Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kutokana na kauli alizotoa mfululizo katika siku chache zilizopita, mtu yeyote hana budi kujiuliza swali, kulikoni tena Dkt Bashiru amepoa na kutaka kujirudi hadi "kutamani" Membe aweze rejea CCM?
Ametamka mwenyewe Dkt Bashiru, akiwasihi wanaccm wenzake, wasisheherekee kufukuzwa kwa kada maarufu wa Chama hicho cha CCM, Bernard Membe, kwa kuwa kumpoteza mwanachama maarufu kiasi hicho kwenye chama ni msiba mzito!
Ameendelea kusema kuwa yeye mwenyewe amesaini barua 14 za wanachama waliotimuliwa CCM na wakaomba msamaha na kurejea tena CCM, kwa hiyo anaisubiri kwa hamu sana barua ya Membe ya kuomba msamaha na hiyo itakuwa barua ya 15 kuisaini na kumrejesha "mwana mpotevu" kundini!
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi hii U turn ya Dkt Bashiru, imetokana na nini?
Si ndiyo hao hao CCM walikuwa wakitamba kwenye majukwaa ya kisiasa, wakimtukana Membe, kuwa chama cha CCM, kuwa ni "baba lao" kwa hiyo hakuna mwanachama, anayeweza kujiona yuko juu ya Chama?
Hivi kumbe chama hicho cha CCM kinatumia vitisho kuwatimua wanachama wake, kikijua kuwa hawajafanya makosa yoyote na baadaye kutegemea wanachama hao watapiga magoti na kuomba msamaha ili warejee kwenye chama chao?
Ina maana baada ya kupima upepo wa kisiasa unavyovuma, huku ukizingatia kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, ndipo Dkt Bashiru ameshituka na kuona hatari kutokana na vitendo vyao vya visasi, vilivyosababisha Membe avuliwe uanachama wake?
Kumbe CCM wameanza utamaduni mpya wa kidemokrasia kwenye Chama Chao, ambapo kuonyesha nia ya kutaka kugombea Urais kwenye chama hicho, inahesabika kuwa ni kosa kubwa la jinai, ambapo unaweza hata kustahili kufukuzwa kwenye chama hiko?
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Membe hakuwa na kosa lolote la kufanya Chama hiko kimfukuze uanachama wake na ndiyo sababu zinazofanya Dkt Bashiru ajutie nafsi yake ya "kutumika" kumtoa Membe, kwa kosa tu la kuonyesha nia ya kugombea Urais, ndani ya chama cha CCM, kwenye uchaguzi wa mwaka huu wa 2020
Hivi tangu lini mtu kuonyesha nia ya kutaka kugombea Urais kwenye Chama cha CCM, ikawa kosa kubwa, hadi kusababisha mtu kuweza kufukuzwa kwenye chama hicho?
Tujiulize swali jingine dogo, hivi ni kwanini hao kina Membe, waliolalamika kuwa huyu Musiba ni nani ndani ya nchi hii, hadi "aruhusiwe" kuwatukana viongozi wakubwa wa CCM, waliostaafu kadri atakavyo na vyombo vya usalama wa nchi, vipigwe "ganzi" na kuogopa kumchukulia hatua zozote za kishetia?
Maswali yako mengi yanayokosa majibu, lakini itoshe kwa hayo maswali machache, niliyoyaorodhesha, ambayo nimeuliza ni kwanini Dkt Bashiru, akose raha kabisa, kwa kumfukuza Membe, kwa sababu tu ya kuonyesha nia ya kutaka kugombea Urais kupitia CCM, kuwa ndiyo kosa lake kuu, lililomfanya mwanachama huyo Membe, apoteze uanachama wake?