Mwanafunzi mtoro
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 222
- 806
Habari waungwa sana wa JF
Leo nimeona nami nijaribu kushea tukio moja ambalo kila nikikumbuka nabaki kusema ni mungu tu.
Siku hiyo asubuhi naelekea stendi kupanda gari ya kuelekea Dar es salaam. Siku moja kabla ya safari nilitanguliza mizigo miwili ya kukaa kwenye buti. Sasa asubuhi nilibeba begi la mgongoni tu hadi stendi . Nilipofika booking office nililiacha begi ndani kisha nikatoka kwenda kukojoa.
Kwakuwa stendi haikuwa Mwanza mjini basi tulikuwa tunasubiri iingie stendi ndogo ili tupande. Wakati narudi tu toka kichakani ghafla basi likawa limeingia. Katika harakaharska tukaifata mizigo miwili tukaweka kwenye buti kisha nikapanda ndani ya gari.
Wakati gari inakaribia maeneo ya Hungumalwa ndio nakumbuka begisikupanda nalo kwenye basi na wala halipo kwenye buti. Nilihisi kuzimia .Nilihisi labda begi nililisahau wakati wa kupakia mzigo kwenye buti nilizidi kuchanganyikiwa nilihisi mwili unaganda.
Begi sio kitu kilichonichanganya bali kwenye begi kulikuwa na laki 8+ . Pesa hizi nilisahau kuingiza kwenye akaunti baada ya kuagiza bidhaa flani kisha kusubiri kama zitapatikana zingine nitume tena . Nikaona haina haja kuweka mfukoni kwakuwa begi nipo nalo acha niweke huko .
Nikajipa utulivu kisha kumfata dereva anishushe. Wakati anatafuta mahali pa kunishusha nikawa nawasiliana na ajenti ambaye tunafahamiana sana. Akanambia nimelisahau kwenye ofisi..hapo nikapumua. Kisha baada ya hapo nikamweleza hilo begi lina pesa.
Nashukuru alipata basi la kunifukuzia hadi niliposhuka. Na hilo basi ndio nilipanda mimi kuendelea na safari.
Hasara ndogo niliyopata ni kuwa basi la kwanza nililipia mizigo ga kwenye buti elfu 10. Kisha karudishiwa elfu 15. Basi la pili nililipa elfu 30 kwakuwa nilikuwa nashuka Morohoro
Tupe mkasa wako na wewe ni kitu gani ulisahau na ukakipata?