Kitu gani kimeikumba WhatsApp?

Kitu gani kimeikumba WhatsApp?

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Habari!

Kuna tatizo limeonekana kujitokeza la kutotuma wala kupokea jumbe zozote zile katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp hivi sasa ninapoandika uzi huu.

Hili tatizo linatajwa kuwakumba watumiaji wa mtandao huu sehemu mbalimbali duniani na hata mimi kwa upande wangu nimelishuhudia tatizo hilo.

Je, kuna yeyote ambaye ameliona tatizo hili ama kuna ambaye WhatsApp yake haina hili tatizo?

Tujuzane!

====

1579441504525.png
 
Hakuna mtandao wa hovyo kama wasap, watu wanapoteza muda kutumiana jumbe na vitu vya kipuuzi, sitaki kabisa kutumia huo mtandao hasa baada ya kugundua kuna wale viherehere wanaokuunga kwenye ma group bila ridhaa yako.
 
Mimi simu moja ninayotumia haina shida ila kuna Tecno ambayo ina WhatsApp groups ilikataa tangu January 4 nikajua ni simu kimeo tu nikaachana nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo, kuna baadhi ya matoleo ya simu hususani ya zamani yalizuiliwa kutumia WhatsApp, hilo linafahamika.

Lakini, hili tatizo la leo ni jipya kabisa.
 
Back
Top Bottom