Habari zenu ndugu wana JF. Ningependa kuuliza kama mnafahamu kuhusu huu ugonjwa kitoto cha jicho ni nini, na unatokana na nini na matibabu yake ni nini? Mzee wangu amepatwa na maumivu makali jicho moja na amenieleza kuwa amepata huo ugonjwa. Nitashukuru sana kama mnaweza kunisaidia kwa ushauri au hata sehemu anapoweza pata matibabu mapema kabla mambo hayajawa magumu.
Natanguliza shukrani, Aluta!
Hii leo nimepata msg yako ingawa nimeipata "late" nataka kukuuliza tu kama umeshapatiwa jibu! Kama umeshapatiwa au bado lakini usimpeleke kwa Dr. Mtanda kwa matibabu hayo kwani....!!! Nifahamishe kama umeshapatiwa jibi kama bado nitakupatia na kukufahamisa wapi umpeleke mzee wako. Heshima mkuu.
Mimi nina matatizo ya macho na nakusudia kwenda kwa huyu daktari kwa vile nimepata sifa zake tele.Mlokole nijulishe kwanini umemkataza jamaa asimpeleke baba yake huko?.Hii leo nimepata msg yako ingawa nimeipata "late" nataka kukuuliza tu kama umeshapatiwa jibu! Kama umeshapatiwa au bado lakini usimpeleke kwa Dr. Mtanda kwa matibabu hayo kwani....!!! Nifahamishe kama umeshapatiwa jibi kama bado nitakupatia na kukufahamisa wapi umpeleke mzee wako. Heshima mkuu.