WanaJF
Habari ambazo zinaenea ni kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Dr Kitila Mkumbo anajiandaa kugombea ubunge Iramba Magharibi 2020 kupitia CCM.
Taarifa za uhakika kutoka kwa watu kadhaa wa karibu na Dr Kitila ni kwamba kiongozi huyo aliyejitenga na ACT hivi karibuni anatarajia kujiunga CCM siku si nyingi kutoka sasa.
Baadhi ya viongozi wa CCM Iramba Magharibi wamegawanyika makundi mawili huku kundi moja likimuunga mkono Mwigulu Nchemba mbunge wa sasa na kundi lingine likimuunga mkono Dr Kitila.
Dr Kitila amekuwa akilitamani kwa udi na uvumba jimbo hilo tangu akiwa Chadema ila kizingiti kikubwa kilikuwa Mwigulu Nchemba.
Kwa sasa Dr Kitila ana uhakika wa kumuondoa Mwigulu kwa kile kinachosemekana anaungwa mkono na ngazi za juu