SoC02 Kitu cha msingi ambacho wengi tunakikosa katika kuyafikia mafanikio katika kila nyanja

SoC02 Kitu cha msingi ambacho wengi tunakikosa katika kuyafikia mafanikio katika kila nyanja

Stories of Change - 2022 Competition

Gody2809

New Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Kila mtu anatamani kufanikiwa katika kila jambo lakini ni wachache wanaoyafikia mafanikio na kuonekana wenye bahati sana. Ulishawahi jiuliza kwanini kuna watu wanaumwa magonjwa yanayosemekana hayaponi lakini wako wanaopona hayo magonjwa? Au kwanini kuna watu wanafanikiwa kwenye biashara flani lakini wengine hawafanikiwi? Wengi wetu hudhani kua hawa wanaofanikiwa wana kitu special ambacho sisi hatuna lakini ukweli ni kwamba kila mtu ana kila kitu anachohitaji ili afanikiwe. Kinachotutofautisha ni ujuzi wa kitumia tuliyonayo. Moja ya kitu kikubwa sana ambacho kila mtu anaweza kukitumia kufanikiwa ni akili (mind). Naam hujasoma vibaya kabisa, kila mtu ana akili na kinachotutofautisha ni namna ya kuzitumia.

Akili (mind) imegawanyika katika pande mbili sitaweza kuzitaja kwa kiswahili fasaha lakini pande hizo mbili ni CONSCIOUS MIND na SUBCONSCIOUS MIND. Conscious mind ni akili inayohusika katika utambuzi wa mambo na hii inatumia milango mi5 ya fahamu. Lakini Subconscious mind ni akili inayohusika kuendesha mambo mwilini bila utambuzi. Mfano mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula ,kuratibu tabia n.k.

Conscious mind hua inapeleka taarifa kwenye subconscious mind na subconscious mind inaziratibu taarifa hizo. Maneno na imani tunazojengewa katika mazingira yetu kwa kujua ama kutokujua hufanya subconscious mind ikubali kua ni kweli hata kama imani hizo ni za uongo ama maneno hayo ni ya uongo. Mfano kitu chochote unachosema huwezi kufanya, subconscious mind yako itakubali kua kitu hiko huwezi kufanya na kama unenavyo kitu hiko hutaweza kufanya. Jiulize ni kitu gani ulisema na kuamini kua hutaweza kukifanya na ukaweza?. Magonjwa , kushindwa na mambo hasi yote sio asili ya mwanadamu, ndio maana kuna kanuni za utajiri lakini hakuna kanuni za umaskini, kuna kanuni za afya lakini hakuna kanuni za kuumwa magonjwa, kuna kanuni za upendo lakini hakuna kanuni za chuki, kuna kanuni za kupata amani, lakini hakuna kanuni za kupata msongo wa mawazo. Na mambo hasi yote yanatutokea sababu ya yale tunayoamini zaidi. Ukiamini katika uchawi, ndipo utaona kila sehemu unarogwa, ukiamini katika magonjwa ndipo utaona dalili za kila aina.

Tunaishi katika dunia mbili ambazo zinahusiana sambamba. Dunia hizo ni dunia tuionayo na dunia iliyopo ndani yetu. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba. Kila kinachokuzunguka katika dunia uionayo kilianza kwenye dunia ya ndani yako. Maana yake ulivyo ndani ndivyo ulivyo nje. Hapa nazungumzia fikra zetu. Sitaki kuleta udini katika makala hii lakini mithali 23:7 katika biblia imeandika “ mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo”. Hii ikimaanisha mawazo yako ndio imani yako na jinsi unavyoamini ndivyo ilivyo kwako. Dunia ya ndani ndio sababu ya matokeo ya nje. Na cha kushangaza ni kwamba wengi tunajaribu kubadirisha matokeo ya nje angali bado hali ya ndani ni ile ile ya zamani.

Subconscious mind hutunza taarifa zozote zinazokuja kwa njia ya maneno ama mawazo na kuzipokea kua ni kweli. Na kuanza kutendea kazi. Chukulia Subconscious mind yako kama bustani na chochote unachopanda kwa maneno au mawazo kinastawi, haijalishi ni kibaya ama kizuri. Mawazo na maneno hasi kwa wengi wetu ni matokeo ya mazingira tuliyokulia lakini una nguvu ya kubadirisha hayo. Wapo watu ambao wamejazwa fikra kua kuna mambo wao hawataweza amahayawezekani nao wakaamini hivyo angali wapo watu wanaofanya mambo hayo hayo na wamefanikiwa. Watu kama hawa wameotesha magugu katika dunia yao ya ndani na kamwe hawataweza ona matunda mazuri kwenye dunia ya nje.

