Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Kash kash zimeanza rasmi sasa!
=====
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Januari 1, 2025, amewahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Ubungo katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Ubungo Plaza.
Pia soma: Orodha ya CV za Wabunge kwa mwaka 2020 - 2025 kutoka kila mkoa Tanzania
Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo ameeleza dhamira yake ya kugombea tena nafasi ya ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2025, huku akitoa onyo kali kwa watu wanaonyemelea jimbo la Ubungo.
"Sasa mimi niseme mambo mawili, kwasababu katika hizi harakati kuna watu wanapitapita, mimi ni mzoefu wa mapambano ya kisiasa, kama umeamua kugombea, gombea sawasawa bila ujanjaujanja", ameeleza Prof. Kitila.
Ameongeza kuwa uchaguzi ni sawa na vita, na kwamba yeye binafsi amejiandaa kikamilifu kwa ushindani wa mwaka 2025.