Kitu gani hasa kimekuwa na mchango mkubwa katika Uchumi wa Tanzania kati ya Filamu ya Royal tour na Ufufuaji wa shirika la ATCL

Kitu gani hasa kimekuwa na mchango mkubwa katika Uchumi wa Tanzania kati ya Filamu ya Royal tour na Ufufuaji wa shirika la ATCL

King_Villa

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2012
Posts
575
Reaction score
380
Habari za wasaa wakuu.

Wakuu leo nilikuwa natafakari mwendo wa Uchumi wetu katika nyanja hizi mbili ila nikaona niwashirikishe wadau wa JF nione maoni yao .

Ila kwanza nianze na tafakari zangu binafsi kwa pande zote .

1.The Royal tour inamchango mkubwa kwasababu nchi yetu bado Uchumi wake uko chini kujiendesha yenyewe kwa asilimia 90.hivyo tunahitaji wawekezaji ili wanapowekeza waongeze Chachu katika Uchumi na Kwa namna nyingine hawawezi kuijua Tanzania bila kuitambulisha kwao hasa katika vivutio vya kitalii. Mfano Tajiri wa china atakapoiona Royal tour na akatamani kuja kutazama vivutio anaweza akahamasika kuwekeza kwetu nasi tukapata kodi,Ajira na vingine vingi.


Kwa upande wa Ufufuzi wa shirika la ndege(ATCL) naona pia sio mbaya kwasababu watalii wengi wataweza kusafirishwa kuja nchini na pia Ajira zitaongezeka Pia usafiri utakuwa wa uhakika hasa katika soko la ndani.

Asanteni wakuu
new-airbus-bombardier-planes-national-carrier-tanzania.jpg

download (4).jpeg
 
Back
Top Bottom