Kitu gani kinafanyika Kenya hakifanyiki Tanzania?

Kitu gani kinafanyika Kenya hakifanyiki Tanzania?

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Wanabodi naomba tujiulize na kujadili bila ushabiki wa kivyama. Hivi ni nini hasa kinachofanyika Kenya ambacho hakifanyiki Tanzania kiasi cha kuwafanya vijana wetu kuona tuko sawa wala hatuhitaji kufa kwa ajili ya kesho yetu?

Vijana Kenya wanalalamikia Uhuni katika Tume ya Uchaguzi, IEBC. Sisi tuko salama na tume yetu? Kenya wanalalqmikia bajeti ya kifisadi, je sisi tuko tofauti? Kenya wanalalamikia kupanda kwa gharama za maisha maradufu ilhali genge la wachache wakiogolea ukwasi pesa za walipakodi. Je, sisi tuko salama kiasi cha kutokuona haja ya kuwawajibisha watawala kungali mapema na si kusubiri uchaguzi?

Kenya wanalalamika mke wa Rais kupangiwa na kutengewa bajeti fedha ya kumhudumia na misafara ya magari. Tumeasahau mafao kwa wenzi wa viongozi iliyopitishwa na Bunge? Hivi kuna watu wenye maisha magumu kwa sasa Afrika Mashariki kama vijana wa Tanzania wasio na ajira?

Kwa vijana wetu hawaguswi na hali hiyo ili wawe tayari kupoteza maisha ya dhiki kesho wenzao waishi maisha ya ahueni? Kwa nini woga? Ni mpaka lini woga? Hivi kuna nchi hapa EAC ambayo hela ya umma inachezewa na Watawala kama Bongo? Nani kawafunga hirizi vijana wetu kuamini kwamba hawawezi kuwafurusha mafisadi madarakani? Kwa nini hawawezi kusema, "enough is enough "?

Tuwaamshe vijana wetu waone damu yao inaweza kuleta ukombozi nq mqbqdiliko chanya sasa siyo kesho. Amina.
 
Back
Top Bottom