Kitu gani kimewahi kukuhuzunisha sana?

Kitu gani kimewahi kukuhuzunisha sana?

daxy Jr

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
88
Reaction score
307
Kwenye picha chini ni mvulana wa miaka 10 kutoka Ghana aliyekufa kwa Saratani. Wazazi wake hawakuwa na pesa ya matibabu hivyo alikaa nyumbani hadi hali yake ilipokua mbaya zaidi, na kubaki na siku chache za kuishi.

Akiwa hospitalini, aliomba hsopitali imsaidie kutimiza ndoto yake ya kupanda ndege kabla hajafa. Hospitali hiyo ilimsaidia kutimiza ndoto yake.

Hisia ya kujua kwamba utakufa hivi karibuni inavunja sana moyo wangu💔

boy3.jpeg
boy2.jpeg
boy1.jpeg
 
Hivi hao wahudumu walikuwa na sababu ya msingi kweli ya kupiga picha za selfie na huyo mtoto huku wakiwa na nyuso za bashasha!! Wamenikera sana. 😡
 
Mimi naona wangeweza kuendelea kumsaidia kwenye mambo ya maana kama elimu. Wangeweza kuchangisha au kuomba scholarship kwenye hiyo kampuni ya ndege.
 
Wakati wake ulikua umefikia ukomo na hapakua na namna yeyote tena ya kumsaidia zaidi ya kusubiria kifo
 
Kujua kwamba utakufa baada ya muda fulani ni jambo jema ukilinganisha na kifo cha ghafla.
 
Ukiachana na mgonjwa wengine wote kwenye self ǝƃuǝsɐM
 
Kwenye picha chini ni mvulana wa miaka 10 kutoka Ghana aliyekufa kwa Saratani. Wazazi wake hawakuwa na pesa ya matibabu hivyo alikaa nyumbani hadi hali yake ilipokua mbaya zaidi, na kubaki na siku chache za kuishi.

Akiwa hospitalini, aliomba hsopitali imsaidie kutimiza ndoto yake ya kupanda ndege kabla hajafa. Hospitali hiyo ilimsaidia kutimiza ndoto yake.

Hisia ya kujua kwamba utakufa hivi karibuni inavunja sana moyo wangu💔

View attachment 2666157View attachment 2666158View attachment 2666160
Inaskitisha sana, anyway.. Hiyo ni natural selection
 
Back
Top Bottom