Habari njema ni kwamba bado hujachelewa kubadirisha dunia yako ya ndani na nitakupa mbinu za kubadiri hayo punde tu. Lakini kumbuka huwezi badirisha dunia yako ya nje kama ndani yako bado hakujabadirika. Nimekua nikijifunza haya kwa muda sasa na ninaona matokeo mazuri yakiendelea kutokea. Nimeona nikipona magonjwa kadhaa bila kutumia dawa yoyote (sisemi dawa hazifanyi kazi ama usinywe dawa, hii ni mfano tu Hai ambao mwenyewe nimepata uzoefu nao), pia mzunguko wa fedha umekua mkubwa kulinganisha na mwanzo. Na mengine mengi siwezi yataja yote. Zifuatazo ni mbinu unazoweza tumia kubadiri mazingira yako ya ndani na kuamini katika mambo chanya.

1. ZINGATIA MANENO UNAYOTAMKA JUU YAKO MWENYEWE

Subconscious mind yako haitambui kua unayotamka ni sahihi ama si sahihi , kazi yake ni kuyapokea na kuyafanyia kazi hata kama unayoongea ni kwa utani tu. Ukisema huwezi kitu flani basi subconscious mind yako itakubali kua ni kweli, ukisema huna pesa, subconscious mind yako itakubali kua ni kweli na utaona uhaba wa pesa ukikuandama. Njia nzuri ya kutumia ni kuanza kua na tabia ya kujitamkia maneno chanya. Jiambie wewe ni mshindi, jiambie wewe unaweza mambo yote,, jiambie wewe unahaki ya kufanikiwa, jiambie wewe una haki ya kua na afya wakati wote, jiambie umepona gonjwa ulilonalo mpaka maneno yako yawe imani na subconscious mind yako iyashike.

2.KUA MAKINI NA YALE UNAYOPOKEA KATIKA MILANGO YAKO YA FAHAMU.

Kama una marafiki ambao wana fikra hasi, jaribu kuwaepuka sababu unapoandamana na walevi tisa , ni wazi kua unaweza kua mlevi wa kumi. Zingatia pia mitandao ya jamii unazofatilia, hakikisha inakupa kitu chanya na sio vitu vinavyokupa stress, tamaa, uoga n.k

3.KUA NA UTARATIBU WA KUONA NA KUHISI MAMBO UNAYOTAMANI YATUKIE.

Nguvu ya kuratibu mawazo yako unayo mwenyewe ,kua na tabia kabla ya kulala kutengeneza picha mawazoni mwako ya kitu unachotaka kitukie, tengeneza taarifa nyingi mawazoni mwako kama mazingira yatakavyokua, watu wakiongea ama kucheka, rangi za nguo n.k. mfano unaumwa na umelazwa, tengeneza picha baada ya kupona kwako, muone daktari mawazoni mwako akikwambia umepona, ndugu na jamaa wa kifurahia kupona kwako n.k kama unataka kufanikiwa kwa biashara basi jione mawazoni mwako kua unahudumia wateja , watu wakikusifia kwa huduma ama bidhaa zako n.k. pia jitahidi kuhisi ile amani ama furaha utakayokua nayo pale mambo hayo yatakapotukia kwani subconscious mind yako haijui tofauti ya dunia yako ya nje na ya ndani.

Kwanini usiku kabla ya kulala ndio muda mzuri wa kufanya tathmini? Hii ni sababu subconscious mind yako hailali hata siku moja, lakini ukilala milango yako mi5 ya fahamu haitaweza kukufanya ukapata mashaka muda huo kwamba mambo hayo yatatukia.

Kwa kuhitimisha niseme kwamba imani ni mawazo ya akili yako, na mawazo yanaletwa na maneno tunayosema ama kusikia, kwahiyo maneno uyasemayo ama kusikia yanaleta mawazo ambayo yanabadirika kua imani. Na unachoamini ndicho unapata maishani mwako. Usikazane kubadirisha matokeo ya nje bila kubadirsha hali yako ya ndani. Badilisha mawazo yako, ubadilishe maisha yako. Asante
 
Upvote 1
Back
Top Bottom