaam, ni mwanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mtu ambaye ni rahisi kwa sera zake kueleweka na watu wa Ubungo, itakuwa na maana kubwa kumsaidia Rais kwa kuwania Ubungo.
Itapunguza ugomvi na kuongeza kura za CCM kule Iramba, itajenga mshikamano ndani ya chama na kuongeza wigo wa watu wazuri wa kuwa nao chamani na serikalini.
Kwa kumsaidia Rais Magufuli, CCM na serikali kwa ujumla, Kitila anatakiwa kuachana na Mpango wa Iramba; Kama anao, ili aepushe mabaya dhidi yake na chama chake.
Ubungo kupo. Kunamsubiri