MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Somewhere in Kigogo Sambusa....
Katika utulivu wa hali ya juu najiuliza haya maisha yangekuwaje bila kitimoto rost, ndizi mbili na kachumbari pembeni? Kungekua na mbadala wake?.... nikiwa ndani ya tafakuri nzito, namwona Dada nadhifu na mrembo akisogelea mezani kwangu kashikilia sinia lenye kitimoto safi imeiva kiwango cha juu.. ni ufundi wa Shirima. Anafika na kuninawisha mikono kisha kutenga vitu na kuanza kuondoka na sinia. Wakati akiondoka namsihi aniletee Pepsi ya baridi.
Basi kazi ikaanza taratibu, yaani one-touch, finyango baada ya finyango. Ile ndo mwendo unaanza kushika kasi, mara ghafla simu ikaanza kuita..... nikajiuliza kwa hasira ni nani huyu anayeweza kunipigia nikiwa kwenye starehe kama hii??..π¬π‘π‘..
Sasa wakati naitoa simu mfukoni kwa bahati mbaya ikaniponyoka.... kwenye harakati za kuiwahi isianguke nikajikuta nimesukuma ile meza ya plastic.... KITIMOTO yote na ile soda ikamwagika.. Aaarghh!!π¬π¬.. kuja kukaa sawa tayari yule mdada kashafuta meza na kusafisha pale chini huku akidai chake......