Kitimoto is overrated haina utofauti wala utamu kuliko nyama zingine..

We kitimoto huijui, mmeuziwa mifuta mingi la hasha hujui kuipika. Ile inapikwa na mafuta yake babu kisha inarostiwa kiufundi unaweza shangaa watu kadhaa mkafuta kilo ya ugali
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Siku ukija kwangu ntakupikia kitimoto ya maana utakuja hadithia humu. Raha ya kitimoto ipikwe,ikaangwe kwa mafuta yake,irostiwe na mtaalamu sio ile imejazana mimafuta tele,nyama laini lain. Inatakiwa iwe ngumu kavuuu
Fundiii, aisee nataka nichukue uber niwasili ulipo. Chukua kilo na nusu, nakuja kulipa anza kufanya mambo mkuu.
 
Hivi mwaipendea nini au yale mafuta? Mm naona kuku is the best nyama ever πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Yale mafuta ni layer tu ya juu. Kuna nyama yenyewe... ile misuli yenyewe. Kaanga na vitunguu alaf unipe mrejesho
 
Da vinci, natoa ofa. Nakupeleka mianzini kwa mahali wanakaanga hiyo kitu kwa kiwango cha kimataifa. Nakwambia haya mawazo utabadili mzeya
Naomba hiyo ofa Comrade labda nitabadir mtazamo wangu
 
Pole mkuu, mm ni msabato, hii kitu imepigwa stop kabisa, afadhali kwa waislam ukiwa na njaa na hakuna chakula kingine unaweza kula. Ila katika usabato ni stop sijaona kama kuna option. Hii kitu nlilishwa bila kujua miaka ya 2002 maeneo ya banana ukonga na washkaji zangu. Baada ya hapo nikawa naila kinoma sababu nligundua ukiondoa nyama ya swala tu kati ya nyama tam nlizowahi kula, basi kitimoto hakuna nyama ingine inayokaribiana na hii nyama
 
Kama kutakuwa na hukumu kwa waliokula nguruwe

1. Wazungu mambo bacon na sausages bila kusahau Sunday roast.

2. Wabrazil mambo ya roast pork na green plantains

3. Wachina hapo usipime.

4. Wachagga, hawa wakwe zangu kiti moto ni sehemu ya maisha ya kila siku

Matthew 7:2
For the same way you judge others, you will be judged and for the measure you use it will be measured to you.
 
Dada angu mm hata sijahukumu mtu na imani yangu hainiruhusu kabisa..
Hoja ni Pork ina u special gani? Maana inasifiwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…