Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Januari 1, 2025, amewahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Ubungo katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Ubungo Plaza.
Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo ameeleza dhamira yake ya kugombea tena nafasi ya ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2025, huku akitoa onyo kali kwa watu wanaonyemelea jimbo la Ubungo.
"Sasa mimi niseme mambo mawili, kwasababu katika hizi harakati kuna watu wanapitapita, mimi ni mzoefu wa mapambano ya kisiasa, kama umeamua kugombea, gombea sawasawa bila ujanjaujanja", ameeleza Prof. Kitila.
Ameongeza kuwa uchaguzi ni sawa na vita, na kwamba yeye binafsi amejiandaa kikamilifu kwa ushindani wa mwaka 2025.
Jimbo la Ubungo lina shida kubwa kwenye upatikanaji endelevu wa huduma ya maji pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara (mfano ile ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi & Kimara - Matosa). Anahitajika Mbunge mwenye ushawishi mkubwa na mbinu za kufanikisha haya mambo
Sina uhakika kama Kitila Mkumbo anaweza kuyafanikisha haya mambo ila nina uhakika mgombea wa Ubunge kutoka Chama cha Upinzani hatoweza kuyapigania mpaka yakatokea - let alone kuconvince wapiga kura, especially if vyama vitaleta wapiga kelele kama Boni Yai
Badala ya kutumia muda huu ambao Kodi zetu zinamlipa kufanya mambo anaongelea kugombea..., Ingekuwa ni kunufaisha wananchi angefanya hivyo sasa sababu anawigo wa kufanya hivyo..., ila ndio hivyo kama kawaida ya hivi so called vyama vya siasa ila ukweli ni platforms za kutafuta Kura ili kwenda Kula
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Januari 1, 2025, amewahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Ubungo katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Ubungo Plaza.
Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo ameeleza dhamira yake ya kugombea tena nafasi ya ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2025, huku akitoa onyo kali kwa watu wanaonyemelea jimbo la Ubungo.
"Sasa mimi niseme mambo mawili, kwasababu katika hizi harakati kuna watu wanapitapita, mimi ni mzoefu wa mapambano ya kisiasa, kama umeamua kugombea, gombea sawasawa bila ujanjaujanja", ameeleza Prof. Kitila.
Ameongeza kuwa uchaguzi ni sawa na vita, na kwamba yeye binafsi amejiandaa kikamilifu kwa ushindani wa mwaka 2025.
Jimbo la Ubungo lina shida kubwa kwenye upatikanaji endelevu wa huduma ya maji pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara (mfano ile ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi & Kimara - Matosa). Anahitajika Mbunge mwenye ushawishi mkubwa na mbinu za kufanikisha haya mambo
Sina uhakika kama Kitila Mkumbo anaweza kuyafanikisha haya mambo ila nina uhakika mgombea wa Ubunge kutoka Chama cha Upinzani hatoweza kuyapigania mpaka yakatokea - let alone kuconvince wapiga kura, especially if vyama vitaleta wapiga kelele kama Boni Yani
Labda arudi Mnyika lakini Boniyai ameshaharibu kujianika kuwa yuko upande gani kwenye mtanange wa kiti cha taifa. Hata ashinde Sultan hana uwezo wa kumpatia kura boni amejitia dole mwenyewe.