Fedha Ni bidhaa ambayo kiujumla hutumika katikati ya miamala mingine, (kwa maana kwamba unatafuta fedha ili kuhifadhi nguvu yako ya kimanunuzi, manunuzi tunayafanya pale matamanio yetu yanapoizidi thamani fedha tunayomiliki, kwa mfano:- unamiliki tsh 20,000/=, sokoni Kuna kiatu kinauzwa tsh 20,000/=, matamanio ya kiatu yanapoizidi thamani fedha ndipo unapoamua kutoa fedha iliyopoteza thamani ili upate kiatu. Na thamani ya fedha ipo kwenye upatikanaji wake!, fedha inapokuwa nyingi kwenye mzunguko thamani yake hushuka Na ndipo hapo fedha nyingi hutumika kununua mahitaji kidogo, Na fedha inapopungua kwenye mzunguko thamani yake hupanda Na hapo fedha kidogo hutumika kununua bidhaa nyingi. Kitu kinachotumika kuthibiti thamani ya fedha kwenye mzunguko Ni sera za kifedha za benki kuu (monetary policy)(kwa mfano:-RIBA), Na sera za kibajeti(fiscal policy), riba inapopanda wafanyabiashara wanapunguza kukopa Na kuwekeza, pia serikali inapoongeza makusanyo yakodi hivyo fedha kwenye mzunguko/kupunguza matumizi, riba ikishuka wafanyabiasha hukopa zaidi na/au serikali ikipunguza kodi kodi/kuongeza manunuzi fedha huongezeka kwenye mzunguko hivyo thamani yake hushuka!. Hii Ni kwa mzunguko wa ndani.
Kwa mzunguko wa nj'e fedha huuzwa dhidi ya fedha ya nchi nyingine kutegemeana Na mahitaji. Tunapomiliki (kwa mfano US dollar) nyingi baada ya kuuza bidhaa zetu nj'e mahitaji yetu kwa US dollar hupungua hivyo thamani ya fedha yetu hupanda dhidi ya US dollar , lakini tunaponunua bidhaa nyingi kutoka nj'e mahitaji yetu kwa US dollar huongezeka hivyo thamani yake hupanda dhidi ya fedha yetu, Na kinyume chake Ni hivyohivyo!. Wenye ujuzi zaidi wataongezea/kosoa nipopungua/kosea!, Nawasilisha.